Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: CCM mwaka huu itavunja rekodi kwa kupata ushindi mkubwa wa kihistoria kwa sababu tunashindana na vyama dhaifu sana!

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: CCM mwaka huu itavunja rekodi kwa kupata ushindi mkubwa wa kihistoria kwa sababu tunashindana na vyama dhaifu sana!

Katika watuambao leo.hii ingekuwa mimi ndio mwenyekiti wa ccm ningewapiga chini ni huyu bashiru na polepole
Huyo mwenyekiti mwenyewe ni afadhali hata ya hao kina Bashiru, yeye hajawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba 10.

Jk ndio mwanasiasa, alipoona mamba hayaendi sawa aliishawishi kamati kuu ya ccm yote ijiudhuru ili apewe na nafasi ya kuiunda upya.
 
Kwao jimbo linachukuliwa na CHADEMA asubuhi alafu anatuletea porojo zake sasa eti upinzani dhaidlfu
 
Bashiru na Polepole ndio wameiuwa CCM, wametoa ushauri mbaya wa kuihujumu CCM.
1.Kununua wanaopigiwa kura badala ya wapiga kura.
2.Kutopeleka maendeleo majimbo ya upinzani mfano Arusha, Moshi, Manyara,Mbeya, Mara hili limesababisha CCM kuchukiwa huko.
3.Kuwatumia polisi kuwanyanyasa wapinzani, hii imeleta matokeo positive badala ya negative, hapa nawapongeza Sana polisi wamefanya kazi nzuri Sana ya kuibomoa CCM kwa miaka 5 kwa kuifanya CCM izidi kuchukiwa zaidi na wananchi juu ya matendo yao ya kuwaumiza wapinzani, hili la matumizi ya polisi ccm ndio wameloose zaidi na upinzani umejengeka zaidi maana watz awapendi uonevu kwa hili upinzani utapata kura nyingi Sana za watz wasiopenda uonevu kwa hili polisi washukuriwe Sana Sana kwa kazi nzuri ya kuujenga upinzani nchini.
4.Kutumia dola kuijenga ccm badala ya nguvu ya umma nguvu ya ushawishi, hii mbinu ikifaa miaka ya 70 na sio kizazi cha sasa chenye global vision kimeona yaliyotokea Malawi, Zimbabwe, Sudani, Tunisia huwezi ukakipropaganda mfu ni sijui Libya.
 
Sasa mbona rafu nyingi mapingamizi, kuenguliwa wagombea, kutekwa na kupigwa wagombea wasirudishe fomu, nafikiri ndio udhaifu anaouzungumzia, tukihesabu kura tutajua
 
Ccm ni chama dhaifu sana kwa sasa, hakiwezi ushindani kinategemea kubebwa na polisi ama tume kwa kuengua kihuni wapinzani na kumtangaza matokeo fake kwa nguvu

MWANDISHI: Baada ya kubaki siku 12 kuelekea uchaguzi mkuu, labda status ikoje kwa upande wa chama cha mapinduzi?

BASHIRU: Ni ushindi mkubwa sana, unajua mwaka huu tumeshindana na vyama dhaifu kuliko wakati wote. Sasa vyama dhaifu hata vingekuwa na wagombea wazuri lazima pia utendaji wao uendane na uwezo wa vyama vyao kwa hiyo mwaka huu ukilinganisha na mwaka 2015 tumeshindana na vyama dhaifu.

Kwa mfano ACT ni chama kipya, chama kilichokuwa na mbunge mmoja wa Kigoma mjini na halmashauri moja, hakikuwa na muwakilishi hata mmoja Zanzibar wala mbunge Zanzibar.

Kimesimamisha mgombea wa Muungano ambae sijui amepotelea wapi, namtafuta sijui yuko wapi? Ningekuwa ndie katibu wake mkuu ningeshaenda polisi, sasa hao ndio tunaoshindana nao.

Wengine ambao wanajikakamua vyama ni dhaifu, kulikuwa na chama ambacho kilikuwa kidogo kimejiimarisha cha CHADEMA lakini kilikuwa na washauri wazuri waliokipa ushindi, wakina mzee Lowassa, mzee Sumaye wako CCM, wako majukwaani wanakitafutia kura.

Kwa hiyo mwaka huu tutegemee matokeo na ushindi ni mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi kwa hiyo tunashindana na vyama dhaifu, vyama vilivyogawanyika, vyama vipya.

Sisi ni chama kikongwe, chama imara, chama ambacho kina umoja zaidi na kinachotupa nguvu ni kwamba mwaka huu hatuna migogoro ndani ya chama, tumeshikamana na hiyo umeiona wakati tunateuana.

MWANDISHI: Kati ya wagombea kuna mgombea gani tishio?

BASHIRU: Hakuna tishio hata mmoja, nimeshakwambia kwamba vyama vyote ni vipya na vyama vyote ni dhaifu kwa hiyo hatuna mgombea tishio
 
Ushindi upi? Bado mna ndoto za kuiba kura tu?
Awamu hii tutajua mbivu na mbichi
Utafanyaje wewe mnyanyembe,zaidi ya kukimbilia kulalamika mitandaoni?
na uchaguzi ukiisha ni marufuku siasa mpaka uchaguzi ujao,taarifa ya habari ndo hiyo.
 
Ni kweli ni vyama vipya vyote
mfano 2015 Chadema ilionekana ina nguvu mno lakini ni kwa sababu kwanza ilibebwa na wanasiasa nguli mobilizers akina Slaa,Lowasa na Sumaye na Profesa Baregu ambao walikipaisha hadi kufikia kukubalika na vyama vyote vya upinzani na kuweza kuviunganisha kwenye UKAWA hivyo kukifanya CHADEMA kiwe kama chama cha kitaifa kwa muda.

Chadema kilvutia wanasiasa mahiri toka vyama vyote vikubwa iwe CCM,CUF nk

Pia kilikuwa na mvuto mkubwa kwa makundi makubwa muhimu katika jamii kama viongozi wakuu wa kidini na waumini wao wa dini kubwa

Pia makundi makubwa ya wafanyabiashara wakubwa walikiunga mkono
Mafisadi yalijazana Chadema

Vita ya ufisadi iliwabeba sana kuliko kawaida lakini walipowapokea mafisadi CHadema ikapoteza mwelekeo agenda kuu ya kuweka raisi ilikuwa kupambana na ufisadi sasa hivi agenda yao ni weka Lisu ambayo ni very weak agenda!!! Ile ya pambana na ufisadi ilikuwa imetulia ndio maana iliungwa mkono na watu wa rika zote tofauti na Chadema ya sasa yenye mikutano inayojaa vijana wadogo watupu ambao ndio wamefikisha umri wa kupiga kura sasa hivi na ambao wengi hawana vitambulisho vya kupiga kura huenda tu kuangalia matukio

CHADEMA si tu ni chama kipya bali kina washabiki wapya vijana wapya ambao 2015 walikuwa hawajafikia umri wa kupiga kura.Ukiona watu watu wazima ujue ni viongozi wa chadema wa mashina au ofisi zake

UKAWA baada ya Chadema kuusambaratisha mhanga namba moja amekuwa CHADEMA.Dar es salaam na mikoa ya pwani vyama vyenye nguvu kubwa sana ni CCM,CUF na ACT wazalendo.Chadema UKAWA waliwachukua CUF wakaiteka DAR KUVUNJIKA UKAWA tumeona uzinduzi wa CHADEMA ulivyododa.Kwa hiyo DAR NZIMA SAFARI HII CHADEMA inafungishwa virago,CUF virago na ACT wazalendo virago sababu UKAWA haupo tena

Sasa hivi yale makundi makubwa yaliyoondoka na Sumaye na LOWASA na Dk SLAA yako CCM YANASUBIRI tarehe 28 october yawaonyeshe Cha mtema kuni CHADEMA KWA HASIRA kwa kuwafukuza watu wao akina SLAA (Bababti) Sumaye (Manyara) Lowasa (MONDULI +ARUSHA) na makundi yao waliyokuwa nayo walipokuwa CHADEMA

Huu uchaguzi mwepesi sababu wagombea ni sura mpya zinazotafuta kura kwenye mgawanyiko mvunjiko wa UKAWA.WASHINDANE WAO KWA WAO KWANZA halafu ndio wageukie CCM ushindi hapo kwao hakuna.
Umenichekesha mkuu, uko timamu na serious kweli??

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Kama maneno hayo yametamkwa na Bashiru, basi ni dhahiri tunao watu wanaitwa madokta lakini bado wanaendelea kuwa wajinga, kwa sababu ya unafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWANDISHI: Baada ya kubaki siku 12 kuelekea uchaguzi mkuu, labda status ikoje kwa upande wa chama cha mapinduzi?

BASHIRU: Ni ushindi mkubwa sana, unajua mwaka huu tumeshindana na vyama dhaifu kuliko wakati wote. Sasa vyama dhaifu hata vingekuwa na wagombea wazuri lazima pia utendaji wao uendane na uwezo wa vyama vyao kwa hiyo mwaka huu ukilinganisha na mwaka 2015 tumeshindana na vyama dhaifu.

Kwa mfano ACT ni chama kipya, chama kilichokuwa na mbunge mmoja wa Kigoma mjini na halmashauri moja, hakikuwa na muwakilishi hata mmoja Zanzibar wala mbunge Zanzibar.

Kimesimamisha mgombea wa Muungano ambae sijui amepotelea wapi, namtafuta sijui yuko wapi? Ningekuwa ndie katibu wake mkuu ningeshaenda polisi, sasa hao ndio tunaoshindana nao.

Wengine ambao wanajikakamua vyama ni dhaifu, kulikuwa na chama ambacho kilikuwa kidogo kimejiimarisha cha CHADEMA lakini kilikuwa na washauri wazuri waliokipa ushindi, wakina mzee Lowassa, mzee Sumaye wako CCM, wako majukwaani wanakitafutia kura.

Kwa hiyo mwaka huu tutegemee matokeo na ushindi ni mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi kwa hiyo tunashindana na vyama dhaifu, vyama vilivyogawanyika, vyama vipya.

Sisi ni chama kikongwe, chama imara, chama ambacho kina umoja zaidi na kinachotupa nguvu ni kwamba mwaka huu hatuna migogoro ndani ya chama, tumeshikamana na hiyo umeiona wakati tunateuana.

MWANDISHI: Kati ya wagombea kuna mgombea gani tishio?

BASHIRU: Hakuna tishio hata mmoja, nimeshakwambia kwamba vyama vyote ni vipya na vyama vyote ni dhaifu kwa hiyo hatuna mgombea tishio
Ni kinyume chake.
 
Chemical Ali waziri wa propaganda wa Sadam Hussein alikuwa anasema wanajeshi watiifu wa serikali wameliangamiza kabisa jeshi la Marekani kumbe wakati huo Sadam Yuko chini ya shimo Kama panya.
 
Back
Top Bottom