Unaruhusiwa kuthamini kufika msibani wewe, lakini usimpangie mtu mwingine jinsi ya kuomboleza.
Kuna watu wanajali sana kumuona mtu kabla hajafa, akishakufa kuzika kwao wanaona si muhimu ilmuradi washaagana na marehemu alivyokuwa hai, wanaona watakuja kuangalia kaburi siku yoyote. Hiyo ndiyo falsafa yao ya maisha na huna haki kuwanyanyapaa kwa falsafa hiyo.
Sasa wabongo wakiona hivyo wanaweza hata kukutukana.
Wabongo wanaweza kujua unaumwa wasije kujutazama kwa miaka, lakini ukifa lazima waje kukuzika. Sasa hapa kitu muhinu zaidi ni kipi? Kumtazama mgonjwa na ikiwezekana kumsaidia wakati anaumwa, pengine hata kuzhia kifo chake ikiwezekana, au kuja kunzika wakati kashakufa?
Wabongo wanapenda kujichomeka kwenye misiba ya watu maarufu.Wakati msiba si wao, familia si yao, maisha si yao.
Mradi tu wanajimilikisha shughuli ambazo si zao.
Sasa mtoto wa Sarungi yuko Ulaya, sijui anaishi vipi, sijui makubaliano yake na familia yao yakoje, hajafika kumzika baba yake.
Mimi inanihusu nini wakati hayo ni mambo ya ndani ya familia ya Sarungi?
Mimi natakiwa nipange mambo ya familia yangu, si kuingilia uhuru wa familia ya Sarungi kujipangia wanazikaje mzee wao.
Familia ya Sarungi imefiwa. Jukumu la jamii ni kui support kwa kila njia, sio kuanza kuisimanga na kuweka siasa katika msiba wao.
Kwa nini point hii inakuwa ngumu sana kwa Watanzania wengi kuielewa na kuikubali?