Dhuluma za Wakenya kwa bandari yetu

Dhuluma za Wakenya kwa bandari yetu

Shida ni viongozi wa bandarini na TRA kutokuwa na vikao vya asubuhi na kuulizana yanayoendelea ndani ya ofisi.
Usikute ni watu wawili tu wanafanya mambo kinyume bila viongozi wao kujua.
 
Sijaonaga watu wapuuzi kama CHADEMA ndio furaha yao iliyojificha,"MAMLAKA HUSIKA KUPITIA INTELEGENSI YAKE ITATUE HUJUMA HII KAMA IPO"
Kivipi, kwa kusema kuwa sekta ya bandari inaendeshwa kizembe na serikali au CDM ndio inaendesha bandari kizembe au kivipi?
 
Mkuu hapo wa kulaumiwa na kuwajibishwa ni hao watendaji wa Serikali na Serikali yenyewe.

Sasa kama hayo makampuni yameona Kenya kuna space ndio wakae wasubirie Serikali yetu iliyosinzia iwatafutie space ambazo hazipo wakati wao ni wafanyabiashara na wana order kibao za wateja wao. Ndi maana wameamua kukimbilia Kenya
Tuna uzembe mwingi sana Mkuu halafu lawama tunataka kuwapa wengine.

Just imagine kama space Dar imekuwa ni ndogo kwani bandari ni Dar tu,kwa nini wasingeipa shavu na bandari ya Tanga mizigo ikachukuliwe huko,ni akili ndogo tu wala ahihitaji kwenda shule. Hapo sia ajabu mtu mroho wa serikalini mmoja ameona akipeleka Tanga hatapata mtonyo wowote kaamua kiuumiza nchi mazima,na huenda huko Kenya sia ajabu port charges zikawa ni ndogo wakahamia mazima huko huko.
Dat is true.tunaisifia dar inaongoza kwa mapato kumbe ni bandari tu sasa wanaogopa kuhamisha shughuri za bandari ili tu dar pabakie dar.
 
Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.
Hebu twende taratibu... hatua kwa hatua!!

Yaani unachotaka kusema:-

1. Mtu anatoka na cargo yake ya kutosha kutoka huko aliko hadi bandarini huku akiwa hafahamu mzigo wake atausafirisha kwa kampuni ipi?! Yaani anafanya kama mtu anayetoka home kwenda kupanda daladala, au basi la kwenda mkoa?

2. Anafika bandarini huku akiwa na lengo la kusafirisha mzigo kwa kutumia Maersk Shipping Line! Hawa Maersk wana nafasi za kutosha za ku-handle mzigo husika lakini WANAUKATAA, na kusema hatuna nafasi?!

Is that what you're trying to say?!

Ni kwamba hii Maersk hivi sasa inamilikiwa na CCM au Serikali?!

Au sijaelewa?

Yaani bepari litoke zake Ulaya hadi Tanzania halafu liajiri watu watakaokataa mzigo?!

Hivi kuna anayeweza kunielewesha ndugu wananchi?!
 
Tanzania tunajimaliza wenyewe,meli kushusha mzigo inachukua week3?

Yani mzigo umeingia Tangu TAREHE 01/10 lakini mpaka leo meli hatujapata chance ya kushusha,TUTEGEMEE next time wateja watumie bandari ya TZ?
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
Hapa Tanzania hatuna ufanisi mkuu, wahusika wanaacha kunyenyekea wateja wao wako bize kutafuta namna ya kuibia serikali. Maboss wa bandari yetu wako very incompetent, ukienda mtu unayejitambua na kutaka kuleta maendeleo pale Wapare wanakuroga.
 
Una uhakika gani kwambw hajui? Mawazir mkatibu wa wizara husika wanafanya nn?
Mkuu 'Detective J',

Muundo wa utawala wa nchi yetu ulivyo ni kwamba Rais ndiye kila kitu. Hao wengine unaowataja hapo wapo tu kutimiza asemacho Rais. Hata wakiwa wanajuwa chochote, wakishaona dalili za mwelekeo alionao Rais, hawana ubavu tena wa kusema wanayoyajuwa.

Unaniuliza nina uhakika gani? Mbona sikuliweka hivyo kama ulivyoliweka wewe. Ni wapi nilipoandika kuwa "nina uhakika"?
 
"Mimi sielewi kabisa Samia Suluhu katokea wapi hata asiwe na msingi wa kujuwa baadhi ya haya mambo. Huyu ni kiongozi ambaye amekuwemo kwenye serikali kwa muda mrefu ya kutosha, itakuwaje hata asiwe amesikia sikia habari zozote kuhusu haya mambo?"

Refer to ulichoandika. Unashangaa rais kutojua? Is nikakuuliza unauhakika gani kwa hajasikia au hafaham hilo jambo??
I mean kuna possibility nyingi.
Probably amesikia.. au ana faham.. but si kwamba hajui kabisa. Possibility ni nying + rais ana sources nyingi za kupata habari
 
Kama kuna 'possibilities' nying, basi hakuna "uhakika", inakuwaje hulioni hilo?
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
TUnajenga mpya Bagamoyo
 
Wakuu wa bandari na wasemaji husika waseme neno juu ya mada hii ingawa binafsi nanusa HARUFU YA UONGO NA KAMA KAUCHOCHEZI kutoka kwa mleta uzi. Hayo ni maoni yangu sasa msinirukie kama mamba!
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
Mada yako ina kurasa tano na inaendelea...

Imenibidi nirudi tena niisome kwa mara nyingine tena ili nielewe vizuri ulichoandika hapa.

Bado inatia mashaka sana na ulichoandika hapa, kwa sababu, kama kuna ukweli wowote ndani ya haya uliyoandika kwa ufupi sana, tena bila ya ushahidi wowote ule, basi kuna jambo kubwa zaidi linaloikabili nchi yetu.

1. Wewe unasema: Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya"..., husemi wao (wakenya) wanahusika vipi na maamuzi ya hiyo 'Maersk'. Hapana, sisemi kuwa hawawezi kuwa washirika wa uamzi huo, tafadhari nielewe hivyo.

2. Unasema: "Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa..." Je, tunapowalalamikia wakenya kuhujumu, tunajuaje kwamba hakuna wahujumu humu humu ndani mwetu, ikiwa ni pamoja na hayo makampuni na pengine watendaji ndani ya bandari zetu wenyewe?

Unapoleta mada nzito ya namna hii, halafu unalashialashia tu na kulaumu, na huweki ufafanuzi wowote, huitendei haki mada yako. Hii ni kama unaweka 'uchochezi' tu usikie watakayosema wachangiaji.

"Msafirishaji akiangalia nafasi za ku'export' mzigo kwa hapa nchini hapati..." Hivi una maana kwamba msafirishaji pekee wa mameli ni huyo 'Maersk' peke yake? Tunajuwa ni kampuni kubwa inayoongoza kwenye maswala haya, lakini siyo kampuni pekee; sasa inakuwaje hawa 'exporters' wetu washindwe kabisa kupata meli za kusafirisha mizigo yao? Hivi meli haziji tena kwenye bandari zetu?

Mkuu, 'Stroke', naelewa unakosimamia, na kwa kweli naungana nawe katika baadhi ya misimamo yako siku hizi, lakini tuwe waangalifu sana juu ya ustawi wa taifa letu. Wakati huu taifa limo kwenye majaribu makubwa sana. Hatutasaidia chochote endapo tutakuwa watu wa kubahatisha tu kwa kuibua mambo bila ya kuwa na uhakika na tunayoyaweka ili na wengine wayaone na wayatolee maoni yao.

Tusiwe watu wa kutafuta kuchochea mihemko tu, kwa sababu hapo ndipo tutakapopigwa kisawasawa na hao wanaotuhujumu.
 
Kwani Maersk ni ya Kenya? si wako independent na Kenya haina mamlaka ya kuwa control.,, hizi fikra za bongo 😂 😂 😂 😂
MAESK Ni international co,labda tujikague sisi je TOZO zetu ni friendly for shipping co?,Hizi kampuni hufanyakazi popote palipo na KODI, rafiki.
HAKUNA MCHAWI HAPA TUJIKAGUE,TUJILINGANISHE,LOBBYING NI BAADA YA HAYO YOTE KUKAMILIKA.
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
Hee! Hii mbumbumbu ya wapi tena! Yaan kukosekana kwa shipping line dar ndo wakenya wanaua bandar! Liserikali lenyewe limelala usingiz wa pono! Linahangaika na wamachinga kutwa kuchaa..mara kuwabambikizia kesi kina mbowe..unazani watawaza sa ngap mambo makubwa na ya kutumia akil kama hayo ya bandar! Jitu la miraba minne JPM ndo lilikuwa na hizo akil! Wengine ni hewaa tuu
 
Back
Top Bottom