waswahili bana tuna matatizo, eti jini!
haya mambo yaliwahi kunikuta, mke wangu alisafiri aliporudi akakaa wiki moja kisha akaumwa sana, sanaaa, mpaka akawa kama anaugua kichaa, akiwekewa dripu anachomoa, akikaa analia anaongea maneno ya ajabu na kujikuna kichwani. alikaa hospital karibia wiki mbili akawa kama amepona kabsaa, akarudi nyumbani akaniomba akapumzike kwao, kufika kwao tu kesho yake akaamka kichwa kinamuuma vibaya mno, mama yake akawa amepungukiwa imani akamchukua alfajiri wakaenda kwa "mtaalam", kule manyanga yakaonesha amerushiwa jini, tena hilo jini liloinilenga mimi likanikosa likaingia kwake!!!
Wakapewa mitishamba na kurudi nyumbani, alipofika nyumbani akachukua msaki akaenda nje akachuchumaa anapiga mswaki, mara hapohapo akaanguka chini, nikapigiwa simu nikamkuta yuko vibaya sana, nikambeba moja kwa moja mpaka hospital, akalazwa tena, wiki nzima haongei, ndugu na majirani wakienda kumtazama kila mmoja anarudi na maneno yake mtaani. akalamba dripu za kutosha, jamaa yangu mmoja ni doctor pale akamsimamia kwa ukaribu sana, baada ya wiki moja mtu akapona, mpaka leo hii yuko vizuri hakuna cha jini wala shetani!