Diamond Platinumz na kauli za kutatanisha katika “ reality show” ya Young, Famous and African

Diamond Platinumz na kauli za kutatanisha katika “ reality show” ya Young, Famous and African

Mzungu na mbongo wakiongea kiingereza huwa wanaelewana sana. Tatizo linakuja mbongo ukiongea kiingereza mbele ya mbongo mwenzako, lazima utaogopa kwasababu atachukua madhaifu tu ili akukosoe, tofauti na mzungu ambaye anaangalia main points ili muweze kuelewana. Shida nyingine ni kwamba mbongo anakusahihisha kwa lugha ileile ya kiswahili[emoji16]. Mzungu akiongea broken swahili anaonekana anajitahidi sana kuongea kiswahili na tunampongeza. Watanzania sijui nani katuroga.
Na hii imepelekea mpaka watoto wadogo kijaribu mambo sababu wanajua wakikosea watakumbana na ukosoaji wa Hali ya juu ndo kwa Tanzania watu wenye uthubutu ni wachache sana
 
Just to be clear.

Mwanaume hawi bitch.

Lakini hiyo ishu inaonekana ni scripted sielewi kwanini wameacha hii scene ionekane
Diamond ni mbwa jike

That is what he/she meant

A bitch ni mbwa jike
 
Hahahaha aisee hebu tafuteni pesa mpeleke watoto shule za maana wasiwe wajinga kama nyie au kama huyo anayejiita bitch.

Yani wewe uliyoko kwa mtogole usikie vizuri sana maneno diamond kuliko editor na director ambao wako na diamond zero distance alafu unasema wamekosea subtitles ??? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

kiingereza ni lugha na sio elimu we kiazi mbatata ,,! hakuna uhusiano wowote wa kuja kiingereza na kuwa na elimu
 
Pamoja na makosa hayo ya Diamond, bado kwenye ngeli anawaza 60% ya watanzania wote.
Upo sahihi, naamini hata mimi kwa kiingereza mondi atakuwa anakijua kuliko mimi, shida inakuja makosa aliyofanya.. Yeyote atakaesikia mtu anasema 31st yrs old hapo lazima astaajabu, hilo ni kosa ambalo linafanywa na wale wanaoanza kujifunza kiinglish.

Ni kama mwanafunzi wa level ya calculus kisha ashindwe kufanya hesabu ya +
 
Hahahaha he is a bitch

Daaah

“Shule twaipendaa shule twaipenda!! Kiuno changu chembamba cha kuvalia mkanda ,mimi mwenyewe mshamba jina langu chakubamba[emoji441][emoji443]”
 
kiingereza ni lugha na sio elimu we kiazi mbatata ,,! hakuna uhusiano wowote wa kuja kiingereza na kuwa na elimu
Hapa kwenye shule nzuri singumzii kingereza nazungumzia uwezo wa kupambanua mambo.
Narudia tena tafuteni pesa pelekeni watoto shule za maana wapate uwezo bora wa kupambanua mambo ili wasitie aibu kama mnavojitia aibu hapa.
 
Kwanini wanajilazimisha kuongea kingereza?, ulishamuona messi na uzungu wake anajilazimisha kuongea kingereza??, akubaliane na khali azungumze kiswahili wamtafsirie basi!, kwanza inaleta uzalendo, muafrika tumia lugha yako
 
Wote nyie mnapoteza muda wenu kwa mambo yasiyo na msingi kwenye maisha yenu

Tabia za kumcheka mtu akikosea kusema au kuandika kiingereza mmetoka nazo shule na kuziendeleza huku mtaani

Huku mkiwa mmesahau hii ni lugha ya kigeni na moja kati ya lugha ngumu zaidi kujifunza duniani iwe kwa kuandika na kuisema

Nguvu hii ya kukosoa kiingereza cha mtu ingekuwa inatumika kwenye maendeleo yetu binafsi, basi kama taifa tungekuwa mbali zaidi

Ila yote kwa yote utajiri wa Diamond unatokana na kuendelea kuongelewa kwenye midomo ya watu kila siku iwe kwa mabaya au mazuri

Na hongera kwa wenzetu walioamua kuwa wakosoaji wa maisha, lugha, mienendo na kila kitu cha maisha ya watu yasiyo wahusu

Hate is real.
 
Back
Top Bottom