Dhuluma za Wakenya kwa bandari yetu

Dhuluma za Wakenya kwa bandari yetu

Wengine tumejua siku nyingi hujuma za kimafia za kenya. Sio kwamba mambo yanatokea tu. Ndio maana hatuamini kwenye ushindani wa soko peke yake.

Tunaamini soko linaweza kukamatwa kwa hila na ujanja. Kwa hivyo tunaamini kwenye udhibiti wa soko. Hapa lazima inteligensia yetu kufanya kazi kama ni genuine problem tuweze rekebisha. Kama kuna mtu anakunywa tujue.

Kama unayosema ndio umeyajua kwa siku nyingi, nasikitika kukwambia umekuwa ukijua upupu kwa siku nyingi!!

Ungekuwa ukijua kuwa uchumi wa Kenya ni mkubwa kuliko wetu, ungejua Mombasa ni gati la nchi za South Sudan, Uganda and beyond, sehemu ya Rwanda. Ungekuwa unajua tayari SGR yao inafanya kazi na kufupisha safari za kutoka Mombasa mpk Nairobi. Ungekuwa unajua Dry Port ya Uganda iko Naivasaha Kenya - ungejua kuwa kuna mzigo mkubwa unakuja au kutoka Kenya na sio Dar es Salaam ambayo si reli ya kati wala TAZARA zinazofanya kazi!

Tusibaki kulaumu tunahujumiwa. Maersk hawezi kuleta 5th generation vessel kuja kupakua container 20 Dar kama anapata tu faidia akiteremsha container 300!! Mliozoea kufanya mambo bila kujali ufanisi wala faida hamwezi kuelewa haya. Kalia “tunahujumiwa” bila kushindana uone kitakachotokea.
 
Mkuu, 'Stroke', sijakusoma kitambo; hii ina maana nimetokea kukuelewa unaposimamia vyema zaidi hivi karibuni kuliko nilivyowahi kukufahamu huko nyuma, hasa enzi za Magufuli.

Lakini hayo tuyaache, tutazame hii hali mpya inayojitokeza sasa. Hao majirani sasa hivi wanafanya juhudi kubwa sana kutaka kuturudisha kwenye mstari wao. Wewe angalia juhudi za utalii, tulishawapiga bao, sasa sisi ndio tunaojipeleka kwao tushirikiane, tugawane watalii.

Maersk ni shirika moja tu wanalotaka kulitumia kuturudisha mfukoni mwao. Hivi sasa mikakati yao ni kuhakikisha mashirika makubwa ya nje yanayokuja kufanya biashara maeneo haya ya huku kwetu, ofisi zao kuu zinawekwa hapo kwao, sisi tunakuwa ni kama 'satillite' yao tu! Hii ni mikakati ambayo Samia ameaumua kujitosa, sijui kwa faida ya nani.
Makao makuu Ya Maersk kwa East Africa yapo Kenya, hivyo wanatumia hiyo nafasi kutuadhibu.

Maersk ina routes nyingi na meli nyingi hivyo ni shipping line muhimu sana.

Kutupiga pini maersk ni kuleta kilio hapa Nchini.
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
Sasa hapo ndio Wakenya wanaua bandari? Acha ujinga wako,boresha bandari yako iwe na hao shipping lines
 
Makao makuu Ya Maersk kwa East Africa yapo Kenya, hivyo wanatumia hiyo nafasi kutuadhibu.

Maersk ina routes nyingi na meli nyingi hivyo ni shipping line muhimu sana.

Kutupiga pini maersk ni kuleta kilio hapa Nchini.
Kwa hiyo unapendekeza nini sasa maana unalaumu as if ni haki yako,kwani miaka yote ilikuwaje?
 
Makao makuu Ya Maersk kwa East Africa yapo Kenya, hivyo wanatumia hiyo nafasi kutuadhibu.

Maersk ina routes nyingi na meli nyingi hivyo ni shipping line muhimu sana.

Kutupiga pini maersk ni kuleta kilio hapa Nchini.
sasa imekujaje wakati mama ndo ana mahusiano mema na Kenya kuliko mtangulizi wake
 
Mkuu, 'Stroke', sijakusoma kitambo; hii ina maana nimetokea kukuelewa unaposimamia vyema zaidi hivi karibuni kuliko nilivyowahi kukufahamu huko nyuma, hasa enzi za Magufuli.

Lakini hayo tuyaache, tutazame hii hali mpya inayojitokeza sasa. Hao majirani sasa hivi wanafanya juhudi kubwa sana kutaka kuturudisha kwenye mstari wao. Wewe angalia juhudi za utalii, tulishawapiga bao, sasa sisi ndio tunaojipeleka kwao tushirikiane, tugawane watalii.

Maersk ni shirika moja tu wanalotaka kulitumia kuturudisha mfukoni mwao. Hivi sasa mikakati yao ni kuhakikisha mashirika makubwa ya nje yanayokuja kufanya biashara maeneo haya ya huku kwetu, ofisi zao kuu zinawekwa hapo kwao, sisi tunakuwa ni kama 'satillite' yao tu! Hii ni mikakati ambayo Samia ameaumua kujitosa, sijui kwa faida ya nani.
Hizi ni porojo za kijinga,kwamba haya yote wewe unayajua ila serikali haiyajui sio?

Makao makuu ya mashirika ya kibiashara na umoja wa Mataifa hayajaanza Jana kuifanya Nairobi base yao.Hapa Tzn hakuna hata shirika moja.
 
Makao makuu Ya Maersk kwa East Africa yapo Kenya, hivyo wanatumia hiyo nafasi kutuadhibu.

Maersk ina routes nyingi na meli nyingi hivyo ni shipping line muhimu sana.

Kutupiga pini maersk ni kuleta kilio hapa Nchini.
Mkuu kama nakupata hivi,

Ila walioharibu hapo Maersk ni wabongo wenyewe. Wizi wizi tu hadi wakahamishia accounting department India. Hivyo unafanya malipo bongo, ila uhakiki wa malipo unafanyikia India.

Sekta husika wawabane hawa Maersk shughuli zote za uendeshaji zifanyikie hapa hapa Tz. La sivyo watu watakimbilia nje sababu ya huu urasimu na huduma mbovu.
 
Source https://www.the-star.co.ke › kenya
Lamu port receives third cargo ship destined for Saudi Arabia - The Star

16 Jul 2021 — The new Lamu Port, Kenya on Thursday received its third cargo ship carrying ... The two ships were on transit from Mombasa and Dar-es-...

New Lamu port set to host first transshipment cargo​

Thursday July 15 2021​

The Lamu port , Kenya will handle its first transshipment cargo today as a ship from Zanzibar will be calling at the facility to deliver freight meant for the Far East...source : New Lamu port set to host first transshipment cargo

Meli ya kwanza imeng'oa nanga katika bandari mpya ya Lamu kuelekea Saudi Arabia
Source : Ktn news Kenya
 
watendaji wetu wamelala usingizi wa pono

Kenya inatumaliza huku ikituchekea.
Kenya ina mkono mrefu na niwabobezi katika hujuma. Corruption ni ingredient ya kupata unachotaka kilaini.
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
Kwa mara ya kwanza umeandika jambo la maana
 
Mnaibiwa kwa vile ya upumbavu wenu na ufisadi kwenye department za serikali na within security operatives, private businessmen working with foreigners to plunder your country kisha CCM inasingizia Kenya., nyambaff, kama mimi nimeshihudia kikundi cha wezi kutoka Tanzania wanashirikiana na immigration officials wa Tanzania at border points, they steal high end cars from Kenya., wana register Tanzania na kuuza kwingine., walimuibiya jirani yangu Prado Tx mpya, new model, ilishikwa namanga kabla ya kuvushwa border, watanzania watatu walikamatwa, na sio mara ya kwanza, wanashirikiana na wakenya, sasa na mimi niseme ni serikali ya Tanzania ina huhjumu wakenya kisa kuna cartels kwa immigration department ya Tanzania? itakua ni upuzi huo., criminal elements are all over., ila hii thread imeonyesha ujinga ambao wana CCM wanayo., fikra za ki fala sana., try to think, idiot.
Nitakutafutia tu siku, nakuhimiza tu uendelee kutembelea jukwaa hili mara kwa mara. Kenya haina kitu chochote cha kujigamba dhidi ya Tanzania, ndiyo maana manajikomba sana ili muendelee kuinuka kwa kuitegemea Tanzania. Wewe tazama sehemu zote za uchumi, ni nini hasa kilichopo huko mnachoweza kudhani kitawainua? Mpo hapo mlipofikia kwa kudandia kwa wazungu, Wamarekani na waingereza. Kama siyo hawa kuendelea kuwafanya kama koloni hali yenu ingekuwa ni mbaya zaidi Halafu unakuja hapa kujigamba kumbe huna lolote.
 
Umeongea points nzuri Sana.

Hilo la makampuni makubwa kuwa na HQs huko Nairobi, hilo Ni kweli kabisa na wakenya wamefanikiwa Sana.

* Ukiangalia Banks kubwa zote za hapa TZ, HQs zake zipo Nairobi (ukiondoa hizi CRDB na NMB).

* Ukiangalia Insurance Company kubwa zote za hapa Tanzania, HQs zake zipo Nairobi

* Ukiangalia hizo shipping company kubwa, HQs zake zipo Nairobi

* Ukiangalia consumer goods company HQs zake zipo Nairobi

Kwa kifupi wakenya wamefanikiwa Sana kwenye vita ya kiuchumi dhidi ya Tanzania. Na ndio maana Balance of payments between Kenya na Tanzania haiwezi kuwa sawa. Sisi tunawapeleke mahindi (ndio export yetu kubwa, wao wanatuletea industrial and consumer goods), Sasa hapa balance of payments itakuwaje sawa.

Wakenya wame acquire viwanda vingi tu hapa Tanzania na mwisho wamevigeuza kama distribution centers (wakatengeneza bidhaa huko kwao na kuleta hapa na kuuza kupitia hizi kampuni za Tanzania ambazo wamezigeuza kuwa just warehousing).

Ukiangalia kwa undani Sana, kitendo cha kuwaruhusu kumiliki banks nyingi Sana hapa Tanzania, maana yake wameushikilia huu uchumi wetu kwa mikono miwili. Kwa hiyo utakuja kuta katika Hali ya kawaida Kenyan companies zinakuwa na competitive advantage dhidi ya Tanzanian companies linapokuja swala zima la priorities kwenye financing za biashara (wakenya watakuwa wanasaidia Sana)

Ukweli Ni kwamba Usalama wa Taifa umefeli pakubwa Sana kwenye ili Jambo. Wao walitakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzanian wanakuwa vinara kwenye kumiliki uchumi (sio wa Kenya Wala Indians).

Mimi Nina mifano mingi na ninajua namna gani hawa wa Kenya wanatudidimiza, Ila shida inabakia kwa Usalama wa Taifa letu, wameweka siasa Mbele Sana.
Mkuu 'Nkuba25', nimekuelewa vizuri sana, na nadhani tutaendelea kukutana kwenye majadiliano ya aina hii kila yatakapokuwa yanajitokeza.
Mimi sielewi kabisa Samia Suluhu katokea wapi hata asiwe na msingi wa kujuwa baadhi ya haya mambo. Huyu ni kiongozi ambaye amekuwemo kwenye serikali kwa muda mrefu ya kutosha, itakuwaje hata asiwe amesikia sikia habari zozote kuhusu haya mambo?

Anakwenda huko na anarudi hapa kwa furaha anajitangaza kwenda "Kufungua Nchi" - anamfungulia nani, na kwa misingi ipi?
 
Makao makuu Ya Maersk kwa East Africa yapo Kenya, hivyo wanatumia hiyo nafasi kutuadhibu.

Maersk ina routes nyingi na meli nyingi hivyo ni shipping line muhimu sana.

Kutupiga pini maersk ni kuleta kilio hapa Nchini.
Hiyo ni sehemu moja ya kutukaba.
Wewe subiri, tutakabwa sana; kwa maana ni kama tumejipeleka wenyewe.
 
Back
Top Bottom