Kama wao wanakuringishia picha wewe huna vya kuwaringishia kwani?
Waringishie mgao wa umeme, maji kutokuwepo wiki nzima, viongozi wezi wanatajwa wameiba kwenye report ya CAG ila wanapeta na ulinzi mmewapa.
Waringishie chawa wanaolipa $3 kumsifia rais na viongozi wengine, waringishie kuandamana ni kosa ila kwenye katiba maandamano yameandikwa ni ruhusa.
Waringishie treni ambayo wengine wanajenga kwa miaka 2 nyie mnaenda 7 na bado haijulikani lini itaisha ili nanyi mkapige picha.
Yapo mengi sana ya wewe kuwaringishia.