Diamond Platnumz akiri kuwa anapenda sana nyoka

Diamond Platnumz akiri kuwa anapenda sana nyoka

Sio kweli,kuna watu wanapenda nyoka kama ilivyo kwa watu kupenda mbwa paka nk.
Nina bro wangu tangu tupo shule ya msingi alikuwa akiona nyoka anamvizia anamkamata kwa mikono karibu na kichwa anamng'oa meno anamuweka mfukoni(wa kaptura) anakuja kututishia nyumbani na shuleni,baadae anamuachia

Kwakua maranyingi tulikuwa nae akifanya hivyo nikajikuta namimi woga ukatoka nikaanza kukamata, japo Mimi nilikuwa siweki mfukoni wala kumtoa meno,namkaba karibu na kichwa nikishamchezea namrusha mbali

Yeye hata vinyonga alikuwa anakamata anamuweka begani anaingia nae darasani wanafunzi wenzake wanatoka mbio.

Kuna wale buibui wakubwa sana wanakuwa na tumbo kubwa,wanatembea taratibu, anachumkua anamnatisha mgongoni kwenye shati halafu anajifanya kamsahau anakuja nae nyumbani au anaenda nae shuleni.

Kwahio naamini wapo wanaopenda nyoka.
Bro wako ndo yule anafanyakaz kaz sabasaba maonyesho.....
 


Bosi wa WCB Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz amejipatia mnyama aina ya nyoka wa kuweka nyumbani.
Katika tangazo lake kwenye Instagram, mwanamuziki huyo alibainisha kuwa siku zote kumiliki nyoka kipenzi imekuwa ndoto yake.
Staa huyo wa Bongo mwenye umri wa miaka 32 alimtambulisha nyoka huyo wake kama rafiki yake mpya.

"Siku zote nimekuwa na shauku ya kuwa na nyoka wangu kama kipenzi [emoji3590][emoji216].. jameni tukutaneni na rafiki yangu mpya," alitangaza siku ya Ijumaa.

Aliambatanisha ujumbe huo na video yake akicheza na mnyama huyo anayeteleza huku kundi kubwa la watu wakiwa wamemzunguka.
Katika video hiyo, Diamond alisikika akikiri upendo wake mkubwa kwa nyoka na kueleza furaha yake kwa kumpata wa kufuga nyumbani

"Huyu mimi namfuga mnyama huyu nyumbani. Mimi napenda nyoka sana," alisika akisema.
Umati ulitazama kwa udadisi alipokuwa akichezea na nyoka huyo kwa usaidizi wa mwanamke aliyekuwa akimuonyesha jinsi ya kumshika. Hakuonesha uoga wowote na badala yake alionekana kufurahi sana kumshika.

Mwimbaji huyo anayetambuliwa kote duniani alifichua kwamba nyoka huyo wake atatambuliwa kwa jina Chichi.
Katika hali ya kawaida nyoka sio wanyama wa kupendwa miongoni mwa watu wengi. Wengi wa wanyama hao wana sumu ambayo inaweza kusababisha kifo au ugonjwa mbaya mara tu wanapomng'ata mtu.

Baadhi ya jamii za Kiafrika huhusisha mnyama huyo na uchawi na hivyo kamwe hawawataki karibu nao. Wale wanaofuga wanyama hao mara nyingi huchukuliwa kuwa wanashiriki katika uchawi.
Ndiyo kwanza bado tupo January lakini Diamond platnumz tayari ameshatoa video bora ya mwaka 2024, kitu gani umekipenda kutoka kwenye hii video ya "yatapita".?
 
Juzi almanusura tugongwe na black mamba🥺🥺maskini sasa hivi chakorii angekuwa marehemu🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹🥹

Mungu yupo jamani
ningekupoteza kipenzi,pole sana
 
Back
Top Bottom