Katiba Mpya au Chama Kipya? Je, Tunataka Kubadili Mfumo au Viongozi?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Watanzania tunahitaji mabadiliko, na wengi tunaamini kuwa Katiba mpya ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo

Tunatarajia itasaidia kurekebisha mifumo yenye changamoto kupunguza migogoro na kuweka mipaka na uwajibikaji katika matumizi ya madaraka

Lakini binafsi napokua nafatilia mijadala kuna maswali hua yananijia kicwani

Moja ya swali ni hili👇

JE, TUNAPIGANIA KATIBA MPYA KWA AJILI YA KUBADILISHA MFUMO, AU TUNATAKA KUBADILISHA CHAMA KILICHO MADARAKANI?

Kwa mfano, CHADEMA wakiingia madarakani je, bado tutadai Katiba mpya kwa nguvu ileile, au msimamo wetu utabadilika kwa sababu tu chama tunachokitaka ndicho kinachoongoza?

Tujadili: Je, tunataka mfumo bora utakaomfunga kila kiongozi, au viongozi tunaowaamini ndani ya mfumo uliopo?

Karibu kwa maoni 🫡

ShesRise_1 ✋️
 
Viongozi bora.

Ukiwa na kiongozi mzalendo kwa nchi na ana akili kubwa, katiba sio ishu sana ila ukiwa na viongozi wapuuzi hata ukiwa na katiba nzuri vipi haina maana yoyote, ndicho kinawakuta Marekani.
Kwahiyo kumbe swala la katiba sio muhimu sana kama tuna viongozi bora

Vipi kama kiongozi akibadilika licha ya kua mwanzoni alionekana mzalendo

Si unajua binadamu
Kuna msemo madaraka yanalevya.
 
Katika rank mtiririko kwa ubora ni
1. Demokrasia na Maendeleo- Canada, Scandinavia, US, Japan, Ulaya, South Korea
2. Maendeleo bila demokrasia-China, Singapore, Russia, GCC
3.Demokrasia bila maendeleo-Kenya, Malawi, Senegal, India
4. Udikteta bila maendeleo- Tz, Uganda, Rwanda, Cameroon
5. Machafuko tu ya kudumu- DRC, Somalia, Sudan, Haiti, Yemen
 
Watanzania shida yetu kubwa ipo vichwani mwetu, siku tukijua ni kwa namna gani sisi ndo virusi wa nchi hii haya mambo madogo madogo kama katiba, mifumo & viongozi vitarekebishika haraka sana.
Heb tufumbue macho kwanza
Shida yetu ni nini hasa
 
Katika rank mtiririko kwa ubora ni
1. Demokrasia na Maendeleo- Canada, Scandinavia, US, Japan, Ulaya, South Korea
2. Maendeleo bila demokrasia-China, Singapore, Russia, GCC
3.Demokrasia bila maendeleo-Kenya, Malawi, Senegal, India
4. Udikteta bila maendeleo- Tz, Uganda, Rwanda, Cameroon
5. Machafuko tu ya kudumu- DRC, Somalia, Sudan, Haiti, Yemen
Hizi takwimu umezipata wapi nikajionee
 
Watanzania tunahitaji mabadiliko, na wengi tunaamini kuwa Katiba mpya ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo

Tunatarajia itasaidia kurekebisha mifumo yenye changamoto kupunguza migogoro na kuweka mipaka na uwajibikaji katika matumizi ya madaraka

Lakini binafsi napokua nafatilia mijadala kuna maswali hua yananijia kicwani

Moja ya swali ni hili👇

JE, TUNAPIGANIA KATIBA MPYA KWA AJILI YA KUBADILISHA MFUMO, AU TUNATAKA KUBADILISHA CHAMA KILICHO MADARAKANI?

Kwa mfano, CHADEMA wakiingia madarakani je, bado tutadai Katiba mpya kwa nguvu ileile, au msimamo wetu utabadilika kwa sababu tu chama tunachokitaka ndicho kinachoongoza?

Tujadili: Je, tunataka mfumo bora utakaomfunga kila kiongozi, au viongozi tunaowaamini ndani ya mfumo uliopo?

Karibu kwa maoni 🫡

ShesRise_1 ✋️
tun

Tunawe kupata viongozi bora lakini tukachelewa sana kupata mfumo bora. mfano halisi ni Tz bongo.
mifumo bora utoa viongozi bora.
mfumo ukiwa bora sometimes mnaweza mkapata viongozi wajinga wajinga lakin mambo yanaenda kwa usawia.
 
Shida yetu ni kutokujitambua na hii inatokana na mifumo waliotuachia wakoloni kuanzia sheria, elimu na dini
Sio Tanzania tu ni Afrika nzima, ndiyo maana serikali yeyote inayojaribu kuleta maendeleo/mabadiliko huwa zinaangushwa na west
Kiufupi bado tupo chini ya wakoloni wao ndio wanaamua tuishi vipi hivyo hata tukileta katiba mpya au kuwa na viongozi tofauti hali ya uchumi itaenda namna mabeberu wanavyotaka na sio otherwise

Japokua Africa ineanza kuamka kuna vizazi vitaleta mabadiliko sababu hakuna lenye mwanzo lisilokua na mwisho

Angalia serikali zote Africa ambazo zina survive ni kama CCM, Museven, Kagame, Biya etc hao wote ni wale ambao wanakandamiza democracy
Ukitaka kupotea wewe jifanye unaleta maendeleo kama Uncle magu, Gaddafi etc
 
tun

Tunawe kupata viongozi bora lakini tukachelewa sana kupata mfumo bora. mfano halisi ni Tz bongo.
mifumo bora utoa viongozi bora.
mfumo ukiwa bora sometimes mnaweza mkapata viongozi wajinga wajinga lakin mambo yanaenda kwa usawia.
Naunga mkono hoja

Ila naomba nieleweshe unaposema
Nakunukuu:👇
Tunaweza kupata viongozi bora lakini tukachelewa sana kupata mfumo bora. mfano halisi ni Tz bongo.

Hapa unataka kusema je ?
 
Back
Top Bottom