Dharau za Rais wa Ukraine ni za level nyingine, anawakoromea Marekani nyumbani kwao. Angalia video

Dharau za Rais wa Ukraine ni za level nyingine, anawakoromea Marekani nyumbani kwao. Angalia video

nchi za afrika trump aliziiti shit hole yaani shimo la mavi, viongozi wake si ndio atawaita uharo? Museveni tu alitishia kumkamata na kumfunga jela, haijulikana Trump anamheshimu kiongozi gani wa nchi gani ya Kiafrika na atatembelea nchi gani ya afrika kama ataendelea na dharau zake kwa mabara mengine. Ulaya yenyewe anaiona kama nyanya masalo tu
Aende kufanya nn huko?
 
Hii dharau na kiburi na kujiamini kwa rais wa Ukraine ni kwa level nyingine kabisa ambayo hainawahi kuonekana Duniani.

Zelensky yuko oval ofisi ama ikulu ya Marekani na awajibi Trump na Vance kwa dharau na kiburi cha hali ya juu sana.

Trump amesema Zelensky ameidharau sana Marekani tena mbele ya ofisi yao kuu.

Binafsi nimevutiwa na ujasiri wa Zelensky, ni wanaume wachache wanaweza kukaribishwa ugenini na bado wakamkoromea baba mwenye mji😂.

View: https://x.com/EndWokeness/status/1895528891164606810?s=09

Unaelewa tafsiri ya:
-JD Vance and Trump just put Zelensky in his place.
View attachment 3255398
Screenshot_20250302-022958.jpg
 
Nimeshangaa kuona watu wanasema Zele ana dharau. Yeye ndio kadhalilishwa. Namsupport kwa kusimamia nchi yake. Huyo VP wa USA ana kiburi sana.
Zele kauliza tuingie peace deal na Russia mna uhakika atatekeleza? Na kaeleza jinsi Russia alivyokiuka makubaliano.
Upon sahihi mkuu, Yani zelesnky alikuwa anaongea uhalisia wa mambo ulivyo alafu trump na vice wake walikuwa wanaongea siasa. Mitazamo miwili tofauti ndio maana hawakuelewana. Alafu peace deal za kisiasa hua zinatuliza upepo kwa muda tu adui anajipanga badae anarudi Tena.

Zeldnsky anataka amani ya kudumu yaani nchi yake iwe na jeshi imara pamoja na physical security guarantee toka US, vitu vitakavyomzuia Russia kumvamia tena na sio peace deal ya maneno Wala makaratasi ambayo Russia amekuwa akivunja mara Kwa mara.
 
Unaelewa tafsiri ya:
-JD Vance and Trump just put Zelensky in his place.
View attachment 3255398View attachment 3255401
Achana na hizo spinning, wewe mwenyewe baada ya kuangalia hayo mazungumzo umeona nini. Vitu viko wazi bado unasubiri uandikiwe uelezwe kilichotokea na wewe ukibebe kilivyo kama likondoo. Wewe umeona nini na tafsiri yako ni ipi, ukiachana na walichokiandika hao ama nilichokiandika mimi?

Ni nani ana guts za kwenda kuvimbia Marekani nyumbani kwao na kujibizana vile? Usisahau Zelensky alienda ili wasaini deal la madini, akafika akagoma na wakaanza kujibizana hivyo, hiyo sio kiburi ni nini?
 
Back
Top Bottom