Kama hizo ni kauli za diasport basi itoshe kusema ni WASENGEREMA na akili zao Hazina akili kabisaa! Kwa hiyo walitaka Mbowe asilipwe fedha zake alizodhulumiwa! Au akilipwa amtukane Rais ili awe mpinzani kweli?! They should learn to give credit where it is due!
Magufuli alikuwa kuongozi wa hovyo kabisa kwa sababu ya kudhulumu haki za watu, kuanzia haki za kuishi, haki za kutoa maoni mpaka haki za mali. Alikuwa ni mporaji wa uhai wa watu, mporaji wa uhuru wa raia, na mporaji wa fedha za watu.
Samia kama amewarudishia watu mali zao ambazo ni haki zao, kuna kosa gani jina lake kunenwa vizuri?
Ushetani wa marehemu ndio uliofanya achukiwe na kila mwenye akili. Anapotokea kiongozi wa kufanya kinyume na matendo ya yale ya kishetani, ni halali kusifiwa, angalao kwa jambo hilo.
Mbowe ana haki, na ni haki yake, kurejeshiwa kilicho halali yake. Kumnyima, ni sawa na Rais Samia kubariki ushetani wa marehemu. Na Mbowe, pamoja na wengine kurejeshewa mali zao, halafu waendelee kumlaumu Rais Samia, sawa na walivyokuwa wakimlaumu Rais aliyekuwa tunda la shetani, kila mwenye akili atamshangaa.