Dilemma: Je, nimwandikishe jina lake kwenye mali zangu au nikubali tuachane?

Ndugu zangu wanaJF, habari zenu!!!

Nimekuwa mfuatiliaji wa mada za JF tangu 2018 na nimekuwa nikivutika mno na elimu itolewayo hapa jukwaani lakini sikuona haja ya kujiunga kama member kwa kuwa nilihisi sina chochote cha kuchangia hapa,ila sasa nimeamua kujiunga rasmi ili kupata ushauri kuhusu tatizo linalonisumbua.

Mimi ni mtu mwenye hali nzuri ya kifedha. Nina nyumba tatu za kisasa na magari mawili (SUV ya kifahari na sedan ya kisasa).

Hata hivyo, hivi karibuni mpenzi wangu ambaye nipo naye mwaka wa tatu sasa ameniambia kwamba anataka niandikishe jina lake kwenye mali zangu, akisema kuwa nisipofanya hivyo basi huo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu.

Nampenda sana na sidhani kama ningependa kumuumiza kwa kumkatalia, lakini watu wa karibu wamenishauri nisithubutu kufanya hivyo. Najiuliza, je, ni sahihi kumwandikisha jina lake kwenye mali zangu, au nifanyeje?

Nahitaji ushauri wenu wa busara.

Asanteni!!!

Ungeweka vizuri kwanza, ni mpenzi au ni mke wa Ndoa?
Je amekukuta ukiwa na hivyo vitu au umevipata baada ya kuoana?
Ukishajibu hayo, nitajua pa kuanzia kutoa ushauri
 
Kitakachokuzamisha siyo kwasababu umetumbukia mtoni,bali ni kwasababu umeshindwa kuogelea.

Kutafuta furaha ya moyo ni pamoja na kupoteza kinachokupa hiyo furaha.

Muache aende
Nimeipenda hii "Kitakachokuzamisha siyo kwasababu umetumbukia mtoni,bali ni kwasababu umeshindwa kuogelea."
 
Wakuu, naomba ushauri wa dhati. Je, ni busara kumwandikisha mpenzi mali zangu ili tu kulinda uhusiano? Nampenda sana, lakini naogopa kuumizwa. Nifanyeje?
Mkuu mimi sina ushauri wa dhati. Si busara kumwandikishia mpenzi wako mali zako na usilinde uhusiano. Usimpende sana na furahi kuumizwa. Fanya hivyo.
 
Uwe unahudhuria vikao ili ujue misingi halisi ya kataa ndoa.

Nakuelekeza umuone KAIMU MWENYEKITI WA KATAA NDOA KANDA YA PWANI,Ndugu Natafuta Ajira akupe MIONGOZO.

Nakala moja uaiche masijala pale makao makuu ya KATAA NDOA ili waweke kwenye faili lako kama kumbukumbu.

Nawasilisha.
Kwangu kukataa ndoa hapana
 
Ungeweka vizuri kwanza, ni mpenzi au ni mke wa Ndoa?
Je amekukuta ukiwa na hivyo vitu au umevipata baada ya kuoana?
Ukishajibu hayo, nitajua pa kuanzia kutoa ushauri
Sio mke wangu na amenikuta nina kila kitu
 
Miaka yote uliyotumia kuifatilia jf haijakusaidia kumbe!, wewe ni zwazwa kama mazwazwa mengine hili halikutakiwa kuwa hata swali hiyo ilitakiwa iwe tiketi yake!. mkuu na note jina lako nikikuona jukwaani sehemu yoyote nakudunda nimeghafirika sana!
Huyo hata hayo magari hana, huwezi ukawa na hela afu ukawa huna akili kiasi hicho
 
Ndugu zangu wanaJF, habari zenu!!!

Nimekuwa mfuatiliaji wa mada za JF tangu 2018 na nimekuwa nikivutika mno na elimu itolewayo hapa jukwaani lakini sikuona haja ya kujiunga kama member kwa kuwa nilihisi sina chochote cha kuchangia hapa,ila sasa nimeamua kujiunga rasmi ili kupata ushauri kuhusu tatizo linalonisumbua.

Mimi ni mtu mwenye hali nzuri ya kifedha. Nina nyumba tatu za kisasa na magari mawili (SUV ya kifahari na sedan ya kisasa).

Hata hivyo, hivi karibuni mpenzi wangu ambaye nipo naye mwaka wa tatu sasa ameniambia kwamba anataka niandikishe jina lake kwenye mali zangu, akisema kuwa nisipofanya hivyo basi huo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu.

Nampenda sana na sidhani kama ningependa kumuumiza kwa kumkatalia, lakini watu wa karibu wamenishauri nisithubutu kufanya hivyo. Najiuliza, je, ni sahihi kumwandikisha jina lake kwenye mali zangu, au nifanyeje?

Nahitaji ushauri wenu wa busara.

Asanteni!!!
Amekuzalia watoto wangapi
 
Mkiambiwa msioe wachaga wa Machame hamsikii.

We mwandikishe tu Kama ndio alikuzaa, maana asiyefunzwa na mama atafunzwa na ulimwengu.
 
Wakuu, naomba ushauri wa dhati. Je, ni busara kumwandikisha mpenzi mali zangu ili tu kulinda uhusiano? Nampenda sana, lakini naogopa kuumizwa. Nifanyeje?
Mkuu
Unacho kipaji cha upumbavu broo.
Muandikishe hili usimuumize mpenzi wako.
Hakikisha hadi chupi ulizonazo anajua idadi yake hayo ndo yatakuwa mapenzi ya kweli toka kwenye moyo wako.
 
Ndugu zangu wanaJF, habari zenu!!!

Nimekuwa mfuatiliaji wa mada za JF tangu 2018 na nimekuwa nikivutika mno na elimu itolewayo hapa jukwaani lakini sikuona haja ya kujiunga kama member kwa kuwa nilihisi sina chochote cha kuchangia hapa,ila sasa nimeamua kujiunga rasmi ili kupata ushauri kuhusu tatizo linalonisumbua.

Mimi ni mtu mwenye hali nzuri ya kifedha. Nina nyumba tatu za kisasa na magari mawili (SUV ya kifahari na sedan ya kisasa).

Hata hivyo, hivi karibuni mpenzi wangu ambaye nipo naye mwaka wa tatu sasa ameniambia kwamba anataka niandikishe jina lake kwenye mali zangu, akisema kuwa nisipofanya hivyo basi huo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu.

Nampenda sana na sidhani kama ningependa kumuumiza kwa kumkatalia, lakini watu wa karibu wamenishauri nisithubutu kufanya hivyo. Najiuliza, je, ni sahihi kumwandikisha jina lake kwenye mali zangu, au nifanyeje?

Nahitaji ushauri wenu wa busara.

Asanteni!!!
Usisubutu kufanya ujinga kama huo mpe chake tu wanawake wengi japo awafanani
 
Back
Top Bottom