Bado naamini uchawi upo, Miujiza hipo na Mungu yupo bila ya shaka yeyote. Chukua muda wako nenda Kwa waganga, tembea vijijini huko utaona.
Shida watu wana-exagerate baadhi ya mambo mpaka wengine wanahisi kuwa hizi ni story za kutungwa but kabisa kabisa Kuna nguvu za Giza ambazo haziwezi kuelezewa kisayansi.
Ngoja tuangalie mifano hii ya kawaida ambayo huenda ikaonekana ya kipuuzi tu,
Wale watoto mashuleni wanaoanguka usidhani ni maigizo au matatizo ya kisaikolojia, ni nguvu za kichawi. Kwanini baadhi yao wawe na nguvu ya kuwashinda wanaume wengi? Kwanini hatujaona wale watoto wakitibiwa kisayansi? Yaani watoto wakianza kupandisha, suluhu huwa ni masheikh na mapadri. What is your comment on it?
Hivi ni kwanini baadhi ya maeneo huwa yanasifika sana Kwa uchawi, kwanini si maeneo mengine. Je ni 'tricks' tu wakazi wa maeneo hayo katika kuwazuru watu wengine? Jiulize tu kwanini cases za kujiua Kwa wahehe ni njingi? Unaweza ukasema ni genetic disposition, but je sayansi imeelezaje hutokeaji wa hiyo genetic disposition au ndio imeishia kusema tu ni 'genetic disposition'. Kwanini Salem, Massachusetts ni maarufu Kwa uchawi na si sehemu nyengine? Kwanini Misitu ya Romania inaogopwa sana Kwa matukio ya kichawi kuliko Misitu mingine? What makes this spatial variation?
Najaribu kufikiria baadhi ya mambo, nawaza ni coincidences au ni uchawi, miujiza au ni nguvu za giza. Wangapi huambiwa nitakuroga uwe chizi na hilo hutokea kweli?
Ngoja nikupe kisa hiki. Kuna kijana mmoja alisomasoma elimu ya uchawi wa kitabu (inahusishwa sana na masheikh). Basi huyu kijana akawa anatumia huu uchawi wake kuchukua wake za watu, na kuzini nao. Wengi walimuonya juu ya hilo ila kutokana na jeuri na kibri chake, huyu kijana hakuacha tabia hiyo. Baada ya muda huyu kijana alipatwa na uchizi then akafa.
Matukio kama haya ni mengi. Je uwingi wa matukio kama haya Huwa ni coincidences tu au Kuna kitu kingine.
Tunaishi katika Dunia ambayo inastaarabika, ni nadra sana kuona matukio ya uchawi hasa maeneo ya mjini kutokana na usasa. Lakini ukirudi vijijini Bado watu wanaishi Kwa kudumisha Mila zao na ni rahisi kuona miujiza. Sisi watu wa Quantum physics, sijui Geochemistry na fluid dynamics si rahisi kuexperience mambo hayo.
Wangapi ni madokta, maprofesa na wabobezi katika fani mbalimbali but still wanaamini katika hayo mambo ya miujiza na supernatural powers? Je, bado ni wajinga, elimu zao hazljawakomboa au ndio walisoma tu kujiingizia kipato?
Jamii Nyingi kote duniani kama Incas, Mayan, Aztecs, Mesopotamia, ancient Chinese, Nubian, Egyptians, Great Zimbabwe na nyengine nyingi zilikuwa Zina practice uchawi, je walikuwa wanawadangawa watu wao tu au uchawi ulikuwa una Practical uses.
Sheria za kupambana na uchawi ziliwekwa hasa nchi za Ulaya na bara la America na watu wengi waliuliwa baada ya kushukiwa kufanya uchawi, Historia inaeleza. Hivi jambo ambalo halina uhasilisia linaweza kusambaa kote duniani, tena likawa na athari zilezile?