Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Jamaaa sio writer mzuri, ana uandish wa secondary...kuna watu wakiandika unakubali. Sio vina vya kufosi
Toa mfano wa mistari yake kisha uyachambue kuonesha huo ubovu unaosema manake isije ikawa ni wewe binafsi ndio unaona haandiki vizuri lakini unavyowakilisha mada ni as if wote wanamuona sio mwandishi mzuri... narudia, toa mfano halafu ushushiwe nondo hapa!
 
Hana ubunifu kwenye uandishi. Almost
Kila nyimbo lazima alitaje jua
Watu kama wewe wanaitwa The Walking Disaster! Awali ulisema Diamond sio writer mzuri, kisha unasema hana ubunifu, almost kila nyimbo lazima ataje jua! Kwahiyo inaelekea ni mfuatiliaji mzuri sana wa nyimbo za Diamond na bado unasema Diamond sio mbunifu!!! Una matatizo aisee....
 
Kiba anauwezo kuliko Nassib,tatizo la Kiba hajitumi tu.Kiba, jitume kama Nassib uone kaka!!!
 
Kiba anauwezo kuliko Nassib,tatizo la Kiba hajitumi tu.Kiba, jitume kama Nassib uone kaka!!!

Naomba point iwe ana uwezo na ajitume,na sio kum compare na Dr 3D hilo ni kosa la jinai.
 
Watu kama wewe wanaitwa The Walking Disaster! Awali ulisema Diamond sio writer mzuri, kisha unasema hana ubunifu, almost kila nyimbo lazima ataje jua! Kwahiyo inaelekea ni mfuatiliaji mzuri sana wa nyimbo za Diamond na bado unasema Diamond sio mbunifu!!! Una matatizo aisee....

Haaaaa anajua kila verse za Raisi....
 
tatizo lako unataka kutafsiri nyimbo zake kwenye maisha yake binafsi, unajua kwanini kuna kitu kinaitwa dedication???

tatizo tumekariri usimlaumu huu ugonjwa tunao toka enzi za Julias,eti akiimba dmond yamemkuta akiimba dada jide kamuimbia mtu
 
Mziki sio lazima uelewe kinachoimbwa! Nini maana ya Prakatatumba?

There u are, ndo maana nkasem tuzo anazo pewa ni sababu ya kuupangalia mzik wake na swaggs bt uandishi ni kawaidaaaa sanaaaa
 
Baada ya Diamond Platnumz kutua jijini Dar es salaam December 2 akitokea Afrika Kusini akiwa na tuzo zake 3 za Channel O, alikutana na wadau, mashabiki pamoja na waandishi pale Escape 1 kuzungumzia ushindi wake na safari nzima ilivyokuwa.

Miongoni mwa maeneo aliyozungumzia ni pamoja na umoja unaohitajika kwa wasanii wa Tanzania ili waweze kuwa wengi katika majukwaa ya kimataifa.

"Ombi langu mimi kiukweli ni moja tu, Unajua lazima kama alivyosema mheshimiwa hapa muziki wetu ushakuwa, watu wanaukubali na tushaona njia kama tunaweza so lazima sisi tujiamini wenyewe tusikaekae sana nyuma kwasababu watu kuna ile kuogopa cha kuona kama aah watanipokea kweli. Na zile za aah ntashindwa kuongea kizungu ntachekwa mi nishachekwa sana kwenye kizungu sana, lakini saizi naweza nikaingia hata Big Brother na broken zangu hivyo hivyo lakini napita hivyo hivyo nimeingia pale juzi Fally hajaongea mi nimeongea ".

Diamond pia ameendelea kuwaomba wasanii wenzake kutotengenezeana beef za wenyewe kwa wenyewe, na hakusita kumtaja Ally Kiba wakati akitoa mifano alipokuwa Nigeria na kujiona yuko peke yake hakuna msanii yeyote wa nyumbani zaidi yake.

"Kingine mimi nilikuwa nataka niombe tufute zile zama zakutengenezeana matatizo wasanii wenyewe kwa wenyewe wa Tanzania kwasababu haiwezi kutusaidia kabisa, alikuwa anaongea kitu mkubwa hapa, nilivyofika Nigeria nilikuwa najiona kama mkiwa kwasababu niko peke yangu, nikiangalia huku simuoni hata Jaguar, huku siwaoni wasanii wenzangu namtafuta Dimpoz namtafuta nani, hata Ally simuoni yaani niko peke yangu."

Credit: BONGO5
 
Back
Top Bottom