Diwani wa CHADEMA, Ally Bananga amwambia Godbless Lema aache ndoto na kumpangia marafiki!

Diwani wa CHADEMA, Ally Bananga amwambia Godbless Lema aache ndoto na kumpangia marafiki!

Kwa upuuzi wako huu lazima mpuuzwe tu maana mtatupigia kura badala ya sisi kupiga kura .
Wacha Bananga agombee ubunge hata urais lakini kama mnamuingiza kwenye choko choko hizi ujue na ajue atagombea nje ya CHADEMA.
Sina haja ya kubandika mikutano yenu ya manunuzi kwa sababu hamna ubavu wa kuendeleza manunuzi yenu mnapojua kuwa taarifa zenu zimebainika.
Nawatakia kila la heri wakaunge mkono juhudi.
HATUDANGANGANYIKI HATUTETELEKI
Mkuu;
Hamdanyanyiki hamteteleki wewe na nani? Jisemee nafsi yako!

Sidhani kama ana haja ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA kwa sababu chama kinapukutika polepole!
 
Hawa ndo wanaume Sasa. Lema Anaenda anapunguza convincing power mdogomdogo... Mwisho wa siku atarudi kwenye fani yake ya Gereji.
 
Jifunze basi namna ya kuandika kwa ufasaha kabla ya kuanza kujifunza kujenga hoja zenye nguvu za hoja!

Elewa kuwa kuandika sentesi kwa herufi kubwa ni kupiga kelele! Ulichofakifanya hapa ni kupiga kelele zisizoeleweka!

Hili somo ulitakiwa uwe umejifunza katika darasa la nne!
MA CCM HAYOOOO.... MAGAMBA HAYOOOOO..... MCHUMIA TUMBO HUYOOOOOO!!!! MGANGA NJAAA HUYOOOOOOOOOOO!!!!!!
 
CHADEMA katika Jiji la Arusha kunafukuta moto wa kisiasa!

Tunauona moshi wa kisiasa na kilichobaki ni moto wa kisiasa kulipuka!

Je,moto ukiwaka utakiteketeza chama au utazimwa kabla haujaleta athari kubwa!

Muda utatoa jibu sahihi!
Kabisa mkuu
 
Chadema imeshajifia huko
Diwani wa Kata ya Sombetini Katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Ally Bananga amejitokeza kwenye chombo cha habari na kudai Godbless Lema na kundi lake waache mambo ya kijinga ya kumpangia marafiki na kumtabiria kuwa anataka kuhamia CCM.

‘’Lema na kundi lake wanataka nisiwe na marafiki kutoka CCM wakati wao wana marafiki kutoka CCM’’ Bananga alisema.

Aliendelea kusema, ‘’Madiwani wote waliohamia CCM kutoka CHADEMA wataendelea kuwa rafiki zangu wa karibu, nitakula nao, nitakunywa nao kwa sababu hawaathiri utendaji kazi wangu kama Diwani. Sidhani kama kuna muda wa kupangiana namna ya kuishi. Kila mmoja alikuja CHADEMA kwa muda wake, kwa matakwa yake na kama atataka kujiondoa, atajiondoa kwa muda wake na matakwa yake’’.

Kuhusu tuhuma za kuhamia CCM, Diwani Bananga alisema, ‘’wananitabiria ndoto za manabii wajinga ambazo ni sawa na kuipigia kura kanzu ya Yesu wakati kaivaa. Bado niko CHADEMA nina wajibu na watu wa Sombetini mpaka nitakapokabidhi Kata mwezi Juni mwaka huu’’ Bananga alisema.

Bananga amesema mambo yanayofanywa ya kupangiana maisha, kuingilia familia za watu na kutuhumiana ni utoto na ujinga hasa ikichukuliwa kuwa tuna miezi michache sana kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Mimi na Diwani Isaya Doita tunapingwa ndani ya CHADEMA kwa sababu huwa hatulei ujinga’’ Bananga alisema.

Ikumbukwe kuwa, CHADEMA juzi ilitoa barua inayoonyesha Diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita amefukuzwa Uanachama wa CHADEMA baada ya kumtuhumu Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake.

Kusoma tuhuma za Lema gonga LINK> CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Kusoma thread ya Diwani Isaya Doita kufukuzwa uanachama wa CHADEMA gonga LINK> Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Diwani Bananga amebainisha kuwa hana urafiki wa karibu na Godbless Lema bali wana mahusiano ya kikazi kwa sababu Lema ni Mbunge wake na Mwenyekiti wa Kanda wa CHADEMA.

Kuhusu suala la kugombea Ubunge katika Jimbo la Arusha, Bananga amesema hakuna mtu aleyeandikiwa na daktari kuwa atakuwa Mbunge milele na atavuka mto akifika kwa sababu umri wake unamruhusu hata kugombea Urais wa Tanzania.

Kusikia kwa kirefu alichokisema Diwani Ally Bananga angalia hii Video.
 
Back
Top Bottom