DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Naelewa Historia Yote ya Israel,Judeans Na hata Waebrania walikotoka na ni kina nani..Ngoja nikufundishe jambo. Uyahudi una maana nne. Katika maana hizo nne ni maana Moja pekee inayo rejea katika kabila.
Uyahudi sio kabila sababu uzao wa mtoto wa Yakubu aloyeitwa Yahudha (Yuda) haipo tena sababu ulisambaratika katika yale mapigano ya dola mbili zilizo anzishwa na mtoto wa Suleyman aliye itwa Yarbiam na mwenzake aliyeitwa Rahbiam. Hawa walikuja kuanzisha dola mbili zama hizo kwa kukusanya dhuria wa nabii Yakubu, na kilikuwa kimepita kitambo kirefu sana.
Maana nyingine ya tamko Yahudi, ni kurudi nyuma kwa kumtaka msamaha Allah kutokana na matendo maovu waliyo yafanya watu, kadhalika katika maana za tamko hilo ni kurudi kwa sauti za kughuna na kupinga Ngoma, haya yalikuwa yakifanywa na viongozi wa kidini wa zama hizo. Maana ya nne, imenitoka. Ila kwa maelezo zaidi ya Historia ya watu Hawa rejea kitabu kolochoandikwa na mwanachioni aitwae Abdulkaadir Shibatulhamd.
Uyahudi ni dini, na itikadi zao ambazo kwazo zinawatofautisha na wengine, na si nasaba au kabila. Mpaka Musa anaondoka hapakuwepo Uyahudi katika ardhi hii, na hii ni kwa makubaliano ya wanachuoni wote wa Historia, na haijulikani lini kwa hakika Uyahudi ulianza.
Kwahiyo hata huyo Yahudha kipindi wanaunganishwa tena dhuria wake yeye hakuwepo, na hili limefanyika hata nabii Suleyman hakuwepo.
Kuanzia kipindi cha Eber (Baba wa waebrania na Mjukuu wa Nuhu)..
Naelewa Israel ilipojitenga na kuwa falme mbili...
Naelewa Pia Israel iliporudi tena kuwa pamoja..
Naelewa pia israel kupoteza makabila Mengine 10 na kibaki na makabila 2 ambayo ni Benyamini na Yuda kwenye vita na Wa Ashuru na Baadae kuungana kwa hizi kabila mbili kati ya Benyamini na Yuda..
Sasa swali langu nilikuuliza kuhusu Musa umenijibu kuhusu Suleyman sasa kati ya Musa na Sulemani nani Ancestor wa mwenzake..
Na kingine nikurekebishe
Yarbiam au Yeroboham alikuwa wa kabila la Efraim na yeye hakuwa mtoto wa Suleiman alikuwa mtoto wa Nabati (Nebati)..
Na kuhusu Rehoboam ndiye alikuwa mtoto wa suleiman aliyezaa na Naamah, binti wa Ammizabad..
Na hapa ndo utawala uligawanyika na Yeroboam kupewa Kutawala makabila 10..
Na suleiman kubaki na makabila 2
Narudia tena swali unasemaje Musa hakuwa Myahudi?