Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Kaongea kweli mswahili hana shukrani ukimbeba lazima akunyee.
 
People don't know about it.. Wanachojua ni kukosoa tu
 


Hajajibu swali bado hawa jamaa wanawaibia sana wasanii ni vizuri wasanii wapate elimu na kujua vizuri haki zao. Kila label ina wekeza lakini msanii mfano akiandika nyimbo hiyo ni haki yake tofauti na uimbaji lakini hawapati haki hiyo kutokana na habari tunazipata. Vilevile producer wa beats naye anatakiwa kuwa na haki ya zile beats kama itatumia sehemu nyingine zaidi ya music mfano movies, advertising anatakiwa kuwa na % yake hapo . Kila label ina gharama laini ni lazimq kuwe na haki
 
Na hiyo point ya mwisho sidhani kama inakwepeka kwa tajiri kama yeye anaetaka kuendelea kua tajiri.

Ni vile tu vijana wanakua hawana mtu wa karibu wa kuwasimamia kwenye hiyo mikataba.
Ni kweli, na hapo ndipo wanapopigwa
 
Nina uhakika BASATA wakiweka hiko kitengo na kuweka vigezo label itakayo baki itakuwa WCB pekee,maanake label nyingine zimekuwa kama vijiwe vya kahawa mchana stori jioni kulala shows hawana,branding hamna wapo wapo tu.
Hakuna namna kama wanafanya biashara udhibiti ni lazima uwepo,vinginevyo hali itazidi kuwa mbaya
 
Cha kushangaza mtu kama P Funk eti naye anamuita Diamond mnyonyaji.

Sielewi ni kwa nini Tanzania ukifanikiwa unachukiwa bila sababu.

Hivi wakati Diamond anatowa nyimbo ya mbagala hawa watu walikuwa wapi?

Diamond ni self made millionaire. Ukichukia uwe na sababu.
 
Eeh sikuzote dharau huanza baada ya raia kuanza kulamba asali. Mtu kachukuliwa hana mbele wala nyuma anapewa mkeka wa 6O/4O anakubali.

Akishabrandiwa na kuwaka, chupi sio tatizo anabadilisha with a few clicks. Ndinga ana afford ndio yanakuja mambo ya kuwaza ananyonywa. Hii sio case ya kwanza. Ndio biashara ya mkataba ilivyo hata Tanzania inagewaga 3% japo dhahabu ni yake. Mabeberu wanazoa 97%
Kiuhalisia mtu akiwa hana ramani hukubali lolote lile imradi aingie.
Akishaona amefanikiwa huanza mambo yake

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wewe kiazi ni mmoja ya vizibo hopeless ulimwenguni.
 
Umaskini unaleta roho mbaya, roho ya hasira , roho ya chuki na roho za husuda.
 
Umaskini unaleta roho mbaya, roho ya hasira , roho ya chuki na roho za husuda.
 
Kaongea CEO,ameeleweka,sasa mtu anataka apate Bure,hakuna kama hicho,lazima ulipie
 
Ni haki yake,ila hizo sifuri za kumbrand msanii ifike mil 500.🤔
Kuna hilo pimbi la kisomali hapo ndo linamshauri waongeze masifuri ili msanii ashindwe waendelee kumnywa
 
Sio mara ya kwanza Mondii kuzungumzia ichi kituu. Malegend wa bongofleva wengi wanaishi maisha ya njaa kutokana na kutoutambua muziki wao kuwa ni Biashara.

Biashara inaanza na cost then profit. So unataka kutoka cost unailipaje?(kumbuka cost ni sawa na deni la benk) Rudisha kwanza then utoke. Na kwa kuzingatia hayo ndiyo maana anayelipa anaachwa awe Huru.

Wasanii wengi wanaendekeza njaa tu lkn jambo kuu la kumsaidia mtu usiyejua atarudisheje pesa yako ni risky. Kuna kifo, kuna kuumwa n.k Unayemsaidia akipata haya matatizo anarudishaje cost za boss wake??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…