Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Acha wafanye wanavyotaka,maana watz wengi. ndivyo tulivyo.
Maisha magumu acha ayaseme Mbowe,wengine endeleeni kujifungia ndani.
Na kelele nyingi zinapigwa nyuma ya kibodi🤣🤣🤣.
Tena kama nyie wa vijijini ndo hamfai kabisa🦻.
Wachache wanajielewa.
Kuna watu bado Wana tishert za 2010 za kikwete wanazitinga🤣
Unaweza kuwa una hoja lakini siyo mahala pake.
Ingependeza ungeshauri nini kifanyike kuondoa tatizo nililoleta hapa.
Mimi ni mkazi wa Dar lakini natafuta mkate shambani vijijini.
 
Niliwafikiria watunga sheria , nikajua wanapiga marufuku magaloni ya plastick lakini labda kuna cane maalumu za alminium au chuma zipo zimeanza kuingia special kwa wanaobeba mafuta kwaajili ya shamba na sehemu nyingine za mbali kumbe wapi, haya vijiji vingi havina fuel station , hii maana yake wenye powertillers, bodaboda, trekta , bajaji waliopo vijijini wafanyeje?
Kuna sheria mpya inaruhusu mwenye mtaji mdogo sana kufungua fuel station vijijini, hakuna tena ule utaratibu wa umbali mkubwa kati ya kituo kimoja hadi kingine.
Pia hakuna kile kigezo cha mtaji mkubwa.
Tatizo linakuja hata kama kila Kijiji au kitongoji kuna fuel station bado mwenye mashine hawezi kuibeba kwenda kujazia mafuta fuel station.

Ningeshauri waagize kila mtaa au Kijiji viongozi wasimamie watu wasiuze mafuta ya kwenye madumu na chupa za maji maarufu kama mafuta ya videbe.
Waruhusiwe kununua kwenye madumu au/na Jerry cane kwa matumizi binafsi.
 
Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.
Mkuu hizi sheria ni wao wameamua tu lakini duniani kuna utaratibu hata kama ni nchi za magharibi wana utaratibu wa kununua mafuta ila kama wanataka wafanye kama huku nje
Kuna madumu ambayo bila hayo huwezi kuwekea mafuta
Dumu la kijani dogo kwa ajili ya Petrol na kubwa jekundu kwa ajili ya Diesel
Mbona miaka ya nyuma yalikuwepo na kukikuwa hakuna tatizo
Hatuwezi kuwa na sheria na zikawa rafiki why?
Kila kitu Kama tumeiga kwa mzungu kwa nia nzuri basi ziendelee hivyo hivyo

Wanipe tenda niyajaze huko
Screenshot_20240930_094056_Google~2.png
Screenshot_20240930_094006_Google~2.png
 
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 Hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi). Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinaififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
REA walione hili, haiwezekani hadi leo watu wanatumia mashinanza maafuta kisaga na kukoboa, ilihali umeme tunaao wa kutosha
 
REA walione hili, haiwezekani hadi leo watu wanatumia mashinanza maafuta kisaga na kukoboa, ilihali umeme tunaao wa kutosha
Mkuu kuna dharula barabarani, majenereta, n.k.
Kuna shughuli za kilimo au migodi midogo nje ya makazi ya watu maporini huko ambako REA hawawezi kupeleka umeme kwa watu wachache sana au mmoja.
Mimi nipo nje ya Kijiji mbali nimejitenga niweze kufuga na nguruwe bila kero kwa watu.
 
Naiona nyororo Ile ya zamani ikirejea...ilipelekea chopa ya jeshi kutua pale

Wamiliki wamalori,tujiandae kiakili malori kuanza kundondoka hovyo maeneo yasipotakiwa kundondoka
 
REA walione hili, haiwezekani hadi leo watu wanatumia mashinanza maafuta kisaga na kukoboa, ilihali umeme tunaao wa kutosha
REA kuhangaika na mafuta ni Sasa na Daktari kumuuzia mgonjwa dawa,wakati Kuna Pharmasia.

REA wamesambaza umeme na kuweka transformers ndogo, matumizi ni makubwa,tumeishia kwenye low voltage.

Nguzo wameweka za miti ,mchwa wameamza kuzila badala ya kuweka nguzo za zenge.

Sasa wataanza Tena kuondia nguzo za miti kuweka za zenge ni mradi na Kodi zetu.

Sasa waanze Tena kuuza mafuta???
 
Wasambaze.
Sasa hayapatikani kirahisi kama zamani.
Waruhusu madumu kwa muda ila iwe kwa muda maalumu wakati wanasambaza hayo maalum.
Mbona iliwezekana kwenye mifuko ya plastic na pombe za viroba.
Hukatazwi kununua mafuta kwenye kidumu bali kuna kidumu maalum kwa ajili ya petrol na diesel. Hili sio jipya. Huwezi kwenda kununua mafuta na dumu la maji ya uhai.
 
 
Mkuu kuna dharula barabarani, majenereta, n.k.
Kuna shughuli za kilimo au migodi midogo nje ya makazi ya watu maporini huko ambako REA hawawezi kupeleka umeme kwa watu wachache sana au mmoja.
Mimi nipo nje ya Kijiji mbali nimejitenga niweze kufuga na nguruwe bila kero kwa watu.
Ni sawa kwa upande wa dharura ,ila kilimo na migodini REA ipeleke umeme, hadi wewe mfuga nguruwe huko porini, unatakiwa ufikiwe na umeme, umeme tunao mwingi hadi tunafungulia mabwawa..
 
Ni sawa kwa upande wa dharura ,ila kilimo na migodini REA ipeleke umeme, hadi wewe mfuga nguruwe huko porini, unatakiwa ufikiwe na umeme, umeme tunao mwingi hadi tunafungulia mabwawa..
Mindset ya haya mashirika bado ipo nyuma karine nzima.
Wanataka faida badala ya huduma.
Hawawezi kuniletea umeme mtu mmoja 6KM kutoka kijijni, ukizingatia mimi mwekezaji mdogo ni start-up.
Sijaanza kufanya return yoyote ya investment.
 
Wasambaze.
Sasa hayapatikani kirahisi kama zamani.
Waruhusu madumu kwa muda ila iwe kwa muda maalumu wakati wanasambaza hayo maalum.
Mbona iliwezekana kwenye mifuko ya plastic na pombe za viroba.
Ni kweli hayo madumu hayapatikani kirahisi.
 
Kuna vidumu maalumu vya petrol waruhusu hivyo, kwa mfano hapo wizarani kwake akitaka mafuta ya Generator anapataje ? wasitufanye watanzania mbumbumbu..

View attachment 3110781
Usikute kuna mtu anataka kuleta biashara ya kuuza hivi vidumu. Kuna sehemu mtu yeyote anayenunua mafuta mkononi anatakiwa awe na dumu hili. Sehemu yoyote ya ujenzi inayotumia mafuta inatakiwa kuwa na dumu hili. Kuna mtu kaona fursa.
 
Kaka mimi mwaka huu huu wakati mafuta yamekuwa adimu nmeishiwa mafuta kwenye generator nikatuma boda sheli wakamkatalia wanasema aje na chombo husika ikabidi aje afunge generator aende nalo ndo wakamuuzia
Haya mambo ya ajabu kabisa.
Generators kubwa kabisa zile zinafungwa na mounting bolts au studs utafungua nati kisha utafunga kwenye boda au kwenye gari kisha ukafunge tena ukitoka sheli?
Mashine yangu ya maji ni kubwa kama power tiller za kulimia au mashine za kusaga, inabebwa na watu wanne au zaidi nifungue na kufunga tena?
 
Back
Top Bottom