Hakuna. Standard ya maisha dunia nzima ni sawa.
that's right, ulikurupuka kujisemea usichokijua.
-Diaspora wengi wanaishi maisha ya viwango vya kawaida. Makazi yao ni kupanga permanently, wachache wana mortgage, wanalipa miaka 30. Wenzao nyumbani, hata kwa mshahara hafifu wa mwalimu, wanajenga...
-Wanaishi kwa kujificha kwa vile hawana makaratasi...
-Wanafanya kazi zenye mishahara midogo, odd jobs, "kazi za ajabu ajabu..."
-Waliochukua uraia wakirudi nyumbani inabidi wafiche passport ya nje, kwa nini, eti wanakwepa $50 visa fee, hawana kitu, na pia inabidi wafiche estate zao zisije kukamatwa na Waziri Lukuvi wa ardhi...
-huko nje hawana potential ya kuwa watu wa maana kama wakurugenzi wa mashirika au viongozi wa kiserikali au mahakama, au chochote kwa vile ni wageni, ni weusi, ni disenfranchised, wana language barrier...
-Wanazeeka wakiwa wamechelewa hatua muhimu za kijamii kama kuoa, kuzaa na kusomesha watoto...
-Wana waste miaka mingi na hela nyingi kutafuta makaratasi kupitia ndoa magumashi, wengine mpaka miaka 10 kama ndoa ya kwanza inadunda, na ni nyingi sana zinadunda...
-Wanaishi kwa msongo wa mawazo na upweke wa kufiwa na wazazi ambao wameshindwa kuja kuwazika...
-Wengine wana makaratasi lakini hawarudi kwa vile nauli hawana! Au anaogopa kurudi hana cha kuonyesha nyumbani, vyeti hana, familia hana, kiwanja hana, hela hana...
-wamekuwa shut out from kusomea au ku practice profession fulani fulani zinazolipa kwa mfano ni Watanzania wangapi ni athletes au wasanii au madaktari au ma lawyer au ma architecture? Mzungu gani atampa Mswahili amchoree jengo? Inabidi wasomee unesi wa kulea wazee, CNA. Wewe unaujua mshahara wa CNA? Profession za maana zipo wanazosomea lakini kuna "glass ceiling," yani kuna dari ukilisogelea unagonga kichwa, huwezi kutoka Mapipa kwa Bi. Nyau ukapewa kuwa Chief Financial Officer wa Ford Corporation.
-Wanaishi kwa u-room mate wengi wengi kwenye apartment.... Bongo nani anaishi na room mate?
Standard of living za diaspora? You kidding me?