Dk. Lwaitama ainanga kambi ya Lissu, asema kwamba kama kupendwa hata DiamondPlatnumz anapendwa sana, lakini huwezi kumpa uongozi wa chama

Dk. Lwaitama ainanga kambi ya Lissu, asema kwamba kama kupendwa hata DiamondPlatnumz anapendwa sana, lakini huwezi kumpa uongozi wa chama

Man'gana ghasarikile.

Dk. Lwaitama asema hayo wakati akihojiwa na SAUTi DIGITAL. Kwamba uongozi wa chama ni suala nyeti zaidi ya kupendwa tu. Dk. Lwaitama alieleza kwamba kama ni kupendwa, Diamond Platinum anapendwa kuliko hata Lissu lakini huwezi kumpa uongozi wa chama.

Dk. Lwaitama alisema kwamba unaweza kuwa mchambuzi mzuri tu, lakini haukidhi kuwa kiongozi Mkuu wa chama.

Dk. Lwaitama amewataka wajumbe waangalie vigezo vya msingi, wasiongozwe na mihemuko wakachagua mtu ambaye chama kikipata dharura ya fedha, yeye hana hata mia, hata gari hana, hivyo chama kinaweza kuyumba.

Dk Lwaitama alisema kama hoja ni kumuondoa mtu aliyekaa muda mrefu, hata Lissu amekaa zaidi ya miaka 15 katika nafasi za juu, kwa hiyo kama ni hoja ya kubadili uongozi, hata Lissu inamgusa kwa kuwa amekaa muda mredu, na kwamba watu wapya ni Odero au Mapunda.

View attachment 3190522
Money talk everywhere
 
DR Lwaitama anataka kiongozi mwenye hela hata chama kikiyumba kifedha anaweza kuingia mfukoni mwake hapa anamanisha kama huna hela huwezi kuongoza chama, kigezo cha kupendwa na wanachama sio kipaumbele sana...kigezo cha kukaa muda mrefu kwenye uongozi yeye haoni kama ni shida...anamfananisha lisu na Diamond kwenye siasa huku mmoja ni mwanasiasa na mwingine ni msanii wa mziki...Hizi hoja hazina mashiko kabisa.
 
Lwaitama yuko sahihi
 
Ohoooo Dokta kapiga U-turn mbele ya Traffic police...
 
Man'gana ghasarikile.

Dk. Lwaitama asema hayo wakati akihojiwa na SAUTi DIGITAL. Kwamba uongozi wa chama ni suala nyeti zaidi ya kupendwa tu. Dk. Lwaitama alieleza kwamba kama ni kupendwa, Diamond Platinum anapendwa kuliko hata Lissu lakini huwezi kumpa uongozi wa chama.

Dk. Lwaitama alisema kwamba unaweza kuwa mchambuzi mzuri tu, lakini haukidhi kuwa kiongozi Mkuu wa chama.

Dk. Lwaitama amewataka wajumbe waangalie vigezo vya msingi, wasiongozwe na mihemuko wakachagua mtu ambaye chama kikipata dharura ya fedha, yeye hana hata mia, hata gari hana, hivyo chama kinaweza kuyumba.

Dk Lwaitama alisema kama hoja ni kumuondoa mtu aliyekaa muda mrefu, hata Lissu amekaa zaidi ya miaka 15 katika nafasi za juu, kwa hiyo kama ni hoja ya kubadili uongozi, hata Lissu inamgusa kwa kuwa amekaa muda mredu, na kwamba watu wapya ni Odero au Mapunda.

View attachment 3190522
Hii post nimeipenda sana.
 
Demokrasia inataka watu waongozwe na mtu wanayempenda.

Kupendwa ni hoja namba Moja ya demokrasia na mtu kuwa kiongozi
kikwete wakati anataka kutia nia, mkapa alitaka kutia ngumu, wakamwambia mkapa huyu mtu anapendwa sana na JWT(JUMUIYA YA WANAWAKE)
mkapa aliposikia hivyo akajua huyu ni mtu wa kina mama, ikabidi abwage manyanga amuache ndo maana alipata kura nadhani 83%
waliompenda gafla walimchoka 2010 cha moto alikiona.
hivyo kupendwa ni mentality tu kama hujaperfom unamwagwa.

hivyo lisu anapendwa kwa sababu ya ukichaa wake, akipewa 1 yr wanammwaga.
 
Dr anaendelea kudhihirisha kuwa 2020 hakuna kura ya CHADEMA iliyoibiwa katika uchaguzi wa Uraisi,isipokuwa hata CHADEMA wenyewe walijua kabisa kuwa walikuwa wamempa mtu kijiti ambae hafai kuwa kiongozi,vinginevyo Dr afute kauli yake,pia Dr ajue kila mtu anapendwa kulingana na sekta au eneo lake ,sasa kuMlinganisha Diamond na Lisu , hii haipo sawa kabisa,Lisu mwanasiasa,Ukimpandisha Kwenye jukwaa la muziki hatopendwa kwa sababu siyo eneo lake hilo,Diamond msanii ukimpandisha kwenye jukwaa la muziki atapendwa kwa kuwa ndio eneo lake, lakini Diamond anaongoza taasisi kama Wasafi moja ya taasisi zinazofanya vyema na kutengeneza ajira,ila siyo ajira ya kisiasa
Huyu "MBONA WEWOOOOO" anakwenda kukiua chama. DJ pamoja na mapungufu yake lakini ana Haiba ya uongozi wenye msingi wa HEKIMA NA BUSARA sana. CDM rejesheni DJ pigeni chini Mbona wewooo
 
Huyu "MBONA WEWOOOOO" anakwenda kukiua chama. DJ pamoja na mapungufu yake lakini ana Haiba ya uongozi wenye msingi wa HEKIMA NA BUSARA sana. CDM rejesheni DJ pigeni chini Mbona wewooo
Kweli kabisa
 
Lisu anapendwa au anahurumiwa!!?Hivi Mrema alitwngeneza wanasiasa wangapi!!?Cheyo ametengeneza wangapi!!?Lisu ametengeneza wangapi!!?Lipumba ametengeneza wangapi!!? Mbowe ametengeneza wangapi!!?(Maana kati ya chama upinzani ambacho kimetengeneza viongozi ni Chadema au Mbowe).Tunakumbuka Nyerere alitengeza wanasiasa wengi au viongozi wengi.
 
mzee Lwaitama anajitahidi sana leo kueleza ukweli :pulpTRAVOLTA:
Mwenye akili awez kumuunga mkono mtu kama LiSU bahati nzuli tumemjua vizuli kabla ya uchaguzi wowote yule abaki Wakili ndiio kazi inayomfaaa kutetea watu ila uhongozi apana atachekesha watu ataumiza watu. Atakamua watu na mikodi kibao!!.
 
Back
Top Bottom