Tetesi: Diwani Athumani au Wambura Camilius mmoja anaweza kuwa IGP, Selemani Mombo kwenda TISS?

Tetesi: Diwani Athumani au Wambura Camilius mmoja anaweza kuwa IGP, Selemani Mombo kwenda TISS?

Status
Not open for further replies.
Mkuu Bramo , huyo Suzy, sio tuu ni binti wa Mama Kamm, bali Mama yake mzazi ni Jaji Mstaafu Salome Kaganda aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi, huyu mama ni Mama Maadili mpaka kwenye damu, hivyo wamelelewa kimaadili, hivyo ili kukusaidia to save ya voucher na time, sikupi namba yake to help you na maimivu, utajisumbua bure na kuishia kuumia bure.

Kama unamtafuta kikazi, nenda kituo chochote cha polisi, number za maofisa wote zipo ila lazima utoe maelezo kidogo unamtafutia nini!.
P.
Waandishi nanyinyi sio watu wa kuwaamini sana,kuna bahasha za khaki mtakuwa mmepitishiwa.

Huyu binti hawezi kuwa igp, u IGP sio taasisi kwamba atasaidiwa mikakati na wasaidizi wake NO.
 
Nashauri hii Kazi apewe Mtaalamu mbobezi wa MI kutoka Jeshini.
Idara imepoteza ushawishi wake.
Ikipendeza LT GEN Mkingule apewe hii Idara.
 
Lt Gen Kombe aliuwawa,kwa maelekezo mahususi.
Aliuza Mkeka muhimu kwa Maadui.
Elimination yake iko Justified.
Vingenevyo angejiua Mwenyewe.
Aliuza mkeka gani mwamba!!?...suala lake huwa linaniumiza Sana akili,maana alijitambulisha,lakini akamiminiwa njugu Kama Rambo na wavietnam
 
Nashauri hii Kazi apewe Mtaalamu mbobezi wa MI kutoka Jeshini.
Idara imepoteza ushawishi wake.
Ikipendeza LT GEN Mkingule apewe hii Idara.

Nashauri hii Kazi apewe Mtaalamu mbobezi wa MI kutoka Jeshini.
Idara imepoteza ushawishi wake.
Ikipendeza LT GEN Mkingule apewe hii Idara.
Mabeyo alikuwa anafaa sema ndio hivyo ni CDF.. TISS wapo walio nyooka.. sema waliyumbishwa yumbishwa
 
DGIS Diwani Athumani kuondolewa, aweza kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP)

Chanzo kinadokeza kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Diwani Athumani Msuya anaenda kuondolewa na anaandaliwa kuwa Mkuu wa Polisi Tanzania (IGP)

Aidha, inaelezwa kuwa yeye na Wambura Camilius ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa kuwa IGP ingawa lolote linaweza kutokea.

Nafasi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa mpya inaonekana inaweza kumwangukia Selemani Mombo ila inadaiwa kuna presha ya kutaka TPDF idara ya Military Intelligence ndiyo itoe Mkurugenzi safari hii.

Imetoka hapa DGIS Diwani Athumani kuondolewa, aweza kuwa IGP - Imevuja!

Hawa ndo waliowahi kuwa Maboss wa Usalama wa Taifa yaani TISS;

Emilio Mzena (1961 to 1975),

Dr Lawrence Gama (1975-78)

Dr Hassy Kitine (1978-80).

Dr Augustine Mahiga (1980-83)

Lieutenant General Imrani Kombe (1983-1995).

Apson Mwang'onda (1995-2005)

Othman Rashid Othman (2005-2016).

Dk Modestus Kipilimba* (2016- 2019)

Diwani Athuman (2019-2022)

MY TAKE;

Kwa Nchi ilipofika, natamani SACP Susan Kaganda, ndo awe IGP Mpya
Kama ni uadilifu yupo Kamishna Wa Polisi anaitwa Wakuliamba. Ni mchaMungu na muadilifu.

lakini pia yupo Ahmedi MSANGI .Yule ni kiboko ya Wahalifu. Nchi Kwa Sasa uhalifu umekua mkubwa sana.
Lakini kama ni kushughulikia mitandao ya kihalifu inayohusisha baadhi ya askari Polisi basi Suzana Kaganda anafaa.

Kama tunataka Jeshi linalofanya kazi Kwa mujibu wa kanuni na Sheria basi Hamduni yule wa Takukuru anafaa sana.

Diwani ATHUMANI Hana Kashfa za Rushwa na ni mtu makini sana japo Siasa za Bashiru Ally na Polepole walisababisha ashindwe kufanya kazi yake vizuri.
Lakini ni mtu makini.
Lakini pia amekua nje ya mtandao wa kipolisi Kwa kipindi alichokua TISS.

Tatizo Kubwa lipo kwenye mitandao ya kimaslahi ndani ya Jeshi la Polisi na mashindano ya kujipendekeza Kwa wateuzi wao kwenye maeneo yenye maslahi na rushwa.
Tume ya maadili Haina nguvu kabisa kudhibiti wale wanaokiuka maadili Kwa wazi.
Mtu anakua RPC Kwa Mwaka mmoja kwenye mkoa A anajenga nyumba tatu Kwa mpigo zenye thamani ya zaidi ya Milioni mia Saba. Hahojiwi ,haulizwi , hatiliwi mashaka alimradi TU anaonekana kushabikia Chama Tawala na kudhibiti upinzani basi anakua mtu safi. Tume ya maadili imebaki kuangalia wale wanaofukuza Polisi wa chini wenye maslahi duni Kwa sababu ya pesa za kiwi wanazopewa lakini rushwa kubwa ,pesa za ujenzi wa nyumba zao ,usafiri ,pesa za kuwalipia wanaowahamisha, pesa za Kununua vifaa na vitendea kazi zinapigwa hakuna wa kudhibiti Wala mkubwa anayefukuzwa. Hapo ni kazi sana kujenga uadilifu ndani ya chombo kikubwa chenya nguvu na mtandao mkubwa unaoumgana mara nyingine na Wahalifu au wanasiasa wanakua ni marafiki na ndugu.

Ni Bora zaidi kuvunja mitandao inayotoka a na kujuana Kwa kufanya kazi pamoja na wakati Mwingine kuiba na kula rushwa pamoja na pia kujua Mikoa yenye rushwa kubwa zaidi na yenye Wafanyabiashara wakwepa Kodi,wauza madawa na magendo. Wahalifu wakubwa mara nyingi wanakua ni sehemu ya kuwapa fursa wakubwa ndani ya vyombo vya Dola na hata kuwaweka kwenye mazingira mazuri ya kujipatia nafasi hasa Kwa kuhonga au kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kuonekana kuwa ni watendaji Bora.

Ili kuvunja mitandao ya kimazoea ni vyema zaidi IGP akateuliwa Toka JWTZ pamoja na Makamishna wa tatu au wanne bila kukosa upande wa fedha na kamisheni za kimataifa zisimamiwe na kamishina kutoka JWTZ.

Vinginevyo Jeshi la Polisi liondolewe kwenye Force libaki kama service ili waondokane na mabavu ambayo wengi wanatumia kama fursa ya kujipatia maslahi Kwa vitisho na kuwafanya wananchi wema kubaki wakiwa na malalamiko yasiyokwisha huku huku raia wema wakiwaogopa Polisi na kushindwa kutoa Taarifa za kihalifu.
 
P
DGIS Diwani Athumani kuondolewa, aweza kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP)

Chanzo kinadokeza kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Diwani Athumani Msuya anaenda kuondolewa na anaandaliwa kuwa Mkuu wa Polisi Tanzania (IGP)

Aidha, inaelezwa kuwa yeye na Wambura Camilius ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa kuwa IGP ingawa lolote linaweza kutokea.

Nafasi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa mpya inaonekana inaweza kumwangukia Selemani Mombo ila inadaiwa kuna presha ya kutaka TPDF idara ya Military Intelligence ndiyo itoe Mkurugenzi safari hii.

Imetoka hapa DGIS Diwani Athumani kuondolewa, aweza kuwa IGP - Imevuja!

Hawa ndo waliowahi kuwa Maboss wa Usalama wa Taifa yaani TISS;

Emilio Mzena (1961 to 1975),

Dr Lawrence Gama (1975-78)

Dr Hassy Kitine (1978-80).

Dr Augustine Mahiga (1980-83)

Lieutenant General Imrani Kombe (1983-1995).

Apson Mwang'onda (1995-2005)

Othman Rashid Othman (2005-2016).

Dk Modestus Kipilimba* (2016- 2019)

Diwani Athuman (2019-2022)

MY TAKE;

Kwa Nchi ilipofika, natamani SACP Susan Kaganda, ndo awe IGP Mpya
Police imechafuka sana inahitaji mtu mwenye misimammo, mkali, mzoefu na mwenye ushawishi sio kutuletea mwanamke tu simply unamuona alivyo vile, kuna shida ya command tena kwa mwanamke anaweza akajikuta jeshi linamgeuka kabisa order zake zikawa toothless.
 
Mh Rais asije akaendelea kuucheza wimbo wa mwanamke anaweza, kwa kuchagua mwanamke kwenye hivi vyombo vya usalama, hasa hasa Polisi na Jwtz atajuta. Ukitaka kujua angalia Uhamiaji wanaongozwa na mwanamke hakuna cha maana kinachofanyika.
 
yule mama kusema kweli wanamdharau sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom