TANZIA Director Nisher afariki dunia

TANZIA Director Nisher afariki dunia

View attachment 2840201
Director maarufu wa video mbalimbali ikiwemo za Wasanii wa Bongofleva ambaye pia ni Mtoto wa kwanza wa Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. GeorDavie, Nic Davie maarufu Nisher amefariki saa nane na dakika tisa usiku wa kuamkia leo December 12,2023.

Familia ya Dr. GeorDavie imethibitisha kutokea kwa msiba huo wa Kijana wao Nisher na kusema msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo Jijini Arusha na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
---

Aliyekuwa Mwanamuziki, Mwandaaji na Mwongoza Video za Muziki #Tanzania, Nic Davie maarufu #DirectorNisher amefariki Dunia Usiku wa kuamkia Desemba 12, 2023 huku Familia ikiwa haijaweka wazi chanzo cha kifo chake

Nisher ambaye ni Mtoto wa Mhubiri Geor Davie amewahi kuongoza Video za Wasanii mbalimbali, baadhi ni Weusi, BenPol, (Unanichora & Jikubali), Fid Q (Bongo HipHop), Baraka da Prince (Jichunge) na Young Killer ft. Fid Q (13) na kupata Tuzo ya Chaguo la Watu (Peoples Choice Awards) kama Director Bora wa Mwaka 2014



Mimi nashangaa nimepata habari za huu msiba zaidi ya wiki moja sasa. Tena inatisha sana stori niliyopata mimi ni kwamba alifiwa na mtoto akaingia kwenye depression kubwa sana iko siku akajichoma kisu na ndivyo alivyokufa. Inasikitisha kama hivyo ndiyo alivyofariki.
 
mzee geodevie atakuwa anajua nini shida, na pengine zilitumika nguvu badala ya hekima na saikolojia katika kumhudumia... nisher kwanza wakishua, mzee ana pesa mzee ana connection, pili yeye mwenyewe mtu mkubwa, maarufu na bila shaka mzigo anao... hizo attempt za kujiua zinaonesha kuna mambo mazito yalikuwa yanamtatiza, pengine madawa, au mambo ya kifamilia.... sasa kuna uwezekano hakupata tiba sahihi ya kimwili, kiakili na kiroho (vitu vote hivi viko ndani ya uwezo wa baba yake)... sasa kuvikosa ndio huko majaribio kadhaa mpaka kufanikiwa kujiua... kifo hakina mbabe ila kama kweli ni kwa kujiua basi mzee wake atakuwa na mengi ya kujilaumu....
swala la kupoteza mtoto ni painfull lakn angepata msaada sahihi lilikuwa ni jambo la kupita, bado ni kijana Mungu angembariki mwingine.. hizo ni assumption zangu kwa sasa until further info kuhusu chanzo cha kifo chake.
Tatizo umempotezaje labda hapo ndio palimsumbua

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Taarifa sahihi ya uhakika Ni kwamba mtoto wa mtumishi wa Mungu kutoka arusha nabii GeorDavie....ajulikanaye kwa jina la maarufu NISHER amefariki dunia

Nisher amekuwa maarufu kupitia kuwa director(mwongozaji wa video za muziki bongo );amewahi kufanya kazi na wasanii wengi Sana.....taarifa zaidi zitakuja

Source:N.Y.U RADIO (ARUSHA)
 
Taarifa sahihi ya uhakika Ni kwamba mtoto wa mtumishi wa Mungu kutoka arusha nabii GeorDavie....ajulikanaye kwa jina la maarufu NISHER amefariki dunia...
Sema amejiua sio kufariki hawa manabii wa mwendokasi malipo yao ni hapahapa duniani
 
Watu wanarogwa ,ndiyo maana usimuamini sana binadamu...Zahara kawekewa sumu na ndugu zake...binadamu roho za korosho sana ,usikute wamempiga kinyama zongo cha depression.

Watu wanapigwa mapepo ya uzinzi(umalaya) ,watu wanapigwa mapepo ya wizi ili mradi wakupoteee direction ,kama ndugu wasipohangaika unapotea....Hata Chid Benzi 100% kapigwa "chuma".
Acha ujinga wa kuamini ulozi mkuu. Nchi hii ina watu wa ajabu sana wanaoamini kila kifo au tatizo kuna mkono wa mtu. Kwan Chid Benz ndio wa kwanza kula unga akapata matatizo ya afya ya akili? Kwann useme mtu kalogwa ilhali inajulikana tatizo lake ni unga? Yeyote aaminiye uchawi kwenye kila jambo ni mpumbavu na mpuuzi.

Back to Nisher, jamaa inaonekana alipata msongo mkali wa mawazo. Life is more than money, kuna watu kibao wenye hela lakini wanateswa na mambo mengine km mapenzi, magonjwa ya akili, mahusiano na wazazi n.k . Ko sa lililofanyika ni kutompeleka Nisher kwa Daktari mzuri mtaalam wa akili ( Psychiatrist)

Gary Speed ( former Wales NT football coach) siku moja kabla, alihojiwa kwenye TV akaeleza mipango mingi ya timu yake, kuonesha ni mtu mwenye mipango ya muda mrefu na furaha Ila mwisho wa siku akajiua. Alikuwa tajiri kuliko Nisher na hakuonesha dalili yoyote ya depression kumbe jamaa alikuwa anaugulia ndani kwa ndani kwa sababu ya mahusiano.
 
Acha ujinga wa kuamini ulozi mkuu. Nchi hii ina watu wa ajabu sana wanaoamini kila kifo au tatizo kuna mkono wa mtu. Kwan Chid Benz ndio wa kwanza kula unga akapata matatizo ya afya ya akili? Kwann useme mtu kalogwa ilhali inajulikana tatizo lake ni unga? Yeyote aaminiye uchawi kwenye kila jambo ni mpumbavu na mpuuzi.

Back to Nisher, jamaa inaonekana alipata msongo mkali wa mawazo. Life is more than money, kuna watu kibao wenye hela lakini wanateswa na mambo mengine km magonjwa, magonjwa ya akili n.k . Ko sa lililofanyika ni kutompeleka Nisher kwa Daktari mzuri mtaalam wa akili ( Psychiatrist)

Gary Speed ( former Wales NT football coach) alihojiwa kwenye TV akaeleza mipango mingi ya timu yake, ila usiku huo akajiua. Alikuwa tajiri kuliko Nisher na hakuonesha dalili yoyote ya depression kumbe jamaa alikuwa anaugulia ndani kwa ndani.

Wanasema kajidhuru nadhan jeraha lilikuwa kubwa mwenye ubuyu atumwagie
 
Back
Top Bottom