PreGE2025 DJ wa Diamond, RJ the DJ atangaza "Mama Tour" kuzunguka zaidi ya mikoa 10 kumuunga mkono Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu

DJ maarufu wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, RJ The DJ, ametangaza ziara yake ya muziki inayojulikana kama "RJ The DJ Mama Tour", ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kaulimbiu ya "Naungana na Mama, Mitano Tena."

Ziara hiyo itapita katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Kigoma, Tarime, Morogoro, Dodoma, Singida, Bukoba, Shinyanga, Kahama, Arusha, Moshi, Tabora, Geita, Tanga, Musoma, Bagamoyo, Ngara, na Dar es Salaam.

Screenshot 2025-03-31 154545.png
Screenshot 2025-03-31 154845.png
 
Huyu tangu alivyozinguana na Lamata amekua kimya sana, sahv kaibukia kwenye uchawa
 
Mpunga umeingia, wasanii mda wao wa mavuno. Andika project peleka utoboe.
 
Hiyo yote ni kujipendekeza
Fuko la Pesa likikuangukia awamu hii usipokula Pesa za huyu mama sahau kula Pesa awamu nyingine huko mbele watu wanacheza na mfumo kula Pesa pita hivi
 
Wakuu

DJ maarufu wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, RJ The DJ, ametangaza ziara yake ya muziki inayojulikana kama "RJ The DJ Mama Tour", ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kaulimbiu ya "Naungana na Mama, Mitano Tena."

Ziara hiyo itapita katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Kigoma, Tarime, Morogoro, Dodoma, Singida, Bukoba, Shinyanga, Kahama, Arusha, Moshi, Tabora, Geita, Tanga, Musoma, Bagamoyo, Ngara, na Dar es Salaam.

Wanachezea pesa za walipa kodi ujinga mtupu
 
Masanii ya bongo yanayojihusisha na siasa, za watawala ni majinga tu, huwezi kukuta, wasanii wa mataifa mengine na level zao wanatumika na wanasiasa, watawala, eti hapa bongo, mpaka kwenye, viwanja vya mpira wa miguu, mashabiki yanaenda na mapango, ya watawala wanasiasa, huu ujinga, sana `Hii tabia huwezi, kukuta kule majuu, wanaenda na mabango, ya wachezaji magwiji, waliotamba, yani hapa bongo, mabango ya wanasiasa, watawala, ndio maana gani hiyo hapa bongo??
 
Nchi imekuwa ya wakata uno
Kila kijana ni mwendo kukata uno tu

Ova
Maisha ya vijana wa siku hizi hayo
Ndio maana wanakataa mpaka kuwa na wake zao na kujituma
Maisha ya kuungaunga tu
Lawama zisizoisha ubunifu zero
Mtu anawaza betting itamtoa kimaisha
 
Wakuu

DJ maarufu wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, RJ The DJ, ametangaza ziara yake ya muziki inayojulikana kama "RJ The DJ Mama Tour", ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kaulimbiu ya "Naungana na Mama, Mitano Tena."

Ziara hiyo itapita katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Kigoma, Tarime, Morogoro, Dodoma, Singida, Bukoba, Shinyanga, Kahama, Arusha, Moshi, Tabora, Geita, Tanga, Musoma, Bagamoyo, Ngara, na Dar es Salaam.

Hiyo tour itamsaidia kupata mtoto,maza mitano tena vijana hawana ajira zaidi ya kusubiria fungu la mwanao abdul maisha yasonge
 
Back
Top Bottom