Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Nyie watu vichwa vyenu sijui vimejaa nini ?



JIWE AKIWABANA NA KUBOBOKA KWENU NA ANAWAAMBIA KABISA HATA UHURU WA KUJIELEZA UNA MIPAKA hamtaki mnasema huo ni udikteta.






Demokrasia ina taratibu zake, ikiachwa bila kufuata taratibu itageuka vurugu, dawa ni kufuata taratibu mlizojiwekea, no more no less.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie watu vichwa vyenu sijui vimejaa nini ?



JIWE AKIWABANA NA KUBOBOKA KWENU NA ANAWAAMBIA KABISA HATA UHURU WA KUJIELEZA UNA MIPAKA hamtaki mnasema huo ni udikteta.
mmejazana huku wengi wenu mnauelewa mdogo sana, tofautisha demokrasia kati ya chama kimoja na kingine cha siasa, vipi wanatakiwa kutoa maoni yao, na demokrasia ndani ya chama, ambapo mnakuwa mnaongozwa na taratibu maalum, ukizikiuka, unaadhibiwa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubakaji ndani ya ndoa ni ruksa kwa sababu blaa blaa blaa ila ubakaji njee ya ndoa sio ruksa kwa sababu blaa blaah.


CHAMA CHA KIMALAIKA mna kazi sana.

Jamii ya IQ yako ndo inataka kumpindua nduli FISIEMU ?



we kibuyu unadhani demokrasia ndani ya chama maana yake kila mtu aropoke tu!, tena nje ya vikao vya chama?! rudini shule msikimbilie jf.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasema hayo km gear y kuunga mkono juhudi. Sasa amewahiwa juu kwa juu aondoke salaama. Ungesikia tu kesho mimi naondoka naenda ccm
Angekuwa na mpango wa kuondoka hata asingesubiri siku nyingine. Angetangaza hapohapo.
 
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.

Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.

Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.

Kufukuzwa kwa Diwani Isaya Doita kunafanya awe Diwani wa 14 katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA aliyeondoka CHADEMA baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:

Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake


Barua ya kumvua uanachama
EPUVdxeXUAA597w


Video ya tuhuma kwa Godbless Lema

Wangempa nafasi ya kujieleza/kujitetea na ikibainika ana makosa, basi angepewa tu onyo na si kumfukuza
 
CCM Ni Bora Mara Mia kuliko hii takataka inayojiita chama Cha demokrasia.
 
Barua ya kufukuzwa (iliyoandikwa na Katibu Kata wake) imetoka baada ya video ya yeye kuwasema vibaya viongozi wa Chadema Arusha ( hakumsema Lema peke yake) kusambaa kwenye social media. Sasa mtu yeyote ataviunganisha hivyo vitu. Kama kuna sababu nyingine basi waliomfukuza wataweza kuitoa. Mimi sio mwanachama wa Chadema kwa hiyo siwezi kujua kwa uhakika kama aliwahi kuwasilisha tuhuma zake kwenye vikao vya kilichokuwa chama chake. Labda wewe utuambie. Kufukuzana ovyo ndiko kulikoonyesha kuwa CUF kuna matatizo. Nisingependa Chadema nao watumbukie huko huko. Lakini mwenye macho haambiwi tazama.

Amandla.......
Kufukuzana hovyo maana yake ni nini? nani mwingine amefukuzwa? Kuunganisha unganisha mambo kisha unajipa majibu mwenyewe haiwezi kukupatia picha nzuri na sahihi kama matarajio yako. Mambo ambayo kinapitia Chadema Arusha hili wala halipaswi kuwashangaza kwa wanaoelewa na hata kufuatilia kwa undani kinachoendelea. Mwache akawasalimie aendako...
 
Mnajiandaa kubeba gamba gani safari hui ?

Wafalme wenu wapige mpunga !

Mambo ambayo kinapitia Chadema Arusha hili wala halipaswi kuwashangaza kwa wanaoelewa na hata kufuatilia kwa undani kinachoendelea. Mwache akawasalimie aendako...
 
Walishakubaliana na diwani huyu jambo la aina hiyo? Umemsikiliza anavyoongea? Eti Diwani asiongelee Mbunge asiyejitambua. Subili Mwezi November Ndo utajua maana ya akili timamu.
KASHACHELEWA KUFANYA BIASHARA YA UTUMWA...., November ndio watafanya nini?,Hata mfanyeje hakika Mtaendelea kuiogopa CDM mpaka mwisho wa Dahari.
 
Kwa Demokrasia ya Chadema, wakosoaji wakuu wa serikali ya CCM, madudu yao ndani ya Chadema hayaruhusiwi kukosolewa

Mbona mapovu tu ,vitisho vingiii, hakuna hata Point , Namna ya maongezi tu inaonesha muongeaji ni mkurupuko
 
KASHACHELEWA KUFANYA BIASHARA YA UTUMWA...., November ndio watafanya nini?,Hata mfanyeje hakika Mtaendelea kuiogopa CDM mpaka mwisho wa Dahari.
Usiseme CHADEMA, sema wachaga kujifagilia. Kwani leo hii CHADEMA ina nguvu kuliko za CUF ya miaka ile?
 
Mojawapo ya tatizo kubwa ambalo chama cha kisiasa hukumbana nalo ni pale kinapoanza kujikusanya kuwa kundi moja lenye lengo moja. CHADEMA kwa sasa inapitia kwenye tatizo hili.

Historia inaonyesha NCCR-Mageuzi ilipoanza kujikusanya kama kundi moja ilijikuta ikiwa nje kama chama kikuu cha upinzani. CUF pia wakaanza kujikusanya lakini nao pia wakajikuta wakiwa nje kama chama kikuu cha upinzani. Kuna uwezekano pia CHADEMA wakapitia njia ileile na kujikuta nje kama chama kikuu cha upinzani.

Chama cha siasa kinapokuwa hakina lengo halisi huwa ni rahisi sana kwa baadhi ya wanachama kuficha malengo yao halisi.

Kujikusanya huku kwa chama kuwa kundi moja huibua makundi matatu kama ifuatavyo;

Kundi la kwanza ni baadhi ya wanachama ambao ama wanakuwa wakubwa zaidi ya chama na kutaka kunyenyekewa au kila wanaloliamua wao lazima na wengine walifuate hata kama ni kwa maslahi binafsi.

Kundi la pili ni kuibuka kwa wanachama ambao malengo yao ni maslahi binafsi ambayo yamejificha na sio lengo halisi kama chama cha kutaka kushika dola.

Kundi la tatu ni wanachama ambao wanaamini lengo kuu la chama na kulifuata lakini hawako tayari kuishi katika unafiki wa kukubali kuendeshwa na kundi la kwanza na kuwa ‘’bendera fuata upepo’’.

Kwa mtu anayemfahamu huyu Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita atakubaliana na mimi kuwa alikuwa ni kati ya wanachama wa kundi la tatu nililolitaja. Ni Diwani ambaye aliheshimiwa sana na wananchi wa Jiji la Arusha lakini kikubwa zaidi alikuwa mtetezi mahili wa lengo kuu cha chama cha siasa.

Kuondoka CHADEMA kwa Diwani Isaya Doita kunatoa picha kubwa kuwa CHADEMA katika Jiji la Arusha kuna tatizo kubwa na muda wa kulitatua unazidi kuwa mfinyu kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Ninajua kuna baadhi ya watu hujenga fikra kwa kutumia hoja za kihemko (emotion reasoning) lakini ukweli hauwezi kudharauliwa kuwa CHADEMA katika Jiji la Arusha kuna tatizo kubwa.

Nakumbuka Mwezi January 2020, Diwani Isaya Doita alitoa tuhuma nzito zinazomuhusu Godbless Lema.

Kama unataka kusoma shutuma hizo unaweza kugonga;
LINK>>>CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Baadaye aliibuka tena Diwani wa Kata ya Sombetini Katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Ally Bananga na kutoa shutuma nyingine kwa Godbless Lema.

Kama unataka kusoma shutuma hizo unaweza kugonga;
LINK>>>Diwani wa CHADEMA, Ally Bananga amwambia Godbless Lema aache ndoto na kumpangia marafiki!

Jana Diwani Isaya Doita amejiunga CCM akiambatana na baadhi ya Madiwani wengine wa tiketi ya CHADEMA katika Jiji la Arusha.

VIDEO kuhusu alichokisema Diwani Isaya Doita baada ya kujiunga CCM.
 
Back
Top Bottom