Mojawapo ya tatizo kubwa ambalo chama cha kisiasa hukumbana nalo ni pale kinapoanza kujikusanya kuwa kundi moja lenye lengo moja. CHADEMA kwa sasa inapitia kwenye tatizo hili.
Historia inaonyesha NCCR-Mageuzi ilipoanza kujikusanya kama kundi moja ilijikuta ikiwa nje kama chama kikuu cha upinzani. CUF pia wakaanza kujikusanya lakini nao pia wakajikuta wakiwa nje kama chama kikuu cha upinzani. Kuna uwezekano pia CHADEMA wakapitia njia ileile na kujikuta nje kama chama kikuu cha upinzani.
Chama cha siasa kinapokuwa hakina lengo halisi huwa ni rahisi sana kwa baadhi ya wanachama kuficha malengo yao halisi.
Kujikusanya huku kwa chama kuwa kundi moja huibua makundi matatu kama ifuatavyo;
Kundi la kwanza ni baadhi ya wanachama ambao ama wanakuwa wakubwa zaidi ya chama na kutaka kunyenyekewa au kila wanaloliamua wao lazima na wengine walifuate hata kama ni kwa maslahi binafsi.
Kundi la pili ni kuibuka kwa wanachama ambao malengo yao ni maslahi binafsi ambayo yamejificha na sio lengo halisi kama chama cha kutaka kushika dola.
Kundi la tatu ni wanachama ambao wanaamini lengo kuu la chama na kulifuata lakini hawako tayari kuishi katika unafiki wa kukubali kuendeshwa na kundi la kwanza na kuwa ‘’bendera fuata upepo’’.
Kwa mtu anayemfahamu huyu Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita atakubaliana na mimi kuwa alikuwa ni kati ya wanachama wa kundi la tatu nililolitaja. Ni Diwani ambaye aliheshimiwa sana na wananchi wa Jiji la Arusha lakini kikubwa zaidi alikuwa mtetezi mahili wa lengo kuu cha chama cha siasa.
Kuondoka CHADEMA kwa Diwani Isaya Doita kunatoa picha kubwa kuwa CHADEMA katika Jiji la Arusha kuna tatizo kubwa na muda wa kulitatua unazidi kuwa mfinyu kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Ninajua kuna baadhi ya watu hujenga fikra kwa kutumia hoja za kihemko (emotion reasoning) lakini ukweli hauwezi kudharauliwa kuwa CHADEMA katika Jiji la Arusha kuna tatizo kubwa.
Nakumbuka Mwezi January 2020, Diwani Isaya Doita alitoa tuhuma nzito zinazomuhusu Godbless Lema.
Kama unataka kusoma shutuma hizo unaweza kugonga;
LINK>>>
CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake
Baadaye aliibuka tena Diwani wa Kata ya Sombetini Katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Ally Bananga na kutoa shutuma nyingine kwa Godbless Lema.
Kama unataka kusoma shutuma hizo unaweza kugonga;
LINK>>>
Diwani wa CHADEMA, Ally Bananga amwambia Godbless Lema aache ndoto na kumpangia marafiki!
Jana Diwani Isaya Doita amejiunga CCM akiambatana na baadhi ya Madiwani wengine wa tiketi ya CHADEMA katika Jiji la Arusha.
VIDEO kuhusu alichokisema Diwani Isaya Doita baada ya kujiunga CCM.