Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Amlee tu, kuna ushahidi upi watakaoutumia wale wa upande wa shemeji kumdai mtoto?
Kwa sasa, hakuna anayejua kwamba yule si mtoto wake zaidi ya yeye, sisi ndugu zake wa karibu na mkewe ambaye ndiyo amefariki.
Kitamaduni watoto atakaozaa mwanamke ni wangu kama nitakuwa nimemtolea mahari ikiwa nitaridhia. Pia mtoto mwenye changamoto ni wa kike, atakuwa na kuolewa ataenda kwake. Tatizo lingekuwa kubwa endapo angekuwa wa kiume
Umenena vyema.
 
Alisema ndugu wa rafiki yake na familia ya mkewe wote ni maisha duni, akimpeleka mtoto huko vijijii atateseka sana, na anapata ugumu maana huyo mtoto anampenda sana baba yake na baada ya mama yake kufariki amebaki naye kama mzazi pekee.
Mambo ni 2 tu hapo Apige kavu au atumie condom.
Either ampeleke Kwa ndugu zake hata kama Wana hali duni ya kimaisha au abaki nae ili aje ashikwe Kwa kosa la jinai.
Kuhusu upendo Huwa unaisha kama yeye upendo wake ulivyoisha Kwa huyo mtoto.
Lakini kama anaweza kujizuia kufanya makosa au kumfanyia vitendo vichafu huyo mtoto basi amlee tu kama Binti yake.
 
We acha ujinga.. Gambe anywe mpaka adondoke kwenye mtaro ndio uchungu utaisha

Inabidi anywe mpaka ajute kuwa malaya

Kila kitu kina gharama yeye aliwezaje kuzalisha mapacha kwa mfano.! Bao lake lilikuwa sio la kawaida. 🤭

Hapaswi kujuta kila ntu apambane na vita yake🤗
 
😂😂 Hapo umemaliza kabisa. Kila mtu ana vita yake, ila kunywa mpaka kuanguka mtaroni si suluhisho. Afanye maamuzi yake akiwa na akili timamu, maana kila uamuzi una gharama zake.
 
Umenena kwa busara sana, huu ushauri utamfikia.
 
Hapo aone kama analea yatima tu, afanye kamq kamuadopt kumfanya wa kwake.
Ushauri mzuri
Kinachouma ni kwamba walisaliti ikiw aliwapenda na kuwaamini. Historia ambayo haiwez kurekebishika
Kweli, anaumia kwa sababu amesalitiwa na watu wake wawili wa karibu zaidi na hana hata uwezo wa kuwauliza kwanini waliamua kufanya vile.
 
Asante kwa ushauri mzuri, utafika kama ulivyo kwa mhusika.
 
Umenena kwa busara sana, huu ushauri utamfikia.
Kama ni wewe umeamua kuuliza kwa njia ya mtu mwingine, naomba ujue kuwa si jambo jema hasa kwa mwanamke kutoka nje ya ndoa. Inahitaji mwanaume mwenye kifua kipana na mwenye hofu ya M/Mungu kuweza kumlea huyo mtoto la sivyo, huyo baba anaweza kumfanyia vitendo vya ukatili ili kulipiza yale aliyofanyiwa
 
Huyo mke aliharibu sana.
Ingawa alitubu baada ya kuona maiti mbele yake akaona ile dhambi inaweza kumzuia kuingia mbinguni.
Hii case ngumu sana.
Hili ni jaribu zito kwake, asipokaa vizuri na nafsi yake soon naye atakufa.
Vijana tuache dhambi, dhambi inaua roho na mwili
 
Hakika binafsi nasema inahitaji uwezo wa akili wa hali ya juu unless otherwise mtu anaweza kumfanyia Binti kitu mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…