Dkt.Ayoub Rioba : Katiba Mpya Isaidie Kukabili Mifumo ya Unyonyaji wa iliyoachwa na wakoloni

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607

Mtoa hoja huyo amesema anaunga mkono upatikanaji wa Katiba Mpya, akisisitiza kuwa haungi mkono chama chochote cha siasa kwa upendeleo, bali hutathmini vyama vya CCM, CHADEMA na vingine kwa kuzingatia hoja na utendaji wake.​

Ameeleza kuwa, ingawa Katiba Mpya ni muhimu katika kujenga taifa lenye haki, usawa na amani, haipaswi kuangazia mgawanyo wa madaraka pekee, bali pia kuweka misingi ya kukabiliana na mifumo ya kiuchumi ya kimataifa inayodaiwa kuendeleza unyonyaji wa nchi za Afrika.

=============

Ndugu zangu nawashukuru sana kwa mijadala tunayoendelea nayo ktk ukurasa wangu.
Kwa wanaofuatilia kwa fikra tunduizi watakuwa wamebaini kuwa mimi sipo hapa kuwa chawa wa chama chochote!

Katika mijadala yangu, nimewasema CCM kama nilivyowasema CHADEMA na vyama vya ushindani!
Tofauti na mashambulizi ninayoyapata hasa kutoka kwa wapenzi kindakindaki wa vyama vya ushindani, mimi huwa ninajiuliza maswali rahisi tu:

Mara zote ni kama hayajibiwi! Natambua wapo makomredi ambao wamedhihirisha kunielewa na ninawashukuru, mnaweza kufuatilia michango yao!

Mimi sipingi sisi kuwa na katiba mpya! Wala sipingi CHADEMA - au Chama chochote kile kuingia madarakani! Nitafurahi sana siku nikiona chama cha ushindani kimeingia madarakani ili nacho kionje joto ya jiwe!
Ninachohoji siku zote - na ningependa muelewe - ni kile kinachoweza kutusaidia kubaini kuwa matatizo ya Afrika - pamoja na ufisadi, ukatili na uonevu wa baadhi ya viongozi wa Afrika - yanachangiwa na mifumo ya dunia iliyowekwa na wakoloni!

Nimesema, hizi katiba zetu, hata tuzikarabati kiasi gani - ninaunga sana mkono mabadiliko ya katiba - hazina majawabu kwa changamoto zetu zote!

Nimejenga hoja kuwa, kuna ushahidi mwingi unaothibitisha kuwa, hata nchi za Afrika zilizobadilisha katiba na kuweka katiba sawa na ya Marekani, bado zina matatizo yale yale ya mataifa ambayo hayajabadili katiba!
Ninesema vipo vigezo vya kiuchumi vinavyothibitisha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vema zaidi kiuchumi na ktk maeneo mengine, kuliko nchi zilizobadili sana vyama madarakani!

Hili sikutaka kulisema, lakini ninalazimika kulisema ili kukamilisha hoja yangu! Ipo nchi jirani ambayo imebadili sana vyama madarakani na mwaja jana kiongozi wake ni kama vile alitutukana Watanzania kwa sababu ya changamoto za Oktoba 29.

Lakini nchi hiyo hiyo vijana wake wamejaa Tanzania, wakifanya kazi za ndani, usafi, ulinzi na zingine ambazo vijana wa Tanzania hawazijali!

Na ktk bandiko langu la mwisho niliuliza ni kwa nini sisi Waafrika hatujachangamkia nafasi nyingi ambazo leo wageni kutoka nje ya Bara letu wamekuwa wakizichangamkia na zinawatajirisha?

Na ni kwa nini changamoto hii ipo Afrika nzima, zikiwamo nchi zilizobadili katiba na hata vyama madarakani? Nikasema, China, kwa mfano, haikubadili katiba kufikia maendeleo ya watu wake iliyofikia leo! China iliamua kujitambua tu, basi!

Hoja yangu ni moja tu: Waafrika tunawajibika kutafuta kiini cha changamoto zetu kwa kutumia fikra tunduizi badala ya kudhani kwamba fikra mihemuko zitatutatulia matatizo yetu, ambayo yamesababisha tuonekane kichekesho cha dunia!

Kwa hiyo, hapa ninaunga mkono jitihada za CHADEMA na wanaharakati wote kwamba tupate katiba mpya itusaidie kuwa na taifa bora zaidi, lenye usawa, haki na amani, kama ilivyosadifiwa ktk katiba ya TANU.

Aidha, ninasisitiza kwamba katiba mpya isijadili tu mgawanyo wa madaraka miongoni mwa wanaowania madaraka, bali iweke vifungu vya kutusaidia kupambana na mifumo ya kinyonyaji ya kimataifa iliyowekwa na mabeberu toka enzi za utumwa!

Kwangu mimi, hayo ndiyo mapambano tunayopaswa kuwa nayo leo, kama Waafrika! Kinyume na hapo, tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu, huku tukijiaminisha kuwa tunatafuta demokrasia!
Chanzo : DKT Ayoub Rioba
 
hili nalo takataka mavi
 
Back
Top Bottom