CCM inapaswa kutangazwa ni kikundi haramu. Na huyu Bashiri ni kiongozi wa genge haramu. Akamatwe ashtakiwe kwa makosa ya uhaini na kuongoza genge haramu.Kikwete akiamka huko na vijembe vya kikwere mnaanza kutafutana kumbe mnatafuta wenyewe mstaafu wa watu.
Kwa mwaka huu mfano tunao kwenye serikali za mitaa CCM ilipita bila kupingwa.
Awamu iliyopita walikua wanang'ata na kupuliza ila sasa hivi mnang'ata tu mpaka wananchi wanaona kinachoendelea bila kificho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Al Bashir
Mpuuzi kweli huyu dikteta wa Sudan
Uliwahi kusema maneno haya mazuri wakati yuko madarakani, au unamponda marehemu?
Duh!!Kikwete atavuna alichopanda , jini alilolifuga sasa limekata fensi
Mkuu,"Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wana imani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana"
Kwa kunukuu tu hayo machache hapo juu, wana CCM hamna Katibu Mkuu ndani ya ofisi yenu nyeti yenye kupaswa kuratibu shughuli za chama, bali bomu lenye kukibomoa na kukipasua chama chenu. Badala ya kufanya juhudi ya kuwaunganisha wanachama na makundi hasimu ndani ya chama, yeye anazidi kukoleza moto.
Atamponza hata huyo anayemsifu na kumuabudu. Ama atakipasua chama chake na kutokea pande lenye nguvu la chama cha kipya cha upinzani chenye nguvu na imara ili utabiri wa Mwl. Nyerere ukapate kutimia. Ama la, atamwingiza anayemsifia ktk historia ya kuwa Rais wa kwanza kutawala kwa miaka mitano tu ndani ya nchi hii.
Sent using Jamii Forums mobile app
BashiruHuo ni ushahidi kwamba CCM ina demokrasia ya kusema ukweli bila kumungunya maneno.
Mlitaka bashiru aseme uongo ili chama kionekane kama kile cha wanamtandao?
Kwani kuna uongo gani katika hayo aliyoyasema Bashiru?
Sent using Jamii Forums mobile app
Chuo Kikuu Dar es salaam na pia alikuwa mchambuzi wa mambo ya siasa kwenye vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa vinamtafutaDr Bashiru kabla ya kuwa Katibu mkuu wa CCM aliwahi pia kuwa katibu mkuu wa chama gani?
WATU WANA IMANI NA UCHAGUZI,BUNGE LINA HESHIMA! Kauli za uchochezi hizi.January 19, 2020
'BAADA YA MZEE KIKWETE KUINGIA KURA ZETU ZILIANZA KUPOROMOKA, CHAMA KILIPATA MSUKOSUKO'' BASHIRU
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru anaichambua safari ya kisiasa ya CCM toka mwaka 2015, ambapo kura za CCM ziliporomoka na Magufuli alipata 58%. Fitna na misukosuko ikawa jadi ya chama. Wasemakweli wakawa maadui wa chama na kupelekea kuitwa na Halmashauri Kuu ya Chama NEC wakapewa adhabu na wengine kufukuzwa . wanaCCM wenye nia njema wakaanza kukaa kando na chama kikaanza kuendeshwa na wachache wababaishaji. Watu wanapata kazi ndani ya CCM bila ujuzi wanapata nafasi hizo kiushikaji. Miradi mingi inayohusu watu (Maendeleo ya Watu) ikafa. Hata idadi ya wapiga kura ikaanza kuporomoka kutokana na wananchi kukosa imani na CCM. Watu hawana imani na vyombo vya kusimamia uchaguzi chini ya serikali ya CCM.
Dkt. Bashiru katika kikao hicho na wanaCCM anasema wote tunaona Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wanaimani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana.
Mkazo ktk Maendeleo ya Watu umezidi kusisitizwa sambamba na Maendeleo ya Vitu chini ya Awamu ya Tano.
Bashiru anaendelea kujadili na kuwaomba rai wanaCCM tusibishanie ndege, flyovers, madaraja na SGR reli Mpya maana sote tunaona Maendeleo hayo ya Vitu na Maendeleo ya Watu hivyo tusikazanie ktk kitu 'matumaini', bali vitu halisi tunavyoviona na kuvishika. Matumaini ni matamanio kama mapenzi huwezi kuvipima au kuvishika na hayana uhalisia hivyo haya Maendeleo ya Vitu kama ndege ni maendeleo dhahiri tusiyabishanie.
Bunge limekuwa na heshima hakuna vurugu. Demokrasia na Haki za binadamu imezidi kuzingatiwa kama ilivyoainishwa na Katiba yetu ya nchi. Chaguzi kama za Serikali za Mitaa November 14, 2019 chini ya wizara ya TAMISEMI zimefanyika bila vurugu na CCM imeshinda kwa kishindo asilimia 98%.
Source: Millard Ayo.
Hapa anatafuta "justification" maana kabla ya kuwa katibu mkuu alikuwa anaikosoa sana serikali na alivyoingia Magu wakampa ukatibu mkuu. (hapa amejibu indirect tatizo ilikuwa ni Kikwete na genge lake)Wametafuta ugomvi nje ya CCM imeshindikana. Sasa wanaanza kutafuta ugomvi ndani ya CCM yenyewe. Wanachotafuta watakipata muda so mrefu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi nikianza form one mwakani inaweza kunichukua miaka mingapi ili niwe na PHD, Msaada tafadhali.