Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amepost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay‘ amemuongelea bungeni.

Kwenye video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘

"Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu"

Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika; "Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo"
 
Ulichokiongea kinaeleweka na ni ukweli lakini jua kuwa kila serikali ina shelia zinazohusu kazi za wasanii na kuna raw inforcement, ndio maana nimetoa mfano ukiwa tanzania ni kawaida kuona magari ya PA ya makampuni yanafanya promotion balabalani kwa kupiga nyimbo za wasanii bila mkataba wowote yaani dj anaweka kwenye playlist anapiga tu, same company utaikuta Uganda imenunua several tracks za kufanyia promotion, hata hao wenye mablogs na ma you tube chanel wengi wanajulikana but hakuna shelia ya kuwadhibiti utaishia kureport youtube ili tu zifutwe. Bado auoni tatizo, unaweza kumkamata mtu na ukashindwa kumshitaki au kulipwa fidia. Serikali kazi yake ni kusimamia hizo haki miliki za wasanii. Sasa hata kama utachukua kampuni ya kusimamia kazi zako kwenye digital platform bila sheria inafanya kazi vipi? Kwa wenzetu kuna shelia na watu wanapigwa faini ya mamilioni ya dola? Na hizo kampuni zinaendeshwa kwa faida, serikali inaweza kuamua destiny ya hawa watu, ndio maana hadhi ya msanii wa uganda, kenya, south adrica , nigeria na tanzania ni tofauti kwa sababu kila nchi ina policy zake kwenye sanaa na nyingine hazipo sawa
Usinielewe vibya, na mimi nachukizwa na wizi wa haki ya mtu, kuibia kitu ambacho wewe unajuwa ni jasho lako sio jambo zuri. Lakini wakati huo huo tujaribu kujikumbusha kwamba sio kweli kama Tanzania haina sharia ya hati miliki. Tumekiwa na sharia hii tokea mwaka 1966, na imekuwa inafanyiwa marekebisho mara kwa mara. Mwaka 2016 Bunge lilifanya marekebisho mengi, moja wapo ililikua ni marekebisho ya ring tone, na malipo kwa wasanii na kazi zao kupitia redio na TV. (una weza kusoma marekebisho hayo kupitia kwenye PDF kutoka tovuti ya Bunge)
https://www.google.co.uk/url?sa=t&s...SMd3tYVfWl6jAfdJg&sig2=twq2PZZmjauJNP3oqVlucg

Cha msingi as I said before, it will take money and knowledge to make copyright law work in Tanzania. Wasanii wetu wanatafuta njia za mkato kujipatia kipato bila kujali au kujuwa kama mkato huo ndio unafungua mianya ya kuibiwa kazi zao. Kuna taasisi ambayo inajulikana kisheria ya COSOTA, unatakiwa kama msanii uandikishe kila kazi iliyo ifanya au kubuni ili ijulikane dunia nzima kama wewe ndio mmiliki halali wa kazi hiyo. Makampuni ya nje yenye nia mzuri ya kutaka kutumia kazi za wasanii wa TZ katika shughuli zao wanashindwa kufanya hivyo kutokama na wasanii wetu kutojiandikisha kisheria mahali popote na hawataki wakitumia kazi ya mtu halafu ajitokeze mtu mwingine anasema hiyo kazi ni yake. COSOTA hawaandikishi mtu bure, you need to pay for the service na ndio maana wasanii wetu hasa wale ambao hawaja toka kisanii wanapitia njia ya mkato kuweka vitu kwenye youtube kujijengea jina.

Kama wasanii wetu wangekuwa wanatambulika kisheria kupitia taasisi kama COSOTA, wangeweza kudai haki yao hata kama ni nje ya nchi. Na ndio maana nikasema unahitaji kampuni au wafadhili wenye pesa kukulindia kazi yako. Serikali inaweza kukulindia haki yako kupitia sheria Kali, lakini kama wewe hujajiandikisha mahali popote kama mmiliki wa hiyo kazi, how could the government protect you??.
 
Huyo hata akifilisiwa sawa tu maana ndie aliekuwa muvaa manguo yakijani nakuimba mchana kutwa akiipigia debe ccm. Halafu kuisu kodi azodaiwa msibishe maana baada uchaguzi huu tumemshuhudia huyu jamaa akiwa tajili gafla kwahiyo wao cccm wanaju walimlipa pesa nyingisana
 
Hahahaaa ccm wanataka pesa yao waliyomlipa wakati wa kampeni 2015.

Si mnaona wengine imewagharim uprofesa?
 
Kaponzwa na Bashite huyo... si alimkaribisha yeye mwenyewe akamuelezea kila afanyacho... sasa alipe tu hamna jinsi
 
WADAU kwanini mmehisi Diamond analalamika kulipa kodi na sio anasapoti wazo la kuitaka serikali "ipandikize mbegu" kwa wasanii na sio kutaka "kuvuna" tu!!?
 
Back
Top Bottom