Wakristo tunajijua ama niseme tunajulikana. Hua hatuna mambo mengi pindi majengo yetu ya ibada yanapotumiwa katika miziki au hata miziki inapoashiria kinachofanywa hapo kinahusiana na dini ya kikristo.
Ndiyo maana hata wasanii wanaona dini ambayo wafuasi wake hawatokurushia mawe ni Ukristo. Wanamuziki wengi wameimbia kanisani, ndani na nje ya Tanzani, Amini ameshoot video kanisani, Mwana FA ameshoot video kanisani, Dudubaya ameshoot video kanisani, Banana ameshoot video kanisani, GK alishirikisha dini ya kikristo, Shaggy kashuti kanisani na Pastor akaonyeshwa ananyonga, T Pain akashut kanisani na wakapageuza dance floor.
Sasa tusiwajudge hao wa nje kwakua wana uhuru mkubwa kutuzidi. Sisi wakristo wa Tz huu wimbo tangu umetoka hakuna siku nilisikia malalamiko, mimi wimbo nimeuona jana lakini hata kama ningeuona kabla bado nisingelalamika.
Kwanini?
Kanisani tunafundishwa kwamba "Kanisa siyo jengo. Lile jengo linaweza likabomoka, linaweza tumiwa kufanya uasherati, kuimbia miziki. Kanisa siyo jengo kanisa ni Wewe. Kama Wewe ukaamua kwamba hii baa inakua kanisa basi baa itakua kanisa" nilifundishwa hivyo nikiwa la sita. Nafikiri kutokana na huu msimamo ndiyo maana wakristo hatukulalamika mpaka BASATA waliposema kwamba video haifai.
Director wa video alijua ugumu uliopo kufanyia shooting msikitini na wahusika wote wanajua huo ugumu.
Turudi kwa BASATA. Tulilalamika kwamba imejaza wazee wakateuliwa wakina Mwana FA kisha komedi zile zile zinaendelea. Wimbo una mwezi watu washauona ndiyo wanaufungia, nataka kujua kama BASATA hua wanaziangalia videos za singeli.
Anyway, mwezi inamaanisha watu zaidi ya laki 5 wameshauona kwahiyo hii ni kazi bure hapa. Ili isiwe kazi bure niliwahi sema zitolewe kanuni na taratibu za kufuatwa pindi msanii anapotaka kufanya video au kutunga wimbo. Ama la, msanii awasilishe kazi zake zipitiwe kabla hazijawa released public, ama la BASATA iwe na maofisa ambao wataambatana na msanii katika kuisimamia video husika mwanzo mpaka mwisho.
Pengine itasaidia kupunguza nyimbo kufungiwa.