Diamond Platnumz ashinda tuzo tatu AFRIMA

Diamond Platnumz ashinda tuzo tatu AFRIMA

Ivi kila tunzo inauzwa kwa shi ngp nataka kujua maana naona jamaa analazimisha umarufu kupitia biashara mbovu ya kununua tunzo
 
Ivi kila tunzo inauzwa kwa shi ngp nataka kujua maana naona jamaa analazimisha umarufu kupitia biashara mbovu ya kununua tunzo
Duh mkuu ivi kila mara ununue tuzo kweli yan tokea aanze muziki anunue tuzo tuuu
 
Unajua watanzania wengi hawawaelewi hawa wasanii wetu na aina ya muziki wanaoufanya na dhamira yao....

Muziki umegawanyika katika makundi matatu na kama msanii usipojua Hitaji lako basi utajikuta umetumbukia kwenye umaskini

Wasanii wa Tanzania wamegawanyika katika makundi haya yafuatayo;

1.Wapo wanaofanya muziki kwaajili ya kujifurahisha na kufurahisha watu(Music for Fan)..Humo utawapata wakina Profesa Jay,Sugu,Vicky Kamata..Hawa hawaangalii kama muziki utawalipa au lah..Inawezekana wamechoka au wameridhika..Hawana Haja na Shows au Tunzo kwa sasa

2.Wapo wanaofanya muziki kwa ajili ya Kutafuta umaarufu ili waonekane wanajua sana kuimba kushinda wenzao na kupata jina(Music for Fame)..Humu wako wengi sana akiwemo Roma mkatoliki, Alikiba,Baraka,Ruby,Nay wa Mitego,ChidBeenz,Mr Blue,Fid Q,YoungDee,na wengineo...kundi hili wanaamini katika ubora wa Sauti na Punchlines,na wanapenda sana kushangiliwa..hawajali kama nyimbo zao zitatoka nje ya Africa au la,wao wanachotaka ni Umaarufu tu..haijalishi ni wa faida au hasara..wanapenda kushindana kusikokuwa na faida,ili mradi tu waendelee kujulikana.

3.Wapo wanaofanya muziki kwa ajili ya Fame(Umaarufu),Biashara na Fedha(Music for Fame and Money)..Humu ndani utamkuta Diamond,Weusi,Chege ameamka na yeye,Vanessa Mdee,Darassa anakuja humu,ChristianBella,Ay,watoto wa WCB,na wengine...
Hawa wako tayari kufanya Kiki yeyote ile ili mradi tu muziki wao uuzike..ni watafutaji wa Collabo zenye Faida kwao na wanachakarika kupeleka nyimbo zao nje ya nchi,pamoja na shows za kimataifa.Hawaamini katika Sauti nzuri,wanaamini katika Melody nzuri na Beat inayoendana na sauti zao..
.Hawakati tamaa,hawaogopi kuingia popote pale wanapoona panamanufaa kwao,wako tayari kubadilika kulingana na soko la muziki..Hawa wanaamini kwenye juhudi na maarifa..

Haya ni mawazo yangu sio sheria, unaweza ukaongezea niliposahau...

Hongera Mr Chibu kwa ushindi...natumai mwakani watashinda wasanii wengi zaidi...
 
Back
Top Bottom