Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi), alizeti, n.k. Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Soma pia:

Thread 'Kukataa Wazo la REA Kujiusisha Kwenye Sekta ya Mafuta' https://www.jamiiforums.com/threads/kukataa-wazo-la-rea-kujiusisha-kwenye-sekta-ya-mafuta.2262255/
Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.
 
Badala ya kudhani wamepata suluhu kumbe wameongeza tatizo
 
Badala ya kudhani wamepata suluhu kumbe wameongeza tatizo
Huku mitaani kuna mapipa au madumu madogo ya bati (siyo Jerry cane) ndiyo wanaruhusu kununulia mafuta kwa sasa.
Haya mapipa hayajazuia biashara ya mafuta ya videbe. Yale ya kuweka kwenye chupa za maji za lita1 au nusu lita. Wanatunza majumbani ovyo kama kawaida.
Kwahivyo lengo la kuzuia hatari itokanayo na uuzaji mafuta holela halijatimia.
Limetimia lengo la waliotajwa kufanya biashara yao ya madumu/mapipa ya bati/chuma.
Hii nchi sijui itajiondoa lini kwenye utumwa wa mafisadi waliovaa koti la wanasiasa. Vijijini kote wanasema hiyo biashara ya watu siyo kuhusu usalama wa raia.
 
Naomba kusaidiwa taarifa - kwa hapa Dar wapi hizo Jerry can za chuma zinauzwa?
Nenda kaulizie maduka ya mashine na vipuri vya mashine mbalimbali kule Ilala CBD Posta, Morogoro road.
Barabara ya BRT (mwendokasi).
 
Back
Top Bottom