Katiba Mpya au Chama Kipya? Je, Tunataka Kubadili Mfumo au Viongozi?

Katiba Mpya au Chama Kipya? Je, Tunataka Kubadili Mfumo au Viongozi?

Shida yetu ni kutokujitambua na hii inatokana na mifumo waliotuachia wakoloni kuanzia sheria, elimu na dini
Sio Tanzania tu ni Afrika nzima, ndiyo maana serikali yeyote inayojaribu kuleta maendeleo/mabadiliko huwa zinaangushwa na west
Kiufupi bado tupo chini ya wakoloni wao ndio wanaamua tuishi vipi hivyo hata tukileta katiba mpya au kuwa na viongozi tofauti hali ya uchumi itaenda namna mabeberu wanavyotaka na sio otherwise

Japokua Africa ineanza kuamka kuna vizazi vitaleta mabadiliko sababu hakuna lenye mwanzo lisilokua na mwisho

Angalia serikali zote Africa ambazo zina survive ni kama CCM, Museven, Kagame, Biya etc hao wote ni wale ambao wanakandamiza democracy
Ukitaka kupotea wewe jifanye unaleta maendeleo kama Uncle magu, Gaddafi etc
Shukran kwa maoni mkuu napenda kama hivi karibu sana

Kwahiyo unataka kusema matokeo ya matendo ya viongozi wetu ni kwa sababu hawana option?

Kwa maana bado sisi tupo chini ya mabeberu kiasi kwamba yoyote ataethubutu kwenda kinyume na mabeberu inakula kwake kama Magufuli na hao wengine?

Kwani Magufuli aliondolewa kwa hisani ya mabeberu ?

Sio wana mtandao kwa mjibu wa pole pole?
 
Naunga mkono hoja
Shukran kwa maoni
Watu wa tume ya uchaguzi wasipokee maagizo.
Shida sio ccm kuwa madarakani Bali wanaingiaje madarakani?
kama wananchi wanawataka wao basi watawachagua sio mpaka waibe na kutengeneza kura feki.
 
Watu wa tume ya uchaguzi wasipokee maagizo.
Shida sio ccm kuwa madarakani Bali wanaingiaje madarakani?
kama wananchi wanawataka wao basi watawachagua sio mpaka waibe na kutengeneza kura feki.
Imagine Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi
Anachaguliwa na mwenyekiti wa ccm

Yaani hili hata mtoto wa darasa la pili linaweza kumshangaza sana

Waliotunga hizi kanuni aiseee
 
Nafikiri wananchi HASA HASA wanataka MAISHA BORA, gharama za maisha zishuke,bei ya bidhaa na huduma zishuke,mazingira rafiki na mazuri ya biashara na shughuli za kiuchumi,gharama ya bei ya umeme,GESI ya kupikia,tozo nankidi za biashara,fursa za ajira, MAISHA BORA KWA UJUMLA BASI halafu na SIMBA NA YANGA..na wasanii wao..bongo muvi na bongo fleva..na pespsi baridi basi

wengi WA WANANCHI hata hawajui katiba ni Nini?ya ZAMANI ipoje?..wengi hata hawana vyama sio wanachama.wa CHAMA chochote na Wala HAWAENDI KUPIGA KURA.

hata Mimi sijawahi KUPIGA kura...

Kiongozi kama mzee RUKSA alifanya MAISHA BORA KWA kila MTU..ndio vitu wanachi wanataka.

watu wakapata RUKSA kuvaa nguo za mitumba bila kuulizwa risiti.kununua sukari bila kupanga foleni..Maisha yakawa Bora kwa kwa WANYONGE.
 
Sawa , lakini hayo yote uliyotaja hapo unadhani yatapatikana vipi?
 
Tunahitaji viongozi bora katika mfumo wa katiba bora, ila basi hata ikishindikana hivyo tupate tu viongozi bora bila hata katiba nzuri kama China.
Mmmh bora katiba.

Ukisema hivo itakuwa kama enzi za Magufuli
 
Mie wala sikusema alikua kiongozi bora ni mdau hapo juu mi nimekazia tu swala la katiba
Sasa kwa nini umesema itakuwa kama enzi za Magufuli na sio kama enzi za Samia?!
 
Na mi pia naona hivyo
Katiba itaweza kumbana yoyote
Katiba nayo inaendana na culture ya watu, maarifa na mwamko wao. Huwezi kulazimisha katiba ya kumbana kiongozi katika jamii ambayo hakuna utamaduni huo. Utamaduni wa Tanzania kwa sehemu kubwa ni wakubwa hawakosei, kuanzia kwenye familia, ukoo, mtaani mpaka ngazi ya taifa.
 
Katiba nzuri ni muhimu ila tatizo la Waafrika liko zaidi kwenye IQ kuwa ndogo kwa majority ya watu na utamaduni.
 
Back
Top Bottom