Wewe unataka kuwaletea Kashifa tu wanajeshi wetu. Kuna taasisi zinatakiwa kufanyiwa mabadiliko ya kimfumo na sio Mtu. Usipobadili mfumo basi ujue hata apelekwe nani bado kutaleta shida tu. Angalia hata yule Jwtz aliyepelekwa TAKUKURU na kutenguliwa , Tatizo sio yeye bali ni Mfumo uliopo na muingiliano na mambo ya siasa. The guy himself is very Smart. Angalia kule MSD mkuu wa pale ni Jwtz lakini jamaa anapigwa majungu kupita kiasi sababu tu ya Smartness yake inanyima watu ulaji. Na siajabu ataondolewa.
Kwahiyo kumpeleka Jwtz Polisi au TISS nikutaka kumpa stress tu.
U smartness wa DG wa MSD unaupima kwa kutumia nini ? Wanajeshi wengi wanaamini katika utii, Unless ueelezee maaana ya smart kwako ni nini ? Kama ni kashfa ya rushwa na yeye yumo, kama ni kashfa ya nepotism na yeye yupo kwa Taarifa za Msd . Ndio maana nimeuliza smartness yake unaipima vipi.
Au ni taasisi gani imeongozwa na mjeshi then ikafanya kitu ambacho raia wa kawaida wameshindwa kabisa ? Kwanza ni kuiba kazi za raia . Mtu ni mjeshi then unamuweka kwenye taasisi maana yake anakuwa na kazi mbili , hiyo kazi ya pili ni nafasi ya raia ambae yupo mtaani hana kazi . Hakuna kitu mwanajeshi amefanya nchi hii cha maajabu tena wengi wamefail na kusingizia raia.
Naungana na mdau kuwa shida sio individual , shida ni rotten system kuanzia Rais Mwenyewe hadi watu wake wote ni uozo na wote wanatakiwa kufanyiwa overhaul akiwapo rais Mwenyewe. Leo karne ya 21 tunagawana umeme huku tunasisitiza viwanda viwanda na kuuza umme nje , bado na still mtu anaguts za kusimama na kujitetea Eti mifumo ya zamani ilikuwa ni outdated na haikufanyiwa maboresho.
Enz ya JPM hatukuwa na shida ya umeme kiasi hiki . Hii nchi inatakiwa kuanza upya. Tatizo ni rotten system ya watesi,
Mtu kama Diwani ni mtu muadilifu sana, na Sio hata muongeaji lakini yupo kwenye rotten system ya watesi, na kwa uadilifu wake walimzunguka na kuchafua hali ya hewa .
Kwasasa wanataka kumtoa ili kuweka ile team yao , so wanakuja hapa na Vigezo vya hafai , na kumchafua fua, hii ni agenda maalum na assimilation policy ya kusafisha masalia yote ya Ngosha.
Ndio maana hii nchi haisongi mbele , kila anaeingia anaweka establishment yake.