Diamond atakiwa kuchagua dini kati ya Uislam au Ukristo

Diamond atakiwa kuchagua dini kati ya Uislam au Ukristo

Kufuatia kitendo cha Diamond kusoma neno kwenye moja ya mstari katika Biblia siku ya jana Mlimani City kwenye Mtoko wa Pasaka.

Sheikh Shariff Majini amemtaka Diamond aamue moja, kubaki kwenye Uislamu aachane na kufuru ya kujichanganya na Wakristo au aende kwenye Ukristo.

Ambapo sheikh amesema kama uislamu umemshinda aondokee.

Watu wanajipa mamlaka utadhani wana miliki dini. Pathetic individuals kwakweli
Mwache muhusika aamue
 
Ila Kuna watu wanashangaza sana
Na mtakasirika hadi mpasuke

Diamond shikilia hapohapo.
Ongeza tamasha jingine la kusifu na kuabudu.
 
Kuna mwingine ikifika jioni anakazana kutoa mawaidha spikani akisikika kuwa kipindi cha mfungo anayefunga kula madhambi yake yote yanapukutika mwilini mwake, eti mungu anamsamehe. Imani zingine zipo duniani kupumbaza watu
 
Huyo sheikh anaonesha ufinyu wa akili zake ulivyo. Anaona dini yake ni kama chama cha siasa cha hapahapa na pia anaona dini yake ni sawa na ushabiki wa simba na yanga. Majini gani hayo aliyo nayo yanakosa akili kiasi hicho?
 
Tattoo kibao, anavaa hereni na kuweka show ambalo ni dhambi
Sasa yote hayo hakukemea miaka aje akemee hili
Kweli kuna unafiki baina yetu na Mungu atusaidie
 
Shekh kama huyu anatakiwa kuwa sehemu ya majaribio ya kauli ya mama kuruhusu mizagamuano kwa watu wazima. Alitakiwa kukamatwa, kisha kupigwa miti ya kutosha na Pinda mubashala
 
Mbona Mazinge anasoma biblia kila siku na hajachimbwa mkwara kama huo
 
Kufuatia kitendo cha Diamond kusoma neno kwenye moja ya mstari katika Biblia siku ya jana Mlimani City kwenye Mtoko wa Pasaka.

Sheikh Shariff Majini amemtaka Diamond aamue moja, kubaki kwenye Uislamu aachane na kufuru ya kujichanganya na Wakristo au aende kwenye Ukristo.

Ambapo sheikh amesema kama uislamu umemshinda aondokee.
Huyo jamaa kwa kujiita Sharifu majini ni muongo na tapeli anaitwa Msolopa alikuwa na kiringe cha uganga pale Mabibo Dar ila sijui kwa sasa pia zamani hizo alikuwa akiwatumia watoto wanaojua kuisoma Quran kwenye mihadhara ya akina Mazinge ,Sule, Kalala wapi, kujipatia fedha.
 
Back
Top Bottom