Division 1 ya point saba imepoteza hadhi, Shule kama Saint Francis wanafunzi "wote" wamenyoosha, nashauri kuanzishwe division 1 ya 6 na 1 ya 5

Division 1 ya point saba imepoteza hadhi, Shule kama Saint Francis wanafunzi "wote" wamenyoosha, nashauri kuanzishwe division 1 ya 6 na 1 ya 5

Hongera zao

Lakini mara nyingi hizi shule wapo kibiashara zaidi..... kwahiyo ushindani wao ni kufaulisha wanafunzi tena kwa kiwango Bora

Hivyo watafanya wawezalo ili kulinda reputation yao na kuwavuta wateja wengi zaidi!

Mwishoni mbali na kusema Kuna shortcut wanapewa ikiwa mtoto ataenda kujifunza kwa bidii akiifukuzia ndoto yake basi atatengeneza uelewaj mzurii juu yake.... Nje na hapo ndo Hawa wakienda advance wanazungusha.....
 
hamna, sasa hivi wanafunzi wana nyanja mbalimbali za kujifunza kuliko zamani, haswa private

sema all in all tanzania hakuna rigorous academics kabisa yaani
 
One iliheshimika mwisho mwaka 2012.

Ukipata hata div two wewe ni mwamba, baada ya hapo tulianza kushuhudia maigizo kibao, mara div five, sijui distinction na ngonjera kibao.
One mwisho 2006,huku kwingine wanazipata hovyo tu,1990s upate one ya saba darasa zima..maavii!.. siku hizi marks kali, kichwani hamna kitu
 
Hii imekuwa too much sasa, hawa mabinti wa saint francis wanaifedhehesha Necta 😂

Division 1 ya saba kwao imekuwa kama kumpa samaka mtihani wa kuogelea, kila mwanafunzi anaibonda !!

Shule imesha master mbinu ya kuwafanya wanafunzi wote wapate division 1 ya saba.

Nashauri kuongezwe division za ziada kama 1 ya 5 na 1 ya sita maalum kwa hizi shule


View attachment 3192124
Wanawachuja sana kwenye selection ndiyo sababu
 
Siri ya hizi shule za private ziko hivi..kufundisha wanafundisha sawa..tena wanafundisha kweli ila mkazo mkubwa upo kwenye kusolve past papers.Muda mwingi wanautumia kusolve past paers na ndio maana unaona wanafunzi karibia wote wanafaulu kwa ufaulu mmoja.Kusingekuwa na mkazo katika kusolve past papers lazima ungeona grade tofauti zipo nyingi.
 
Watanzania bhn wanafunzi wakifeli wengi huo mwaka wanaitwa mwaka wa vilaza wakifaulu sana huo mwaka unaitwa ufaulu wa mchongo.Sisi ni watu tunaopenda kusikia habari mbaya za watu
Sio hata watanzania ,haya ndo maisha ya mwanadamu hata ww ukifanikiwa wapo watakao kupongeza na wapo watakao kuponda ile mbaya
 
Lengo la Mtihani kupima uelewa. Siôyo⅞ kufelisha wanafunzi. Kama wanafunzi wamelewa sioni tatizo. Ninapokerwa ni pale naambiwa matokeo lazima yafuate "statistical normal distribution curve " . Eti wawepo waliofaulu wa chache na waliofeli wachache lakini wa wastani wengi. Eti usipopata hiyo kaavu basi Mtihani ulikuwa dhaifu ama ulikuwa na mapungufu!
 
Ndio ananipa mashaka sio siri wala sio kichwa! Hapo ndio nmegundua wanasemaga hizi shule wanafaulisha kimchongo
Form two ni rahisi sana, hawa vijana wote waliopata kuanzia 3 wajitafakari. Hata hao wa 2 wajiulize
 
Form two ni rahisi sana, hawa vijana wote waliopata kuanzia 3 wajitafakari. Hata hao wa 2 wajiulize
Shule kama kigogo secondary kuna mitoto imekula mazero
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom