hoja ya mleta uzi ilikuwa nzuri ila huenda uwasilishaji wake wa kukera ndo umefanya watu wameenda against
pia katika maisha ya mafanikio jifunze, usijifananishe na mwngne (hilo ni kosa kubwa utakuwa umefanya)
MFANO ULIO HAI
mimi na ww tunafanya biashara ya aina moja ,mtaji wa aina moja (hapa namaanisha mimi nimeingia na 500k na ww pia 500k
biashara tumeifanya ndani ya mwaka mmoja tu mi nikawa mbali kukuzidi ww( yaan mara tatu ya mtaji wako)
unabaki unajiuliza mbna mm nimepiga hatua sana???
sasa hujui humo katikat nimekutana na nini ,huenda tumegawana mali za urithi,huenda ndugu wameona tu wanichangie kukuza mtaji,huenda kaka yangu ameniwezesha zaid na zaid
tukija kwako humo katikat umepata majanga ya kufa mtu ,kila ukitaka kuinuka yanakuja matatzo yanalamba ukichokuwa nacho.
NJE YA TASWIRA
watu wataamini nina pambana kuliko ww,wataamin ww ni mzembe,au huna uwezo wa kuzalisha biashara na kwenda na muda
KWA HIYO USIPENDE KUJIFANANISHA,NJIA UNAZOPITIA NI TOFAUTI NA WENGNE.
MWISHO
kuna watu kwenye maisha wana kismart yaan mtu agonga 60yrs hajawahi kukutana na majanga makubwa wala mitikas migumu ya maisha ,ila ww hata 28 hujafikisha mara umeibiwa ,mara umefiwa na mke ,mara nyumba imesombwa na maji hahaha