Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Yani unamuinea huruma Mondi aliekuzidi kila kila kitu?

Kwa nini usiuonee huruma ukoo wako unaotafunwa na umasikini?
 
Hawa wanaharakati unaowaita ni wasomi na wana exposure ya hali ya juu sana wananifikirisha sana.Exposure yao na usomi wao unawafanya wanashindwa kutambua sio kila mtu lazima awe mwanaharakati kama wao,watu wengine wameamua kuwa wafanyabiashara na mfanyabiashara yeyote anaside na upande utakaomletea faida hyo ndo principle dunia nzima.Hata hao wazungu mnaowaona ni watu wanaosimamia haki pale linapokuja swala la biashara watasimama na ilipo faida.Ndo maana mpaka leo wanaendelea kuinvest Uganda na Rwanda.Diamond ni mwanamziki na mfanyabiashara cku Chadema wakiwa madarakani ataside nao na ccm ikirudi tena atakuwa nao vilevile.Na labda wanashindwa kuelewa au wanajitoa ufaham serikali zetu za Africa ni ngum sana kukuacha ukaishi kwa amani ukianza kuwakosoa refer akina Lissu,Mbowe,Sugu na wengine ndo maana hao akina Kigogo wamejificha kuhofia usalama wao ila wanataka wenzao waende front wakale shaba,au wamesahau kilichomkuta Marehem Remmy Ongala na wimbo wake wa Mrema?
 
Kijana hana washauri wazuri !! mambo ya Usanii na Siasa ni kuwa makini nayo saana, watanzania wanamuhukumu kupitia mitandao.

Ningekuwa mimi, nabadilisha benchi lote la ufundi, naomba radhi naanza ukurasa mpya !!
Ila Roma ndio ana washauri wazuri? Sugu je?

Pr. J?
 
Ila Roma ndio ana washauri wazuri? Sugu je?

Pr. J?
Kuna tofauti kubwa kati na Msanii mpigania HAKI za binadamu na Msanii anayesifu dhuruma na uovu wa watawala!! nafikiri hapo ndipo mnapompoteza Nasibu. Sasa kwa sababu nyie ni wabishi haya mwambieni aendelee then atauona mwisho wake.

Mitandao ya kijamii ndiyo silaha tosha iliyobakia ya watanzania.

 
Endeleeni kujidanganya ahahahhahah
 
Ule wimbo wa Diamond "acha nikae kimya" nadhani watu wengi hawakuuelewa au waliuelewa lakini wameamua kujifanya hawakuelewa. Acha nikae kimya ilikuwa ni mamna ya kuwasilisha hisia zake kuwa hata yeye hafurahishi na baadhi mambo mabaya yanayotendwa na watu wake wa karibu. Sioni kama ni sawa kusema eti alikuwa anafurahia au anawatetea waliomteka roma na kuufungia wimbo wa ney wa mitego
 
Yaani aombe radhi kisa hakuisapoti chadema ila aliisapoti sisiemu, upuuzi kabisa! Ungewashquri hao unaowaita wasomi wanaharakati wa-mind their own eff business...
kua mtulivu, soma kwa makini. hawamshutumu kwa kufanya kampeni ccm, analalamikiwa kwa KUKAA KIMYA pindi uonevu uliposhamiri katika jamii, mfano baada ya kutekwa ROMA yeye akatoa nyimbo inaitwa ACHA NIKAE KIMYA leo yamemkuta hahahahahaha
 
Nafikikiri hujaelewa kilichoandikwa,hakuna aliyesema kisa hakuisapoti chadema, hapa kinazungumzwa kipindi watu mbalimbali wanapata matatizo kama kutekwa kwa Roma, Nay, kufungiwa kwa wasanii kww kuonewa yeye kama msanii mkubwa alifanya jitihadw gani?
Kwani kutekwa kwa Roma si wasanii haohao waliandamana wakiwemo WCB mpaka kwa Mkuu wa mkoa na akaahidi atapatikana na akapatikana. Mbona hili halisemwi tena nakumbuka Babu tale ndio alikua mstari wa mbele kwelikweli toka utawala wa Nyerere mpaka Jpm watu wametekwa na wameuwawa kwanini iwe kwa hawamu ya tano tu na kwa diamond pekee?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kigogo aliwahi kufanikisha kitu gani tangu aanze harakati zake ili tumuone kweli ni akili kubwa?

Nyingi tu na wewe unazijua au kama umesahau muulize Kenge Lugola.
 
Ni kweli tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…