Diwani wa Kawe aliyetoweka tangu Februari akutwa Tabata kwa Mwanamke

Diwani wa Kawe aliyetoweka tangu Februari akutwa Tabata kwa Mwanamke

Diwani wa CCM Wilaya ya kinondoni akijulikana kwa jina la ukoo wa Rwakatale amabaye alikuwa akitafutwa na ndugu na jamaa zake amekutwa ktk nyumba ya mwanamke mmoja aitwae Ashura huko Tabata kwa mujibu wa taarifa za polisi leo.

Polisi wanadai Mwanamke huyo kwa kabila ni mzaramo alikuwa na diwani huyo kwa wakati wote na alifika kwake akiwa ktk hali ya ulevi. Ikumbukwe kuwa Meya wa kinondoni alisha wahi kutoa taarifa za kupotea kwa Diwani huyo na akasema anazo taarifa kuwa huenda kuna watu wamemficha.

Tunaomba huyo mwanamke Ashura apewe ulinzi mkali na ajengewe Sanamu asije kudhuriwa na watu wabaya wasio litakia mema taifa hili wanao tumiwa na Mabeberu. Na pia nyumba yake iwekwe ktk orodha ya vivutio vya watalii na Mali asili ya taifa hili.
Maendeleo hayana Vyamaa.
 
Dooh [emoji15] Diwani Aliyepotea Tangu Mwezi wa Pili Akutwa Kwa Mwanamke
EATV May 24, 2022

Jeshi la polisi Kanda maalum Dar es salaam limesema Diwani wa Kata ya Kawe Mutta Rwakatare aliyetoweka tangu mwezi wa pili amekutwa nyumbani kwa mwanamke mmoja Tabata Dar es salaam

Mwanamke huyo Ashura Ally ameliambia jeshi la Polisi kuwa Diwani huyo alifika nyumbani kwake akiwa katika hali ya ulevi

Hivi karibuni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni alinukuliwa akieleza kuwa Diwani wa Kata ya Kawe Mutta Rwakatare, hajulikani alipo tangu mwezi wa pili mwaka 2022.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limesema baada ya taarifa hizo walifanya uchjunguzi wao na ufuatiliaji wa taarifa hizo na kufanikiwa kumpata diwani huyo tarehe 23/05/2022 akiwa kwenye nyumba ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Ashura Ally Matitu, miaka 43, Mzaramo mkazi wa Tabata darajani ambaye alidai kuwa Diwani huyo ni rafiki yake wa siku nyingi

Mwanamke huyo aliwaeleza Polisi kuwa diwani huyo alifika nyumbani kwake tarehe 19/05/2022 huku akiwa katika hali ya ulevi uliopindukia.

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa Kutokana na mazingira ya ulevi ambayo Diwani huyo amekutwa nayo na maombi yaliyotolewa na ndugu zake kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya matibabu, ndugu pia walitoa kumbukumbu za nyuma, mwenendo na tabia za Diwani huyo hivyo Jeshi la Polisi limemkabidhi diwani huyo kwa ndugu zake kwa matibabu na tiba zaidi za kisaikolojia
 
Diwani wa CCM Wilaya ya kinondoni akijulikana kwa jina la ukoo wa Rwakatale amabaye alikuwa akitafutwa na ndugu na jamaa zake amekutwa ktk nyumba ya mwanamke mmoja aitwae Ashura huko Tabata kwa mujibu wa taarifa za polisi leo.

Polisi wanadai Mwanamke huyo kwa kabila ni mzaramo alikuwa na diwani huyo kwa wakati wote na alifika kwake akiwa ktk hali ya ulevi. Ikumbukwe kuwa Meya wa kinondoni alisha wahi kutoa taarifa za kupotea kwa Diwani huyo na akasema anazo taarifa kuwa huenda kuna watu wamemficha.

Tunaomba huyo mwanamke Ashura apewe ulinzi mkali na ajengewe Sanamu asije kudhuriwa na watu wabaya wasio litakia mema taifa hili wanao tumiwa na Mabeberu. Na pia nyumba yake iwekwe ktk orodha ya vivutio vya watalii na Mali asili ya taifa hili.
Maendeleo hayana Vyamaa.
Nawapa pole waumini wa Mch Msaidizi Mutta Rwakatare wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B shetani alimpitia Mtumishi 🙈😭
 
Nawapa pole waumini wa Mch Msaidizi Mutta Rwakatare wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B shetani alimpitia Mtumishi 🙈😭
Kwamba ni mtumishi? Uchunguzi ufanyike, kuna harufu nainusa hapa.
 
Back
Top Bottom