Diamond ashindwa kupanda Mlima Kilimanjaro, Steve Nyerere azitapika Tsh. Milioni 2

Diamond ashindwa kupanda Mlima Kilimanjaro, Steve Nyerere azitapika Tsh. Milioni 2

Wakuu, binafsi nilifuhia sana, Waziri Hamis alivyohamasisha wasanii wengi kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Mara moja, kwa kauli mbiu Twende Zetu Kileleni...
Safari ilianza Jana Jumamosi Tarehe 28/09/2019, Ilikuwa ya siku sita.
Lakini Diamond, Steve Nyerere na Dogo Janja wamerudi leo Jumapili baada ya kuchoka sana... Walifika kituo cha kwanza Mandara wakarudia mbele kidogo ya Mandara.
Changamoto kubwa ni kupanda Mlima kwa mhemko, na pia nilishasema tena hapa kwenda gym kila siku hakukupi uwezo wa kupanda mlima Kilimanjaro. Na pia jamaa walionekana wakienda kwa kasi sana, Kosa kubwa... Kilimanjaro ni Polepole.
Bado nina wazo la kupanda Mlima Kilimanjaro na WanaJF walioko committed.
Na wote tutatoboa...
Wasanii waliobakia, wajitahidi sana ili watoboe.
Mkuu taratibu zikoje ? Na gharama , kama vifaa na misosi
 
Ukikamilisha mchakato kuhusu kupanda mlima unitag kiongozi
Wakuu, binafsi nilifuhia sana, Waziri Hamis alivyohamasisha wasanii wengi kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Mara moja, kwa kauli mbiu Twende Zetu Kileleni...

Safari ilianza Jana Jumamosi Tarehe 28/09/2019, Ilikuwa ya siku sita.

Lakini Diamond, Steve Nyerere na Dogo Janja wamerudi leo Jumapili baada ya kuchoka sana... Walifika kituo cha kwanza Mandara wakarudia mbele kidogo ya Mandara.

Changamoto kubwa ni kupanda Mlima kwa mhemko, na pia nilishasema tena hapa kwenda gym kila siku hakukupi uwezo wa kupanda mlima Kilimanjaro. Na pia jamaa walionekana wakienda kwa kasi sana, Kosa kubwa... Kilimanjaro ni Polepole.

Bado nina wazo la kupanda Mlima Kilimanjaro na WanaJF walioko committed.

Na wote tutatoboa...

Wasanii waliobakia, wajitahidi sana ili watoboe.
 
Halafu hako kajamaa kama uliangalia interview yake kanasema kanafanya showz 3hrs non stop so katapanda mlima kwa siku moja eti kupanda mlima kitu gani bana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kupanda Mlima Kilimanjaro sio mchezo alafu nashangaa wanashindwa kupanda Marangu Route , Ingekuwa Lemosho au Machame Ingekuwaje? Nimepanda Lemosho Route hadi kileleni [emoji123]
Hongera mkuu!!
Whisky route...
 
Asante.
Mimi nilitoboa ila ilikua shughuli mpaka kwenda na kurudi salama. Mtu akikwambia kafika kileleni inabidi umpongeze kwa kweli.

Hawa wasanii wengi kama nawaona watakavyokua wanabakia hawaendelei mbele na safari
Uliniahidi kwenda tena...
This time njoo tupandie Machame.
Haitakuwa ngumu
 
Mkuu mie nilishaenda kule tena kwa njia ngumu ya machame, lakini sikujikana, ila niwe mkweli tu kuna siku nililia, nikajuta na kujiuliza nini kimenipeleka kule
Mimi nilifanikiwa kupanda huo mlima sababu ilikuwa ni sehemu ya kozi
 
Huo mlima unahitaji mazoezi na uwe na afya njema na sio hela.
 
Unahamasisha watu kupanda mlima halafu wahamasishaji wenyewe wanashindwa kupanda hata kwa dau huku wakijitetea waziwazi kwamba hawawezi kuweka maisha yao rehani.

Hapo unakuwa umehamasisha au umekatisha watu tamaa?
 
Back
Top Bottom