Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Ndoa zina useng* mwingi sanaaa.
Anayopitia mwamba namuonea huruma
1. Awe ana amka usiku na kufungulia mziki na kuweka nyimbo ya dini anayoipenda.
2. Hii nyimbo itamfanya alie na asali
3. Apige maombi, kwa kuwa kutakuwa na muziki basi si mbaya awe anasali hata kwa sauti na aliye tu maana moyo umebeba mengi.
4. Ni Mungu pekee ndio anaweza kumuelewa, arudi kwa Mungu asali sanaaa

Time heals, Atapona tuuuuu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Wanaume Huwa hatukatai watoto!!hata kama ujauzito alikabidhiwa mwingine halafu wewe ukalea!!

Kwanini!!?coz maisha yetu yamejaa kuhitajika na sio kupendwa kwenye jamii sasa SI vizuri kuongeza idadi ya maadui coz fainali uzeeni!!
Huyo mwanamke na jamaa yake waliofariki wamelipia karma yao hivyo yeye amlee tu vyema mtoto hana hatia!!

Huwa tunachukua hatua Fulani kama mwanamke Bado yupo hai japo sio kwa kulipa kisasi bali kuweka mambo sawa!!

Unaweza ukaoa na maisha yakaendelea!
 
Wewe umeandika mambo ya maana sana.
You are matured enough
 
Daaah, kufilisika kabisa 😂
Mimi kama mwanamke hakuna kitu kitaniuma kama kukosa watoto wangu au hela aiseeh!

Cc: Seran
Pesa unaweza pata nyengine na watoto unaweza pata wengine ila kuhusu swala kugongewa halifutiki yaani ukigongewa hamna namna unaweza Fanya ili ufute kule kugongewa hata uioshe, hata ukimuacha, ata ukitafuta mwanamke mwengine Bado haufuti kuwa mwanamke wako alitumiwa na mwanaume mwengine.inshort ndy jambo linaloumiza sana Kwa mwanaume.
 
Kitanda hakizai haramu Yule mtoto NI wake akitaka mambo yawe mengi awatangazie walimwengu ili ashuhudie udaku Ila akitaka aishi kwa amani ibaki sili yake kwishaaa
Kitanda hakizai haramu si kwa kila Me, hujawahi kuona baadhi ya Me hufanya mauaji hata ye mwenyewe kupotea au kujiua? Hapa panahitaji hekima ya Mungu pekee si kiurahisi namna udhaniavyo.
Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Ushauri mzuri utamfikia.
Nina wasiwasi na hiyo issue ya DNA,aliipimia wapi? Mahakama gani ilimpa ruhusa ya kufanya hiyo DNA? coz DNA ina taratibu zake,sio kama kwenda kupima Malaria tu.,
Nairobi mkuu, haya mambo ya kipuuzi ya kuhitaji court order tunayo bongo tu!
Labda swali langu niwaulize tu wana jamii,Je marehemu alikua sahihi kutoa hiyo siri kua huyo mtoto hakua mtoto wa mumewe?
Marehemu alitoa siri kwa mumewe na kumuomba msamaha, hakutaka kufa bila kutubu hiyo dhambi yake.
 
Wamasai huwa wanawezaje ku handle hizi situation?
Hata wachaga nafikiri huwa hawakatai mtoto ambaye amepatikana katika namna hiyo.
 
Amlee tu kwani shida iko wapi mkuu

Maamuzi ya marehemu yaheshimiwe, kitendo cha kuamua kumuambia ukweli baada ya miaka 7 wakati akiwa karibu kufariki maana yake ni kwamba angetaka mtoto aendelee kulelewa na huyo mwanaume basi angekufa na siri yake kama alivyoishi nayo kwa miaka 7.
Mwanamke ndiye alijua wakati sahihi wakumtambulisha mtoto huyo kwa biological father wake, ila kwa kuwa aliona yeye hana muda mrefu akaamua kulikabidhi jukumu hilo kwa mume wake, ila dhamira ya mwanamk ni kwamba mtoto wa watu lazima akatbulisjwe kwa baba yake halisii.

Upande wa mume asijifanye ana nyota ya ustawi wa jamii kutaka mung’ang’ania watoto wa watu, amtafute baba halisi wa mtoto amkabidhi mtoto wake, baba wa mtoto ndiye atoe ruhusa ya jamaa kuendelea kulea huyo mtoto.

Haya mambo ya kung’ang’ania watoto wa watu kwa misemo ya kipumbavu eti kitanda hakizai haramu au kosa siyo la mtoto ndiyo matokeo yake watoto wakikua wanatiana mimba au kuoana.

So jamaa aridhike na watoto alio nao, asimdhurumu huyo mtoto haki ya kumjua baba yake wa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…