Umeongea points nzuri Sana.
Hilo la makampuni makubwa kuwa na HQs huko Nairobi, hilo Ni kweli kabisa na wakenya wamefanikiwa Sana.
* Ukiangalia Banks kubwa zote za hapa TZ, HQs zake zipo Nairobi (ukiondoa hizi CRDB na NMB).
* Ukiangalia Insurance Company kubwa zote za hapa Tanzania, HQs zake zipo Nairobi
* Ukiangalia hizo shipping company kubwa, HQs zake zipo Nairobi
* Ukiangalia consumer goods company HQs zake zipo Nairobi
Kwa kifupi wakenya wamefanikiwa Sana kwenye vita ya kiuchumi dhidi ya Tanzania. Na ndio maana Balance of payments between Kenya na Tanzania haiwezi kuwa sawa. Sisi tunawapeleke mahindi (ndio export yetu kubwa, wao wanatuletea industrial and consumer goods), Sasa hapa balance of payments itakuwaje sawa.
Wakenya wame acquire viwanda vingi tu hapa Tanzania na mwisho wamevigeuza kama distribution centers (wakatengeneza bidhaa huko kwao na kuleta hapa na kuuza kupitia hizi kampuni za Tanzania ambazo wamezigeuza kuwa just warehousing).
Ukiangalia kwa undani Sana, kitendo cha kuwaruhusu kumiliki banks nyingi Sana hapa Tanzania, maana yake wameushikilia huu uchumi wetu kwa mikono miwili. Kwa hiyo utakuja kuta katika Hali ya kawaida Kenyan companies zinakuwa na competitive advantage dhidi ya Tanzanian companies linapokuja swala zima la priorities kwenye financing za biashara (wakenya watakuwa wanasaidia Sana)
Ukweli Ni kwamba Usalama wa Taifa umefeli pakubwa Sana kwenye ili Jambo. Wao walitakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzanian wanakuwa vinara kwenye kumiliki uchumi (sio wa Kenya Wala Indians).
Mimi Nina mifano mingi na ninajua namna gani hawa wa Kenya wanatudidimiza, Ila shida inabakia kwa Usalama wa Taifa letu, wameweka siasa Mbele Sana.