Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

Dkt. BITEKO na EWURA, Zuio la kuwauzia mafuta wateja wenye dumu (gallon) linaleta maafa vijijini kwa wakulima wanaotumia mashine za diesel na petrol

ukitaka mafuta ya generator unabeba generator lako unapeleka sheli ?
 
Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?
Wanataka mtumie hii🐼👇

1000012755.jpg
 
Niliwafikiria watunga sheria , nikajua wanapiga marufuku magaloni ya plastick lakini labda kuna cane maalumu za alminium au chuma zipo zimeanza kuingia special kwa wanaobeba mafuta kwaajili ya shamba na sehemu nyingine za mbali kumbe wapi, haya vijiji vingi havina fuel station , hii maana yake wenye powertillers, bodaboda, trekta , bajaji waliopo vijijini wafanyeje?
 
Hilo sio zuio, ni ukweli.
Petrol ni maafa, isioo hifadhiwa vizuri.
Tangu enzi za mkapa walikuwa wanstumia mbinu Gani kupata hayo mafuta
Huu ni mradi wa kijinga mnataka kubuni au kuanzisha.
Ewura wanafanya kazi nzuri ni kibano kibakie hapo hapo
 
Hilo sio zuio, ni ukweli.
Petrol ni maafa, isioo hifadhiwa vizuri.
Tangu enzi za mkapa walikuwa wanstumia mbinu Gani kupata hayo mafuta
Huu ni mradi wa kijinga mnataka kubuni au kuanzisha.
Ewura wanafanya kazi nzuri ni kibano kibakie hapo hapo
Tusaidie wewe watumie mbinu gani kupata hayo mafuta wakayaweke kwenye magenereta yao au mashine zao nyinginezo
 
Watafute njia mbadala,sisi wenye vigari vyetu tusioweza kujaza full tank kuna mida kigari chako kinakuishia mafuta maporini huko,hivi vipetrol station bubu vya vidumu ndio mkombozi wetu...
 
Tatizo uwezo mdogo wa viongozi wetu.Hawaangalii mambo Kwa upana.wao wanaangalia mazingira Yao tu yanaowazunguka.Mimi Huku kijijini Nina makarasha yangu ya kusaga mawe ya dhahabu ambapo mafuta Huwa nafata Kwenye madumu kilomita 50 kwenda mjini.Hii Hali ya kuzuia madumu imenichanganya maana nimejiajiri hapa kwenye mradi wangu ninaoupenda.Kutuletea umeme kijijini hamutaki na mafuta kubeba kwenye madumu na hiyo hamutaki.Hivi huyu kizimkazi anajua maana ya uongozi kweli?
 
Kama tuliku tuna nunua petrol, mafuta ya taa na dizel hadi kwenye mabobo ya maji ya kunywa na kwenye chupa za soda na hatukupata madhara yeyote sasa kwa akili ndogo sana Ukiachana na habari za vijijini . Swali dogo na la kijinga la kujiuliza ni vipi kama generator likiisha mafuta. je, tutalibeba na kwenda nalo huko kwenye station wanako jazia mafuta ?

Nb: Au kuna biashara za mabepari za magoni ya kubebea mafuta wanatafuta soko kwa nguvu?
 
Mara kadhaa huwa nasema humu Tanzakiza Kuna wapumbavu ambao ndo wapo kwenye ngazi za maamuzi/kimaamuzi.

"60% ya watumishi waliopo serikalini Wana uwezo mdogo"Prof Asad.
 
Hiyo sheria labda itemise dar tu sio huku vijiji kwetu au watu wa mwambao wa pwani ambao both zao zinatumia mafuta ya dizel au petrol mana huwezi kubeba mashine ukaenda nayo sheli kila siku ni usumbufu.

Chadema hawana makali hayo msiwaogope mana naona mnadhani kama vijana wao ndio wanunuaji wakuu kwa ajili ya maandano
 
Kuna hali mbaya inaendelea huku vijijini baada ya sheria, kanuni au amri ya kukataza wananchi wanaoenda vituo vya kuuzia mafuta na dumu au galoni wasiuziwe mafuta.

Hii sheria au amri haikuzingatia maisha halisi ya nchi masikini kama Tanzania.

Kuna mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kusindika vyakula vya binadamu na mifugo, mashine za kilimo cha umwagiliaji ambazo zinatumia nishati ya diesel au petrol.

Huwezi kubeba hizi mashine kwenda nazo petrol filling station ( sheli ).
Mimi nafanya kilimo cha umwagiliaji kutumia mashine kubwa ambayo ipo fixed, mounted karibu na chanzo cha maji. Bado kidogo nipate hasara baada ya kukosa mafuta. Mashine hii pia naitumia kupandisha maji kwenye mabanda ya mifugo na makazi yaliyopo juu mlimani.
Nilikosa maji siku 4 Hali ilikuwa mbaya.

Imenilazimu kununua mafuta ya uchochoroni kimagendo ambayo ni hatari. Pia yanaweza kuwa machafu yakaharibu mitambo. Mafuta haya huchangia wizi wa mafuta na serikali inakosa kodi.

Nawaomba mtume watu vijijini kupata hali halisi. Kuna watu watapata hasara kubwa au kupoteza maisha kwa kukosa mafuta.

Huku shamba kuna watu wamejiajiri na kuajiri kwenye biashara za kukamua mafuta ya mawese(ya chikichi). Wanatumia diesel kazi zimesimama.
Watu wote hawana gari za kwenda kununulia diesel sheli na wengi hawajui kwa kupata mafuta ya magendo.

Najiuliza ikitokea dharula yoyote gari ikaishiwa mafuta njiani itakuwaje endapo hawataweza kuletewa mafuta kwenye madumu?

Najua Kuna utaratibu mpya wa kutoa leseni ya kujenga vituo vidogo vya watu wenye mtaji mdogo vya kuuza mafuta vijijini. Lakini bado mteja mwenye mashine atakatazwa kwenda na dumu kununua mafuta, na mashine hawezi kwenda nayo kituoni atafanyeje huyu mteja?

Sheria zetu zingine zinaififisha juhudi za kukuza uchumi wetu sekta ya kilimo.
Changamotoo sana hamna wakututetea inaumiza sana wakulima huyu aliyetunga sheria hii Mungu anamuona
 
Acha wafanye wanavyotaka,maana watz wengi. ndivyo tulivyo.
Maisha magumu acha ayaseme Mbowe,wengine endeleeni kujifungia ndani.
Na kelele nyingi zinapigwa nyuma ya kibodi🤣🤣🤣.
Tena kama nyie wa vijijini ndo hamfai kabisa🦻.
Wachache wanajielewa.
Kuna watu bado Wana tishert za 2010 za kikwete wanazitinga🤣
 
Back
Top Bottom