Dkt. Ashatu Kijaji: Biashara Kariakoo zinaendelea, wafanyabiashara wametumia Demokrasia na Uhuru wao kufungua au kutokufungua

Dkt. Ashatu Kijaji: Biashara Kariakoo zinaendelea, wafanyabiashara wametumia Demokrasia na Uhuru wao kufungua au kutokufungua

ameamua kubadilisha maneno kutoka mgomo kuwa uhuru wa kufunga na kufungua maduka,
Yuko happy anagonga meza hana wasiwasi kiongozi shupavu aliyeaminiwa na Mh. Rais!
Na posho juu anapata.
 
Hivi kuna mgomo au? Manake Ukiona picha unaona vipeperushi Ati "Kamata Kamata ya TRA yawafukuza wanunuzi wa Nje" na Wachuuzi wakiendelea na Biashara!

.Nilifikiri mgomo huu ni wa kukataa Sheria ya Usajili wa Store/Stoo za Bidhaa.
Kuna Siasa za Uharakati hapo?
 
#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amewataka wafanyabishara wanaofanya biashara katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, kuendelea na biashara hizo, baada ya wafanyabishara hao kugoma kufungua biashara hii leo.

Makalla ametembelea eneo la Kariakoo na kushuhudia maduka mbalimbali yakiwa hayajafunguliwa ambapo wafanyabiashara hao wamegoma kwa kile wanachoeleza kuwa ni kutokana na kuongezeka kwa gharama nyingi za ulipaji kodi na kamata kamata wanayokumbana nayo. #EastAfricaTV

1684138225454.png
 
#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amewataka wafanyabishara wanaofanya biashara katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, kuendelea na biashara hizo, baada ya wafanyabishara hao kugoma kufungua biashara hii leo...
Huyu jamaa anakuaga mbabe sana huyu.
Kijana wa J.K
 
Mbunge wa Makete mh Festo Sanga ameliambia bunge kwamba 50% ya Wafanyabiashara wa Kariakoo wanatoka kwenye Jimbo lake la Makete ( Wakinga)

Source TBC

Je, Sanga yuko sahihi au amelidanganya bunge?
 
Huyu mama huwa ni mjinga sana (samahani)
 
Hii kupeana uwaziri kijinsia sasa mambo Sio mambo Huku kariakoo.

Uwezo wa Huyu Waziri ni mdogo sana sana.
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la Bunge la 12 Mkutano wa 11, Kikao cha 25 leo Mei 15, 2023.



WAZIRI MASAUNI: SERIKALI HAIJAJIRIDHISHA URAIA PACHA NI MATAKWA YA WENGI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema “Bado Serikali haijajiridhisha kwamba uraia pacha ni takwa la Wananchi wengi, ndio maana hata katika mchakato wa katiba uliokwama hakukuwa na pendekezo, Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanzisha utaratibu wa Hadhi Maalum kwa Watanzania waliochukua uraia wa Nchi nyingine.”

Awali, Mbunge Agnesta Lambert Kaiza alihoji kama Serikali haioni haja ya kuwasilisha Muswada wa marekebisho wa uraia Pacha akieleza kuwa kuwakana Watanzania wanaochukua uraia wa Nchi nyingine ni sehemu ya ubaguzi.

MWONGOZO KUHUSU MGOMO SOKO KUU LA KARIAKOO
Mbunge wa Makete Festo Sanga ameomba mwongozo wa Spika kuhusu mgomo unaoendelea kwenye soko la kariakoo ukihusishwa na kamata kamata pamoja na changamoto zingine za ukusanyaji wa mapato.

View attachment 2622501
Festo Sanga, Mbunge wa Makete
Sanga amesema kuendelea kwa mgomo huu kunakosesha taifa mapato, pia mikoa inatikisika kwa kuwa wafanyabiashara wengi nchini huchukua biadhaa hapo.

Akitolea maelezo ya kinachoendelea kariakoo muda huu, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema "Kumekuwa na majadiliano ambayo yanaendelea kati ya Serikali na wafanyabiashara wetu ambao wapo kariakoo, kuhusu hoja zao mbalimbali ambazo wanatamani Serikali izifanyie kazi na mpaka sasa hivi tunapoongea Mhe. Spika, Mhe. Mkuu wa Mkoa pamoja na wataalamu wetu kutoka wizara ya fedha, wizara ya viwanda na biashara wapo kwenye kikao na uongozi wa wafanyabiashara wa kariakoo"

View attachment 2622490
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji
Ameongeza, "Na yapo baadhi ya maeneno ndani ya Kariakoo ambayo shughuli zinaendelea na wengine kama ilivyo uhuru wa kila mtu kufanya kile anachokiona, anatakiwa kukifanya, wengine wamefunga maduka yao wengine maduka yanafanya kazi"

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Bunge halitajadili hoja hii kwa sasa hadi pale atakapojiridhisha kuwa madai ya Mbunge Festo Sanga yana ukweli, pia kwa kuwa jambo hilo linafanyiwa kazi na Mkuu wa Mkoa.

Katika Mwendelezo wa Sakata hili, Mbunge Hawa Mwaifunga amesimama kuomba pia mwongozo ambapo amesema Wafanyabiashara wamegoma kufungua maduka yao hadi siku ya Alhamisi watakapopatiwa majibu ya malalamiko yao.

View attachment 2622494
Hawa Mwaifunga, Mbunge wa viti maalumu
Amedai pia kauli ya Waziri wa Viwanda kuwa baadhi ya maduka yamefunguliwa sio ya kweli kwa kuwa hakuna duka lolote lililofunguliwa, na kuna onyo kwa wafanyabiashara yeyote atakayefungua biashara ni halali ya wengine.

Waziri Dkt. Ashatu Kijaji amesisitiza kuwa "Wapo wafanyabiashara waliotumia uhuru wao kufungua maduka na wapo waliotumia uhuru wao kufunga maduka, ni demokrasia, hakuna mtu anayelazimishwa kufanya jambo"

Amesema kwa sasa Serikali bado ipo kwenye mazungumzo na wafanyabiashara na ikitokea kuna maelezo mengine atayatoa.

SPIKA ASITISHA BUNGE BAADA YA HITILAFU YA UMEME
Shughuli za Bunge Jijini Dodoma zimesitishwa kwa muda hadi saa kumi jioni kutokana na hitililafu ya umeme ndani ya Bunge

Spika Dkt. Tulia Ackson amelazimika kusikitisha shughuli hizo saa nne asubuhi ya leo Jumatatu Mei 15, 2023

hizi nchi zetu bwana,tatizo la umeme mpaka bunge linaahirishwa,mara uwanja wa taifa.kweli afrika ni bara la giza.
 
Mbunge wa Makete Mhe. Sanga ameomba Bunge lijadili kwa dharura mgomo wa Kariakoo.

Spika amemuuliza Waziri wa Biashara ambaye amejibu hakuna mgomo ila Wafanyabiashara wametumia uhuru wao wa kufunga au kufungua.

Festo Sanga amesema anazo taarifa kamili kwa sababu 50% ya Wafanyabiashara wa Kariakoo wanatoka Makete.
Nyakati zile tusingekuwa naye huyu na hawa ndio wanamfanya maza aonekane hajui kulea watoto kuliko baba.
 
Back
Top Bottom