Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Aisee!

Kuna watu wanaridhika jamani.

Tshs. 1.5M ni wastani wa $750.

Watu wanatengeneza zaidi ya $1000
Ndani ya wiki na ni kazi ya kawaida.
Huyu atahitaji Kurogwa kurudi.
Mkuu mazingira in tofauti purchasing power ya $ 750 mfano US no tofauti sana na ilivyo TZ, gharama za Maisha huku bado zipo chini sana.
 
hahhhahhah aisee
 

Kwanza mimi sio wa Lumumba ni mwananchi wa kawaida.

Lingine maisha kweli ukipiga hapa kazi tu.. utafurahia.. tabu watanzania uvivu uvivu katika mengi n.k
 
Ukiacha baridi kali hata mzembe wa nje anaishi maisha bora kuliko akiwa Bongo. Unazungumzia nchi ambazo hazina kukatika maji wala umeme. Ukikodi nyumba friji, jiko la umeme, microwave, hita na AC viko katika kila nyumba. Nyumba nyingine unapata na dishwasher (la kuoshea vyombo) na mashine ya kufulia. Hakuna anaefua kwa mkono wala kuanika nguo kwenye kamba. Kwanza jua hakuna vipindi vya baridi.

Usafiri ni wa maana sana matreni na mabasi ya uhakika. Kuwa na gari ni karibu kila mtu anayo.

Vyakula wenzetu walishatatua tatizo la chakula siku nyingi. Hutasikia mtu analalamika bei ya sembe wala sukari. Watu wananua tu mtu ukimuuliza kilo ya sukari bei gani hatakuelewa.

Shule za hawa jamaa sio siri darasa la pili lina vifaa ambavyo chuo kikuu cha UDSM au sijui UDOM hakuna. Yaani kumtoa mwanao Marekani uende kumsomesha shule ya kata Kigamboni ni kumdhulumu haki yake. Kwanza akizaliwa nje ana uraia wa nje.
 
Kipofu hawezi muonyesha njia Kipofu mwenzake.pateni msaada wa mawazo kutoka kwa wenyeji waliofanikiwa halafu changanya na za kwenu.
 
Kabla ya kurudi unatakiwa uwende kunusa japo miezi miwili alafu unaondoka,Ukienda kichwa kichwa sio maisha bali watu wenye roho mbaya wanakuvuruga..
 
Rafiki ninasubiri Danish pastries hapa Kwamtogole
 
Na asikuongopee mtu teknoloji inafanya watoto wa wenzetu kuwa na akili. Yaani mtoto wa kimarekani wa miaka kumi haya makitu ya computer sijui kudownload app, kuskan, kunetwok na wenzie kwenye vitablet na gemu atakutoa ushamba wewe babake.
Utakuta mtoto wa miaka kumi anajua kununua tiketi za treni za kwenye mashine. Anaweza kusoma njia na ratiba za matreni.
Halafu TV. Huu ni ushauri kwa wabongo. Waacheni watoto waangalie vipindi vya televisheni za watoto vya kingereza hasa channel za kimarekani. Yaani mtoto anasoma email na text zako kabla wewe mzazi hujajua kama anajua kusoma.

Teknoloji zimefanya mpaka walimu wao wa shule wanasema watoto wa siku hizi ni balaa.
 
Hakuna. Standard ya maisha dunia nzima ni sawa.


that's right, ulikurupuka kujisemea usichokijua.

-Diaspora wengi wanaishi maisha ya viwango vya kawaida. Makazi yao ni kupanga permanently, wachache wana mortgage, wanalipa miaka 30. Wenzao nyumbani, hata kwa mshahara hafifu wa mwalimu, wanajenga...

-Wanaishi kwa kujificha kwa vile hawana makaratasi...

-Wanafanya kazi zenye mishahara midogo, odd jobs, "kazi za ajabu ajabu..."

-Waliochukua uraia wakirudi nyumbani inabidi wafiche passport ya nje, kwa nini, eti wanakwepa $50 visa fee, hawana kitu, na pia inabidi wafiche estate zao zisije kukamatwa na Waziri Lukuvi wa ardhi...

-huko nje hawana potential ya kuwa watu wa maana kama wakurugenzi wa mashirika au viongozi wa kiserikali au mahakama, au chochote kwa vile ni wageni, ni weusi, ni disenfranchised, wana language barrier...

-Wanazeeka wakiwa wamechelewa hatua muhimu za kijamii kama kuoa, kuzaa na kusomesha watoto...

-Wana waste miaka mingi na hela nyingi kutafuta makaratasi kupitia ndoa magumashi, wengine mpaka miaka 10 kama ndoa ya kwanza inadunda, na ni nyingi sana zinadunda...

-Wanaishi kwa msongo wa mawazo na upweke wa kufiwa na wazazi ambao wameshindwa kuja kuwazika...

-Wengine wana makaratasi lakini hawarudi kwa vile nauli hawana! Au anaogopa kurudi hana cha kuonyesha nyumbani, vyeti hana, familia hana, kiwanja hana, hela hana...

-wamekuwa shut out from kusomea au ku practice profession fulani fulani zinazolipa kwa mfano ni Watanzania wangapi ni athletes au wasanii au madaktari au ma lawyer au ma architecture? Mzungu gani atampa Mswahili amchoree jengo? Inabidi wasomee unesi wa kulea wazee, CNA. Wewe unaujua mshahara wa CNA? Profession za maana zipo wanazosomea lakini kuna "glass ceiling," yani kuna dari ukilisogelea unagonga kichwa, huwezi kutoka Mapipa kwa Bi. Nyau ukapewa kuwa Chief Financial Officer wa Ford Corporation.

-Wanaishi kwa u-room mate wengi wengi kwenye apartment.... Bongo nani anaishi na room mate?

Standard of living za diaspora? You kidding me?
 
Nimekujibu hivyo ili upite tu. Dont waste your time quoting me.
 
.........All I can say maisha ni popote. Hapa bongo wengi tumezoea maisha ya ujanja ujanja (wizi wizi). By the way, make no mistake, wapo wanaotengeneza clean money na wanaishi vizuri tuu. Lakini hao ni wachache ambao hawategemei political favors kuendesha maisha yao. Lakini kama ambavyo JPM ametuonyesha wengi walikuwa ni magumashi ndo maana usishangae leo wengi kuhamia CCM....kwa sababu TRA wakichungulia tuu madaftari ya biashara wengi wataishia segerea. Yet, kwa diaspora ni kula jasho lako kweli kweli!!

So my friends in diaspora, msikatishwe tamaa na sisi tulio home. Wengi ni kelele na kuzoea shortcuts kwa vitu vidogo sana. Na wivu! Ndo maana wengi humu ukiwapeleka nje ni ngumu ku-cope. Hivi jiulize mtu ni civil servant mshahara hata million haifiki...leo ana ghorofa Mbweni! na hana mkopo... Imagine....(zile nonsense za biashara na side activities..have been debunked by JPM) ndo maana wengi leo wanalia. Lakini nje ukitaka ghorofa utaratibu upo and if you work hard, really hard you can have that ghorofa.

Mimi kuna diaspora nimekutana nao Germany, UK, US, Italy nk....they are working so hard and they support many extended family members kwa hela hiyo hiyo ya kufagia. Ofcourse wajinga wapo wanaoendekeza drugs na Pombe. na kila Jamii hao watu hawakosi.

Msikatishwe tamaa na watu. Rudini bongo kama mmeshafanya savings za "kueleweka na mmejipanga" vizuri (relative term so to speak).

Kikubwa: Avoid kutumia hela ndugu eti akufanyie investments kama ujenzi wa nyumba au kununua viwanja. NEVER TRY THAT! wengi wamelizwa. Na kwa aliyepata hela kwa jasho lake ananielewa. But ultimately ni vizuri kuwa na property nyumbani whether DSM au Magu!

Changamoto ni nyingi Lakini maisha yanawezekana.
 

Mkuu hiyo $1000 na Ushee ninayokueleza
Uelewe ni kwa wiki.

Na sikatai matumizi yapo lakini haingii
Akilini mtu anaeweza kusevu hata net $1000 nje kwamwezi,

Aje umlipe Tshs.1.5M kwa mwezi.

Tunaridhika mapema sana tu wabongo.
 
sasa kama Tanzania opportunities ziko nyingi huko abroad unaenda kufanya nini?.....na sijawahi kusikia mtu anafanya kazi abroad anaishi Tanzania
o
Hujawahi sikia?basi ongeza exposure...tofautisha kufanya kazi abroad kwa muda na kuishi abroad... Kazi iko based bongo... Kwenda abroad is js part of the job
Taasisi kama UN,IMF,WB,NGO,Balozi,TISS, Wizara ya Mambo ya Nje..nk...wanasafiri sana..inategemea upo kitengo gani..
 
Diaspora, pigeni box, fanyeni kazi zenu za ofisi n.k. Ila mkumbuke kuwekeza huku, wazee wetu waliobahatika kwenda huko karibu wote walirudi na kuendeleza libeneke hapa...
Nyumbani nyumbani tu, kwa elimu yetu ya shule za kata, secondary na vyuo zimewafikisha wengi huko, wakavuna wakarudi, TZ bado bikira ukilinganisha na ughaibuni, kuanzia kwenye miundo mbinu, afya, elimu, ustawi wa jamii na technology..
Suala ni kutumia hizo elimu, exposure na ujuzi kufanya ya huko kwetu, hizo ndizo opportunities, mawazo yasiwe kutaka kuajiriwa tena, ya nini wakati fursa za kujiajiri ni nyingi kuliko kuajiriwa TZ?!
 
Mkuu mazingira in tofauti purchasing power ya $ 750 mfano US no tofauti sana na ilivyo TZ, gharama za Maisha huku bado zipo chini sana.

Ni kweli mkuu.
Lakini mimi nimelinganisha kipato cha WIKI MOJA kwa mtu NJE na Kipato cha MWEZI MZIMA Bongo ambapo jamaa anadai Inatosha sana ndio maana nikasema yeye anaridhika mapema.
 

mbona majawabu yako sawa kabisa? mimi naishi 1st na 3rd. hayo yote niliyoyataja ni machache kati ya mengi ambayo diaspora yeyote yanampa changamoto.
 

mengi uko sahihi. kama huna shughuli ya kufanya ughaibuni. labda ukafikiri kitendo cha kutua ughaibuni tu basi ni kuukata bora urudi au ubaki home. kule ni shida. hakuna mtu wa kukuthamini. unakuwa kitu cha kudharaulika. sasa yoote hayo ya nini wakati wewe siyo mkimbizi, kwenu hakuna vita ya nini kwenda kuteseka nchi za watu!!??
kwanza nchi ikiwa na diaspora wengi ni dalili ya kuwa failed state. nchi zote zilizo na mizozo na kuzorota kwa uchumi ndiyo zenye asylum seekers wengi. HALAFU mTanzania ukiomba asylum hawatakupa kwa sababu kwenu hamna vita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…