Diaspora watatu wa Mzee Sarungi hawakuja kumzika baba yao

Tungekuwa tunafuatilia rasilimali za nchi yetu kama tunavyofuatilia maisha ya watu..., Amini nakwambia, hata senti moja isingepotea bure...

Ila ndio hivyo tena (our energy and resources are misplaced); Anyway to each their own...
 
I wish hii ingekuwa ndiyo utamaduni wetu kuanzia leo. Misiba ya Bongo, hasa ya watu maarufu sasa hivi imekuwa ni kama kero. Hakuna privacy kabisa kabisa. ''TV online'' zinapiga kambi nyumbani (mpaka sebuleni) kwa mfiwa, wa-record. Wafiwa wana-rekodiwa wakilia na kuomboleza. Kusema ukweli mimi ningekuwa natoka familia maarufu halafu tufiwe na ndugu yetu ambaye ni maarufu, ningefanya kama ulivyosema, wacha wapige kelele.
 
Walikuambia wewe ukazike? Wewe ni mchimba makaburi?
 
Basi wafuasi wake .. wanaharakati wenzake kule mjini X wasitupe lawama kwanini Mama samia hajatoa salam za pole ..
Hao ni kama nyumbu wanaojiendea ovyo, hawajielewi. Nishaelezea hapo juu.

Hutakiwi kuwa unafanya kampeni kubwa sana za mabadikiko ya katiba za kumpunguzia rais madaraka mengi aliyopewa kikatiba, halafu hapo hapo wewe mwenyewe unamuongezea rais nguvu ambazo hata hajapewa kikatiba na kutaka kufanya msiba hauna umuhimu mpaka rais autambue na kutoa rambirambi.

Ni ujinga. Ni kutojielewa.

Rais hana umuhimu huo kwenye misiba ya watu.

Na inawezekana familia ya Sarungi inatoa statement ya kumuondolea rais umuhimu huo, lakini hawa watu walio kamanyumbu wengi wanaojiendea ovyo kwa mkumbo tu, hawaelewi somo.
 
Hakuna kitu kama values za waafrika. Kila kabila lina taratibu zake na kila familia inafanya inachoona ni sahihi. Subiri baba yako afe ndiyo utekeleze hizo african values.
 
Je hata angezikwa na dunia nzima , kipi kingebadilika?

Ahsante
 
Mkuu,

Hiyo point ni ya wazi kabisa lakini Watanzania wengi hawaielewi.

Washakariri msiba ni hivi na vile.

Sasa hivi misiba, hususan ya watu maarufu, imekuwa kama reality shows za kwenye TV.
 
Kuna Watanzania wengi ni sadists.
Nafikiri Watanzania wengi wanathamini sana kuonekana msibani ndio maana hata Steve Nyerere huwa anahesabu wakina nani wamefika na wapi hawakufika katika misiba yao wasanii.
 
Nafikiri Watanzania wengi wanathamini sana kuonekana msibani ndio maana hata Steve Nyerere huwa anahesabu wakina nani wamefika na wapi hawakufika katika misiba yao wasanii.
Steve Nyerere ndo nani huko Tz?
 
Ulitakwa ukamzike Sarungi?
 
Values za kulazimishana kuhudhuria misiba na values za kipumbavu
 
Nafikiri Watanzania wengi wanathamini sana kuonekana msibani ndio maana hata Steve Nyerere huwa anahesabu wakina nani wamefika na wapi hawakufika katika misiba yao wasanii.
Unaruhusiwa kuthamini kufika msibani wewe, lakini usimpangie mtu mwingine jinsi ya kuomboleza.

Kuna watu wanajali sana kumuona mtu kabla hajafa, akishakufa kuzika kwao wanaona si muhimu ilmuradi washaagana na marehemu alivyokuwa hai, wanaona watakuja kuangalia kaburi siku yoyote. Hiyo ndiyo falsafa yao ya maisha na huna haki kuwanyanyapaa kwa falsafa hiyo.

Sasa wabongo wakiona hivyo wanaweza hata kukutukana.

Wabongo wanaweza kujua unaumwa wasije kukutazama kwa miaka, lakini ukifa lazima waje kukuzika. Sasa hapa kitu muhimu zaidi ni kipi? Kumtazama mgonjwa na ikiwezekana kumsaidia wakati anaumwa, pengine hata kuzuia kifo chake ikiwezekana, au kuja kumzika wakati kashakufa?

Wabongo wanapenda kujichomeka kwenye misiba ya watu maarufu.Wakati msiba si wao, familia si yao, maisha si yao.

Mradi tu wanajimilikisha shughuli ambazo si zao.

Sasa mtoto wa Sarungi yuko Ulaya, sijui anaishi vipi, sijui makubaliano yake na familia yao yakoje, hajafika kumzika baba yake.

Mimi inanihusu nini wakati hayo ni mambo ya ndani ya familia ya Sarungi?

Mimi natakiwa nipange mambo ya familia yangu, si kuingilia uhuru wa familia ya Sarungi kujipangia wanazikaje mzee wao.

Familia ya Sarungi imefiwa. Jukumu la jamii ni kui support kwa kila njia, sio kuanza kuisimanga na kuweka siasa katika msiba wao.

Kwa nini point hii inakuwa ngumu sana kwa Watanzania wengi kuielewa na kuikubali?
 

Walihuzulia kwa njia ya mtandao. yaani zoom.
Familia ndiyo waamuzi wa mwisho, wengine watazamaji tu
 
Mtoto wa Manji alikuwa anajitengeneza yeye na familia yake mazingira mazuri ya kuzifikia fursa za biashara kwa Waswahili ndio maana akafanya hayo yote.
 
Hali kama hajiza ruhusu hakuna shida. Atakuja kuwaona wakati mwingine
Anaweza kuja na anaweza asije kabisa pia, inategemea kaburi lina umuhimu gani kwake.
 
Unaandika kishabiki utadhani kichwa umeweka rehani kukopa hela ununue dela.
 
Na hiyo ni haki yao.

Familia yao, maisha yao, maamuzi yao.

Tatizo liko wapi?

Pilipili ya shambani kwa familia ya Sarungi nyie inawawashia nini?
It’s funny how people are getting bent out of shape, fuming and frothing at the mouth about a bereavement arrangement of another family who are seemingly fine with whatever they agreed on.

Suala ni la kifamilia. Kama wao walikubaliana na wakaelewana kuwa baadhi yao hawatoweza kushiriki moja kwa moja kwenye msiba wa baba yao kwa sababu zozote zile, tatizo liko wapi hapo?

Kuna mambo mengine mtu unaweza kudhani ni mepesi sana kuyaelewa, kumbe wapi!

Watu wameumia mno kwa kukosekana kwa Maria.

SMH.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…