Dk. Bashiru ayaonya mashirika ya kimataifa kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania

Dk. Bashiru ayaonya mashirika ya kimataifa kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
1574937608402.png

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameyaonya mashirika ya kimataifa akiyataka kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Novemba 28, 2019 wakati akizungumza na wajumbe wa chama hicho mkoa wa Magharibi mjini Unguja, Zanzibar.
Amesema ni marufuku ofisi yoyote ya CCM kufanya kazi na taasisi za kimataifa zisizokua na uhusiano na chama hicho.

Dk Bashiru amesema uwepo kwa taasisi za kimataifa nchini Tanzania isiwe sababu ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yasiyowahusu.

Mtendaji mkuu huyo wa CCM amewaonya mawaziri na watendaji wa chama hicho tawala nchini Tanzania watakaobainika kushirikiana na taasisi za kimataifa kwamba watapoteza kazi.

Chanzo: Mwananchi
 
'Amesema ni marufuku ofisi yoyote ya CCM kufanya kazi na taasisi za kimataifa zisizokua na uhusiano na chama hicho.'

Mwambieni WB, IMF, AFDB, USAID, UKAID hawana mahusiano na CCM tuone anaweza kuwafanya nini?

Hio mikwara muwe mnaipiga kwa Wafanyakazi wa Umma, wakina Nape, January, Membe etc msivuke mipaka.
 
Anawaonya watu kusema ukweli wa mambo yaliyojiri, hawa wakiamua kuacha kuingilia mambo yetu hata unga ulle wa YANGA, hatauona wala hata pata muda wa kuongea upuuzi atabaki nyumbani akishuhudia wanae wakipata utapiamlo.
 
Huyu akiwekewa vikwazo ataanza kulialia
'Amesema ni marufuku ofisi yoyote ya CCM kufanya kazi na taasisi za kimataifa zisizokua na uhusiano na chama hicho.'

Mwambieni WB,IMF,AFDB,USAID,UKAID hawana mahusiano na CCM tuone anaweza kuwafanya nini?

Hio mikwara muwe mnaipiga kwa Wafanyakazi wa Umma,wakina Nape,January,Membe etc msivuke mipaka.
 
Kwanza hadi dk hii hayo mashirika yatakuwa yashapata umbea...ole wake Bashiru!siku ht wazibe kamrija tu tutatftana balaa
 
Mwambie Mbowe aache usanii wa kifala kwanza
Jua hatuishi kisiwani, fanyeni haki muache nyodo. Nyie mna nguvu kama za Gadafi au Saadam Hussein?? sasa hivi wako wapi??
JUENI DUNIA INAZUNGUKA JUA. One day lazima utoe hesabu ya zuluma
 
unakumbuka unga wa njano!!!mbona hatukusema tunaaingiliwa na mabeberu?unakumbuka SIDA,DANIDA,etc etc mbona hutamki kuingilia na mataifa ya kigeni?watanzania sio wote wapumbavu.
 
Jamaa wanamcheki tu wanasema hiiiiii.

Jamaa alivyopata hicho cheo alipoenda kujitambulisha pale mwananchi communications akamwambia mwandishi mimi naitwa dr.Bashiru na wewe mwenzangu unaitwa Dr.Gani,mwandishi akajisemea tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii yaya gete
Kwanza hadi dk hii hayo mashirika yatakuwa yashapata umbea...ole wake Bashiru!siku ht wazibe kamrija tu tutatftana balaa
 
Back
Top Bottom