Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Kuna miaka fulani nilifanya kazi Hospitali 1 kubwa sana ya Kanisa ipo mikoanya Kaskazini kule, sasa pale wakaja doctors from USA kwa project moja hivi tukawa tunaoshi nao na tukazoeana kbsa bcoz program zao tulikua tunafanya pa1 sasa kuna Sister mmoja ni Mnigeria nae alikuwepo miongoni mwa wanaproject 1 day anawaambia wale wazungu Kesho ni muda wa kwenda Kanisani tena anawalazimisha kabisa (WANIGERIA SI MNAWAJUA WALIVYO WAKOROFI?) Wale wazungu wakamwitikia lkn kichwani mwao walikua wanamg’ong’a

Mmoja akanifata kuniambia Sr. Z anatuambia maneno ya kwenda Kanisani wakati anasema yeye sasa mzungu huyo β€œMimi nina miaka 27 sikumbuki kanisani nilienda lini labda mama alinipeleka nikiwa mdogo” Mm sifagilii kabisa kuhusu hizo mamboπŸ˜‚ ndio utaamini waafrika wengi sisi ni makolo tunaamini mavitu tuliyomezeshwa ambayo yanatugharimu muda na hela nyingi sana
 
Religion will in the future be replaced by humanism. i.e. dont do to others what you dont want to be done to you.
 
Nadhani ingependeza zaidi ungetuambia wewe binafsi ni kitu gani umevumbua baada ya kuachana na hizo dini.

Ili tuamini kwamba kuna uhusiano hasi Kati ya dini na uvumbuzi.
Nimeipenda hii!
Inatakiwa upate ulinzi
 
Kwamba Dr Luka aloandika Injili na Matendo ya Mitume ni mungu? Na ww katika karne hii unaamini kabisa kuna mtu anaongea na Mungu live? yale yaleee, eti Muhammad aliongea na kukabwa na malaika!! low minded people!
 
Wachina ndo maana wako mbali sana kiteknolojia, na wahindi nao wanasonga sana...sie bize kujaza matumbo ya kina Mwamposa eti tutakua Mamilionea. Eti mtu unatoa sadaka ya kujimaliza. Kuna maza katoa penseni yake yote...now analilia chooni! Low minded.
 
ivi mungu ni zaifu.? mbona watu ndo humtetea mungu na dini take watu nauwa wenzao walio ikataa dini kwakigezo eti wanatetea dini yamungu au huyo mungu sio muweza wa yote na Kuna mengi hawezi?
Kuna ule upugi, mtu kanunua kitabu cha dini, anaamua kukichoma au kukikojolea, halafu nchi nzima watu wanauana, wanachoma magari, nyumba n.k kisa eti mtu kachoma kitabu cha mungu...huu ni ujuha na ujinga wa viwango vya lami. Low minded kabisa. Dini zinatupumbaza badala ya kutusaidia
 
Kwa hivyo wewe unakubali mwanaume mwenzako akuwoe ?? maana inayokataza ni dini , wasiofuata dini wanaruhusu
Hiyo ni moral demand, sio dini. Mbona watu wa dini wanafanya huu uchafu? tuseme wamefunzwa na hizo dini? Kwenye dini hizo hizo kuna wazinzi, walevi, wafiraji na wadhambi wengine.

Hivi case ya Afande (muislam) alowatuma kina Clinton (mkristo) unaifuatilia? Dhambi haina dini wala jamii.

Dini ni low minded issue!
 
Huyu mwana anajichanganya! Yeye dhambi ni ngono ngono tu! anasahau kuwa hata kusema uongo tu ni dhambi.

Dhambi ni issue ya moral authority tu. Ile dhamiri ndo inatuambia lipi baya na lipi zuri, sio lazima uwe kwenye dini ndio ujue lipi baya au lipi zuri.
 
Nadhani ingependeza zaidi ungetuambia wewe binafsi ni kitu gani umevumbua baada ya kuachana na hizo dini.

Ili tuamini kwamba kuna uhusiano hasi Kati ya dini na uvumbuzi.
Hahahaha aisee hili jibu hana hata umpe miaka alfu moja
 
Mtu Akiwa atheist ina maana haamini inachosema dini. Dini inakataza ushoga, kumwoa mama yako mzazi, dada yako nk Kwa hivyo unapoipinga dini ina maana unakubaliana na kuruhusika kuyafanya hayo yaliyokatazwa
Nikuulize, kabla ya dini kuwepo, watu ndo walikua wanafirana na kungonoka?
Acha kujichanganya. Tabia hizo ni za watu waovu ambao wamejaa kote, kwenye dini na nje ya dini.

Dini inakataza kusema uongo, wewe husemi uongo???

Low minded kabisa.

Atheism sio kutokuamini dini, Atheism ni kutokuamini imani yoyote ila kubase kwenye Fact and uhuru wa fikra, tafiti na kupata majibu kisayansi. Hizo imani za sijui majini na mashetani ni ushamba.
 
You must be joking, sayansi haijawahi jibu suala la origin of life which starts and goes hand in hand with the question of origin of universe itself, what was there before the big bang? Hiyo form four ipi inajibu swali hili?
 
Na Mimi nikuulize ni lini kulikuwa Hakuna dini ?
Jee ikiwa huna dini yaani huna kinachokukataza Zaidi ya Sayansi, Jee unaweza kuolewa na mwanamume mwenzako au kumwoa mama yako , Sayansi haisemi kitu kuhusu kutotaka au kuolewa
 
Kwa hivyo kwenye atheism Hakuna moral demand au vipi , yaani ni uamuzi wako tu kuolewa na mwanamume mwenzako au kutoolewa?
Wenye dini wanaokwenda kinyume ziko sheria Za dini, Sasa kufuatwa na kutofuata ni topic nyengine
 
Watu wasio na akili wanapenda sana kufarijiwa πŸ˜†πŸ˜†
 
Sio kweli, walio gerezani kwa Tanzania 99% ni watu wa dini kubwa mbili. Pia kuna masheikh na mapadri wengi waliokamatwa kwa kesi za ulawiti.
Dini inakataza uovu, lkn sio kwamba mwanadini hawezi kutenda dhambi hasha! Ambacho kinaliliwa hapa Ni ile hofu yakutenda maovu na ambayo inatokana na Dola pamoja na Mungu. Mwanadamu bila contro Ni mnyama amini nakwambia. Chukulia huamini Mungu then unawatoto unawapa maadili yanayotokana na Nini? Sayansi au!!
 
Nakataa, mbona naona maprofesa wakipiga magoti mbele ya sanamu? Tena katika fani ya sayansi ambapo hawezi kuamini kuwa nyoka aliongea na binadamu!!!
 
Nakataa, mbona naona maprofesa wakipiga magoti mbele ya sanamu? Tena katika fani ya sayansi ambapo hawezi kuamini kuwa nyoka aliongea na binadamu!!!
Kilichoandikwa kwenye biblia kipo vile kilivyo na unaposoma biblia vizuri unakuta hata haya ambayo unayaona Ni makosa utakuta unayaelewa kwa upana wake. Utakuta wewe ndio mwenye makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…