Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi), alizeti, n.k. Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Soma pia:

Thread 'Kukataa Wazo la REA Kujiusisha Kwenye Sekta ya Mafuta' https://www.jamiiforums.com/threads/kukataa-wazo-la-rea-kujiusisha-kwenye-sekta-ya-mafuta.2262255/
 
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 Hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi). Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinaififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Hii ni kawaida sana kwa viongozi waliolewa madaraka. Huweka sheria na kanuni bila kujali athari zake kwa wananchi. Wanajifikiria wao tu. Ndiyo maana kila siku tunasema bila kubadilisha uongozi ni bure.
 
Aisee wakati wanatunga sheria walitumia reasoning yoyote kweli?
Ni hivi: Madaraka yanalevya na viongozi wakishalewa madaraka hufanya mambo bila kujali athari zake kwa wananchi. Hii ni kanuni ambayo kuikwepa dawa yake ni kubadilisha uongozi tu. Kiongozi akishajua kuwa akivurunda ataondolewa hawezi kubweteka. Tatizo la CCM ni kuwa wanajua hata wakivurunda hawataondoka kwani watatumia nguvu. Dawa ni wananchi kuungana na kuwaondoa. Wakija wengine wakivurunda nao wanaondolewa.
 
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 Hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi). Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinaififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Kuna vidumu maalumu vya petrol waruhusu hivyo, kwa mfano hapo wizarani kwake akitaka mafuta ya Generator anapataje ? wasitufanye watanzania mbumbumbu..

can2.jpg
 
Back
Top Bottom