Dk. Lwaitama ahoji, kama Lissu anasema hataki maridhiano, je anataka kuchukua silaha kupambana na serikali? Asisitiza umuhimu wa mazungumzo ya vyama

Mazungumzo ya kutafuta maridhiano hayawezi kuwa ya milele kwa hiyo kwa sasa imetosha!
 
Bila
Kuendelea

Kufanya maridhiano na kitu kama ccm ni kuendelea kufanya upumbavu wa hali ya juu. Kuna vitu viwili kuacha kabisa kufanya maridhiano au kubadili mwelekeo. Kama mbwai na iwe mbwai.
Bila shaka umelewa
 
Lissu ameeleza mapendekezo yao ambayo yote CCM waliyakalia kimya "hadi baada" ya Mbowe kumpa Samia tuzo ya maridhiano ndiyo wakajibu kwa maandisha kuyakataa yote. Katika hali kama hii kuna haja tena ya kuongea na hawa watu?
 
Kauli hizi za sasa ni tofauti na zile kauli za twitter za kusapoti Lissu ni kama amefanya U turn.

Nilisema humu hata kule X kuhusu yale aliyokuwa anayasema mwanzo yalinifanya nimuone sehemu ya wale wasomi ambao wanahitaji kuelimishwa upya ili kuondoa ujinga.

Alichonukuliwa hapa walau amezungumza objectively na ndivyo msomi abavyopaswa kuwa sio kuongozwa na mahaba.
 
Lissu ameeleza mapendekezo yao ambayo yote CCM waliyakalia kimya "hadi baada" ya Mbowe kumpa Samia tuzo ya maridhiano ndiyo wakajibu kwa maandisha kuyakataa yote. Katika hali kama hii kuna haja tena ya kuongea na hawa watu?
Unaita maridhiano huku wanakataa mapendekezo? Hakuna maridhiano ki waste of time
 

Kama naweza kutumia lugha ya kitaa kuonesha point.

Kuna maridhiano, halafu kuna kuhanithiwa.

Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Haya maridhiano ya Samia ni ujinga, wapinzani wanatumiwa tu Samia apate kiki kwamba anafanya maridhiano, wakati hamna lolote.

Na hata Lissu kugomea maridhiano inaweza kuwa ni mbinu ya kupata maridhiano ya kweli.

Kwenye hili namuelewa sana Lissu.
 
Issue ya Lissu kwenye suala la maridhiano iko kwenye yale ambayo kikatiba ni haki ya wananchi, hayo Lissu hataki kuridhiana na mtu maana kikatiba ni haki raia kupewa sasa mmaridhiana nini?.

Ukiangalia topic zote za mariadhiano ndio hayo ya kwenye katiba, sasa kwanini mpoteze muda maana its either ni haki yenu mpewe au watawala wabadili katiba na kuyaondoa.
 
HUYU Mzee Lwaitama mnafiki sana,Leo anaongea hivi kesho anabadilika!! Kasharamba ASALI mrambo wenye mpango wa michongo.

😃😃 Huyu ni Confused professor 🚴🚴
 
Lissu ameeleza mapendekezo yao ambayo yote CCM waliyakalia kimya "hadi baada" ya Mbowe kumpa Samia tuzo ya maridhiano ndiyo wakajibu kwa maandisha kuyakataa yote. Katika hali kama hii kuna haja tena ya kuongea na hawa watu?
Mapendekezo hayo yalikuwa yapi? Ninavyojua yafuatayo yalikuwa sehemu ya mapendekezo:
1. Zuio la mikutano ya hadhara ya kisiasa liondolewe.
2. Kesi za kubambikwa zifutwe na mamia ya watu waliokuwa ndani waachiwe.
3. Walioomba hifadhi nchi za nje wahakikishiwe usalama wao ili waweze kurudi.
4. Wakina Halima watolewe Bungeni
5.Tume Huru ya Uchaguzi ipatikane.
6. Katiba Mpya based kwenye ili ya Warioba ipitishwe.

Hauwezi kusema CCM ilikataa yote wakati matatu ya mwanzo walikubali na kutekeleza kwa kiasi kikubwa ( kuna wafungwa hawakuachiwa). CCM walianza kupata kigugumizi kwenye hayo masuala matatu ya mwisho kwa sababu yanatishia wao kuendelea kushika dola.
1. Wakina Halima ndio wanalipa Bunge la sasa uhalali ( legitimacy) kidemokrasia kwa kuwa angalau na wapinzani.
2. Tume Huru kabisa ya uchaguzi inaweza kuja na matokeo ambayo hawayataki.
3. Katiba Mpya nayo itatikisa hegemony ya CCM.
La kwanza linavumilika kwa sababu ni wazi baada ya 2025 hawatakuwa wabunge wa "CDM " na umuhimu wao kwa CCM utakuwa umekwisha.
Ya 2 na 3 itaweza kupatikana kwa presha kutoka ndani na nje ya Bunge. Mikutano ya hadhara ina nafasi kubwa katika kufanikisha hilo.

Ingawa ile tuzo inaweza kutafsiriwa vingine lakini pengine ilihitajika ili kumpa nguvu Mwenyekiti wa CCM kusukumiza suala hili ndani ya chama chake.

Lissu alikosea katika hili. Lakini hawezi kukiri kwa sababu hapendi kukubali makosa yake. Sio pragmatic kama Mbowe.

Amandla...
 
Hayo unayosema yamekubaliwa siyo maridhiano bali hayo ni haki yao ya kikatiba ni kwa vile tu yule mwendawazimu aliyaweka kibabe. Maridhiano ilikuwa kuweka misingi mizuri ya mifumo ya uchaguzi na sheria ili yale yaliyotokea 2019 na 2020 yasijirudie tena lakini si wote tumeona yale ya 2019 yamejirudia tena na kuzidi kwani 2019 Magufuli alifuta uchaguzi wote lakini hakuua mtu lakini 2024 uchaguzi ulivuruguwa kwa 100% na zaidi wagombea wengi walitekwa,waliteswa na kuuwawa sasa watu kama hawa utafanya nao maridhiano kweli?
 
Hayo umejitungia
 
Watanzania wengi wanaoomba wapewe CV za watu wanaendekeza hulka zile zile za kipumbavu ambazzo hututambulisha kimataifa. Tuna wivu, chuki, roho mbaya za kila aina na kejeli za kijinga ambazo husababishwa na ukosefu wetu wa elimu.

Prof Lwaitama yupo kitambo sana akisikika kwenye vyombo vya habari kichekesho anayeulizia CV yake unakuta yeye form four alipata division 0.
 
Kweli kabisa
 
Mbona sasa katiba mpya haipatikani na ni haki ?

Unadhani katiba,mpya ni sawa na kwenda haja kubwa chooni?

Key boards warriors mnashangaza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…